Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Bunge kutoa adhabu ya kumsimamisha vikao vya Bunge lote la Bajeti Waziri Kivuli wa Fedha ndg. Halima Mdee ni mwendelezo wa kukandamiza mawazo mbadala.
Wengine wote wamesamehewa au kupewa karipio Kama kiini macho tu. Hii ni Bajeti ya pili mfululizo Waziri Kivuli wa Fedha anasimamishwa. Mdee aliomba radhi hadharani ndani ya Bunge wala sio kwa kujificha, anasimamishwa kuhudhuria vikao.
Walioomba radhi vyumbani wanasamehewa. Hakuna uzandiki ulio uzandiki mkubwa Kama huu. Huu ni mpango maalumu kuzuia Waziri Kivuli wa Fedha kufanya kazi yake wakati huu ambapo Ndio haswa wakati wake. Maamuzi haya ya Bunge ni ya hovyo na yanadhalilisha Bunge.