Zitto ampongeza Rais Magufuli pamoja na Bodi ya rufaa za kodi

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,310
6,544
Andiko lake FB

"Uamuzi wa Bodi ya Rufaa za kodi kuhusu Kampuni ya African Barrick Gold ( ABG) ni uamuzi utakaokuwa na mafanikio makubwa kwa nchi. Wawekezaji waliokuwa wanaumia njia za kihasibu kukwepa kodi Tanzania wataminywa na itabidi wafikiri mara mbili. Hukumu hiyo inayotupa tshs 82 bilioni itatupa mabilioni mengi zaidi kwani sasa itakuwa ' a precedent'. Inajibu swali muhimu sana kwenye kodi za kimataifa ' Kwanini Kampuni yenye kuzalisha mapato Tanzania ilipe kodi nje ya Tanzania'. Tunaita ni BEPs ( Base Erosion and Profit Shifting) katika lugha ya harakati za kupinga ukwepaji kodi kutoka nchi zinazoendelea.

Nitakuwa mwizi wa fadhila nisipomshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuwezesha kuharakisha kesi za kodi. Uamuzi wake huo umesaidia nchi sasa na baadaye kwenye masuala ya ukwepaji kodi"
 
Magufuri ni sawa na Maisha na Maisha ni magufuri bila ya kurekebisha maisha viumbe vya tanzania vitakufa kwa njaa tu.
 
Inaonyesha signature yako ulii copy bila kuisoma. Usingekuwa na msimamo huo
Inatakiwa ukosoe panapostahiki na kusifu panapostahiki.......I'm still in the line of my signature....
 
BTW kushambulia na kukosoa are quiet different
Zote ni style za kuwekana sawa. Inategemea na mpokeaji ataichukuliaje hoja husika, kwa maneno yenye maana ileile.
Na mara nyingi wasiojiamini wanakimbilia kudhani anashambuliwa
 
Kwann watanzania kwenye masuala ya utaifa tuna tofautiana wakati inchi za wenzetu likifika suala la utaifa wanaweka tofauti zao pembeni wanapiga kazi ifikie wakati kama inchi tujifunze kupitia wengine mfano marekani wapo wamoja kwenye masuala ya utaifa kuliko vyama je umewai kuona pendera za vyama kwenye uchaguzi wa marekani zaidi ya bendera ya taifa lao Nakupongeza Mh John Magufuri kwa jitiada zako pia zitto kwa kuona na kupongeza matokeo mazuri katika ukusanyaji wa kodi safari bado ndefu ila kuna matumaini
 
Naona sasa kidoooogo vijana tunaanza kuwa na akili za kupevuka.
Maana naona siku hizi kama uchama unaanaza kupungua hivi kwenye mambo ya kitaifa.
Au tuseme wakosoaji wanaogopa watakosolewa wao?
Hii inatia moyo kidogo......
 
  • Thanks
Reactions: Mss
Back
Top Bottom