Hivi mtoa hoja kabla ya kumuhusisha zito pekee Kwa hilo ukimfikiria tu pinda utendaji wake yuko sahihi? Mfano juzi mhe.Lugola alivokuwa anampa makavu laivu alikuwa wapi mpaka madudu yote yanatokea habari za kitelegencia hazikumfikia? haingii akilini nilichosikitika zaidi baadae nilitegemea yeye atajiuzulu kumbe anatangaza wenzie kusitishwa uwaziri wao sasa cha kujiuliza anaowatangaza wakina nani na yeye nani tena anaonekana hajutii hata uzembe wake inasikitisha kuwa na waziri mkuu wa namna hiyo mawaziri watatu wanaondolewa kwa kashfa kama hizo yeye ajione hana tatizo, tatizo analo nashindwa kumuelewa hajielewi au anajibaraguza.
Wanawake wamebakwa, wamezalilishwa, wamewekwa vilema vya maisha, wengine wamepoteza maisha inasikitisha, inahuzunisha tena sana sikuwahi kufikiri hata siku moja kwa tanzania hii ya sasa yaha mambo bado yapo. Kama wewe unaona zito anamuonea Mhe. Pinda si kweli zitto unamsikia kwa vile anapo pakusemea wengine hatuna nasi ungetusikia.
Mhe. Lowasa sina mapenzi naye lkn alikuwa anaonesha yaani msisimko na jambo pia ana take action kwa hilo namsifu, mengine ni mapungufu yake lakini halikuwa mchapakazi.
Mhe. pinda ajiulize mara mbili mbili yuko sahihi na utendaji wake? ikiwa yeye alikuwa hajui kilichoendelea nani wa kumuuliza? kama mawaziri wanamdanganya ! Wakuu wa mikoa na wilaya wote wako chini yake pia hiyo hajui na wakati anaongea na Rais anamwambia madudu yaliotendeka tiyari ilikuwa swali moja tu lakumuuliza ulikuwa wapi haya hakitendeka? Ninamaswali mengi sina wa kunijibu juu ya hili lakini inasikitisha.