Zitto atua Dodoma kuinadi ACT

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698

Zitto-Kabwe ACT.jpg
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto anatarajia kuanza ziara ya siku moja mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwa mikoa 10 nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Katibu wa ACT-Wazalendo wa Mkoa, Denis Nyandwi alisema lengo la ziara hiyo ni kutambulisha rasmi chama hicho kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma.

"Pia ziara yake hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ili wajiandikishe kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura ili waweze kushiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao."

Alisema uongozi wa chama wa mkoa ukiongozana na vikundi mbalimbali vya ngoma utampokea rasmi kiongozi huyo katika eneo la Gairo, kesho na atapitiliza moja kwa moja kwenda wilayani Bahi.
"Akishapokewa na uongozi wa mkoa ataelekea moja kwa moja wilayani Bahi katika Kijiji cha Chiduo ambacho chama chetu kilishinda katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo atapata fursa ya kuzungumza na wananchi ambapo atavikwa uchifu wa kigogo na baadaye atarudi Dodoma Mjini na kuhutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Mashujaa," alifafanua.

Alisema kiongozi huyo wa chama atashiriki katika chakula cha jioni sanjari na kushiriki kwenye mkutano wa ndani wa kuchangia ziara yake kutoka kwa mashabiki, wapenzi na watu wenye mapenzi mema na chama hicho.

Mwenyekiti wa Mkoa wa ACT -Wazalendo, Eva Kaka alisema wanajivunia ushindi wa kishindo ilioupata wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo kilishinda na kutwaa uongozi wa Serikali katika kijiji cha Chiduo na kuwataka Watanzania watarajie ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.

"Tuna uwezekano mkubwa wa kushinda viti katika ubunge na madiwani zaidi ya 30 kwa Mkoa wetu wa Dodoma, hii itawezekana kwa sababu tumejipanga kutoa elimu ya upigaji kura na ile ya uraia kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma," alisema Kaka.

Mratibu wa ziara hiyo kwa Mkoa wa Dodoma, Steven Shekulukai alisema maandalizi kwa ajili ya ziara hiyo yamekamilika. Aliomba vyombo vya habari nchini kushiriki kikamilifu kukitangaza chama kifahamike zaidi kwa wananchi.

CHANZO: Habari Leo
 
Watanzania wanataka kusikia habari ya Katiba mpya kama inafaa ama haifai, Tume huru ya uchaguzi, Uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na Uchaguzi mkuu mwezi October - sasa mtu mwingine eti anatanganza chama chake kipya!!
 
Kwa Dodoma hawezi kutudanganya lolote aende zake Kigoma huko.dodoma hatutaki watu wanaoeneza udini na wanajisifia maisha yao.sisi na CCM au wengine UKAWA basi.
 
akili zako zimeishia hapo au mbege za mchana?

Ukweli ndo huo na Dodoma ZZK anakuja kupiga mayowe tu hatuna muda nae sisi sio kijiwe chake cha Urusi na meza ya duara vilivyopo kigoma ambavyo amewashikia akili mpaka na wake wao.hatuhingwi na matisheti yake.
 
Aje Dodoma tu kuangalia magoroja yake na si kutudanganya watu dodoma,uongo wake apeleke mwandiga na mwanga.
 
ACT ndio chama bora kwa sasa, hiki chama kitakuja kuchukua nchi siku zijazo..."I have a dream, that one day ACT will take the control of our government"
 
Vyama vya majina ya kizungu haya hatuvitaki kabisa. Bora CCM iendelee kutawala kama CDM ikishindwa. Hatutaki kuhudumia matumbo ya watu hapa Wananchi tumecoka. Habari za ZZK sio mpya. Ni sawa na alikokuwa
 
Ukweli ndo huo na Dodoma ZZK anakuja kupiga mayowe tu hatuna muda nae sisi sio kijiwe chake cha Urusi na meza ya duara vilivyopo kigoma ambavyo amewashikia akili mpaka na wake wao.hatuhingwi na matisheti yake.

nyie mmeshikwa akili na CCM?
 
ZZK ni mpiga zumari wa CCM ... Ruzuku yote inatoka CCM... Maandalizi ya mikutano yao inaratibiwa na CCM ,...
Watanzania wanataka kusikia habari ya Katiba mpya kama inafaa ama haifai, Tume huru ya uchaguzi, Uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na Uchaguzi mkuu mwezi October - sasa mtu mwingine eti anatanganza chama chake kipya!!
 
Back
Top Bottom