Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

dah yaani mbowe na lowassa na wanachadema kibao wamemkaushia....siasa ni ngumu sana
 
Naona hii nchi binaadamu ni Wanasiasa tu, hao Wapiga kura Gerezani huwa wanatembelewa lini? au mpaka Mwanasiasa aingie humo ndio Wanasiasa wenzake wakamsabahi?
 
Zitto nowadays hapatikani kabisa FB
 
Awamu ya tano inaimatisha upinzani kwa stahili ambayo baadae watashindwa kbs kuudhibiti....maana wanatengeneza watu jasiri,watakaokuwa tayari kupambana,kukaa jela na hata kufa!muda utatuambia!
 
Kuna vitu wanasiasa wetu wanatakiwa kijifunza kutoka kwa Zitto lakini cha ajabu kuna baadhi ya pro-Chadema watakuwa wamechukizwa na hili.
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa Mahakama Zetu.
 
Zitto alivyo na siasa za bila kumtukana MTU
Wala kumvunjia heshima mtu

Alipaswa kumpa ushauri huo lema
Ili afanye siasa za akili na sio kutafuta kick kwa matusi
Acha ujinga mtochini, ebu tuambie matusi aliyotukana? Mh Zitto amesema tuko nyuma ya Lema kwa ajili ya kutafuta haki.
 
Mie natamani lema akae huko walau mwaka mmoja tu
Huyu kazidisha upuuzi
Ndio akili yako, kutamani wenzako wafe ili ufurahi, ujue na wewe yatakupata kabla jua halijachwea. Lakini kwa kuwa unawaju wanaomuweka ndani ongea nao, wamuweke huo mwaka ambao wewe na familia yako mtufutahi.
 
Ili kuendeleza solidarity kwelikweli na Ruyagwa atukane tukane viongozi wa nchi ili wakaungane gerezani. Lissu alitukana tukana, lkn amenyooshwa sasa ni mtu safi sana
 
Hongeta Zitto kwa ulichofanya, msife moyo katika kusimamia yale yaliyo kweli na kumweka mtanzania huru.
 
Tunazungumzia suala la haki za binadamu kama vile halituhusu, siku yakitufika na sisi ndipo tutakapoona umuhimu wa watu km lema, kama mnabisha tusubiri... Lkn tukumbushane wakati mikutano ya wanasiasa inazuiwa kinyume na katiba, Zitto aliwaambia waandishi wa habari. wakubwa wakitumaliza nyinyi mtafuata wakacheka, île sheria ya habari wakubwa wakiamua hata kesho watafunga vyombo vyote vya habari wanavyovichukia kwa mujibu wa sheria, ndugu zangu Uwovu tuupingeni ili usije ukaturudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…