Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,273
- 25,297
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, amesema wanafuatilia kwa Spika wa Bunge ili asaini nyaraka zitakazowezesha kufikishwa mahakamani viongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kukaidi agizo lililowataka wawasilishe mikataba 26 ya gesi asilia mbele ya kamari hiyo ili ikaguliwe.
Wakati Zitto akisema hayo, kuna taarifa kwamba Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ina mpango wa kuzishughulikia halmashauri zinazotuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma kwa mtindo unaoendeshwa na PAC.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), aliyasema hayo alipozungumza na NIPASHE katika viwanja vya Bunge, mjini hapa jana.
Alisema hatua yao hiyo inalenga kudai taarifa za mapitio na mikataba 26 iliyoingiwa kati ya serikali na wawekezaji katika nishati hiyo.
Zitto alisema agizo la PAC kwa TPDC lilitolewa tangu Januari 26 mwaka 2012, lakini hadi sasa halijatekelezwa.
Jumatatu wiki hii, PAC iliamuru polisi kuwaweka rumande Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, Michael Mwanda, kwa kukaidi agizo hilo la PAC.
Andilile na Mwanda walikaa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi jijinu Dar es Salaam kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa bila sharti lolote.
"Kwa sasa tunafuatilia Spika asaini hati ili tuwafikishe mahakamani. Mikataba lazima wataitoa tu," alisisitiza Zitto.
CHANZO:NIPASHE
http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=73933