Turbulence
Senior Member
- Apr 24, 2012
- 153
- 30
Wabunge wengi wanapenda posho. Kama una event unamwalika mbunge kamwe hatakuja kama huna posho! Na akifika usipompa posho basi ni ugomvi. Kama watoto. Mimi nimeyaona --- mara nyingi. Lakini pamoja na hayo, ninyi Zitto na Lema, acheni up.umbavu wa kutupiana mipasho hadharani. Kuna mambo mengi ya msingi ya kitaifa ya kuyajadili na kuyashughulikia. Kwa upande wangu, janga la kwanza la matumizi mabaya ya Serikali ni manunuzi (procurement). Zaidi ya asilimia 85 ya bajeti ya Serikali inatumika kwa manunuzi. Na huko ndipo wizi unapofanyika. Bei zinakuwa inflated hadi asilimia 1,000 (elfu moja). Sasa Zitto na wenzake waliangalie pia hili. La posho ni tatizo, lakini ni jepesi ukilinganisha na hilo la procurement. Again, achene upuuz.i wenu wa kupashana hadharani.
zitto katika facebook wall yake leo.
kuchukua au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi (principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho.
Sio posho tu, hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu, kwamba siwezi kuwa waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao.
Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu serikali haiwalipi walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu za afya huko vijijini nk.
Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.
Kuna single imetoka tunaambiwa kuna anazopokea gizani sijui laki 7, sijui milioni mara hela za mafuta na hoteli. hebu tuambieni ukweli wa tuhuma hizo, maana kama ni kweli atakuwa anatuchanganya sasa!
Zitto katika Facebook wall yake leo.
Kuchukua au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi (principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho.
Sio posho tu, hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu, kwamba siwezi kuwa Waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao.
Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu Serikali haiwalipi walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu za afya huko vijijini nk.
Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.
Mmebaki kupiga majungu ya kike bila ushahidi,zitto angekuwa anapiga kimya na nyinyi ushahidi mnao thubutu wachaga wangekesha mitandaoni kumwaga ushahidi ili aondoke kulinda shamba la mahindi(chadema)ili manyani yamalize kula mahindi .
Ya kwenu ccm yamewashinda. Mnachochea watu wafarakane CDM. Mmeula wa chuya. Wasaliti wanatupwa nje mkawape ubalozi na wanaokosea wanarudishwa kwenye mstari kulingana na msimamo wa CDM.Hapa upumbavu ndiyo unaosumbua watu kweli kila mtu anayo mapungufu yake lakini hawa wanaomsemea mabaya zito waseme zitto kafanya nini na wapi kama wakinipa mifano nitaelewa lakini kupanga kumchafua zito kijinga bila ukweli wowote ni upumbavu kamwe hawataweza kumwathiri zito kirahisi kwa uroho wao tu wa kutaka kuwa viongozi wa chadema wa milele.
mkuu unaweza thibitisha madai yako au ndo zile propaganda unaendeleza kwa masilahi binafsi kwenye mambo serious kama haya.yote haya watanzania tunayaona. na pia ni uzalendo kutoka kwa mzalendo mwenye uchungu na nchi yake.
shida iko pale anapokataa posho halafu anachukua mabilioni gizani, ambayo ndiyo malipo ya hovyo kabisa kupita zote. kuna maana gani ya kukataa posho za wazi halafu gizani anapokea mabilioni ambayo ni kodi za watanzania?
yote haya watanzania tunayaona. na pia ni uzalendo kutoka kwa mzalendo mwenye uchungu na nchi yake.
shida iko pale anapokataa posho halafu anachukua mabilioni gizani, ambayo ndiyo malipo ya hovyo kabisa kupita zote. kuna maana gani ya kukataa posho za wazi halafu gizani anapokea mabilioni ambayo ni kodi za watanzania?
...teh teh nayale mamilioni yaliyofichwa ujerumani ungeyakataa ningejua kweli wewe ni muungwana,kwa siri unatafuna,vinavyoonekana unavikana. Kumbuka wanaokusaidia ndo wanatoa siri ikiwa pamoja na mmoja wa wahasibu wa Mohamed enterprises jina kapuni kwa usalama wake...