Zitto ampa mtihani Prof. Muhongo

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
98,016
Points
2,000

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
98,016 2,000
• Ashindwa kujibu hoja, adai si mtu wa kulumbana

na Ratifa Baranyikwa | Tanzania Daima


SIKU moja baada ya Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, kuibana serikali akiitaka ifafanue juu ya upotevu wa sh bilioni 86 za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amekwepa kuzungumzia suala hilo.

Wakati Waziri Muhongo akikwepa, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Jenerali mstaafu Robert Mboma, nao walishindwa kutoa ufafanuzi.

Katika taarifa yake juzi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), akinukuu taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyobaini upotevu wa mabilioni hayo pamoja na mambo mengine alimtaka Waziri Muhogo aeleze hatua alizochukua baada ya kukabidhiwa taarifa hiyo kuhusu maofisa waandamizi wa wizara waliohusika na wizi huo.

Hata hivyo katika hatua ya kushangaza, Waziri Muhongo, alipotafutwa kwa njia ya simu ili azungumzie juu ya upotevu huo wa mabilioni ya shilingi, alisema hana cha kujibu na kwamba taarifa hizo yeye hajazisoma.

Alipotakiwa kuelezea hatua alizozichukua yeye kama waziri dhidi ya wizi huo, Prof. Muhongo, hakuwa tayari bali alisema yeye sio mtu wa kulumbana na kwamba kama kuna fedha zimeibiwa kuna taratibu za serikali.

"Tuongee mambo ya maendeleo, kuna wengine kulumbana ni kazi yao; sisi wengine taaluma zetu sio hizo," alisema Prof. Muhongo.(Mhhh!)

Mapema gazeti hili lilimtafuta Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi, kuzungumzia taarifa hizo bila mafanikio.

Zitto katika taarifa yake mbali na Wizara ya Nishati na Madini pia alimtaka Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma juu ya kiwango cha fedha ambacho Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme wa dharura kati ya Novemba 2011 na Oktoba 2012.

Alipotafutwa, Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kuzungumzia juu ya suala hilo, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alivyotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi pia hakujibu.

Juzi, Zitto alibainisha juu ya kuwapo kwa ripoti zinazoonyesha kuwa kuna kikundi ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia kwenye ununuzi wa mafuta mazito ya mitambo ya IPTL.

Alisema juhudi zilizofanywa na Kamati ya Bunge ya Hezabu za Mashirika ya Umma ambayo yeye ndiye Mwenyekiti wake, Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Nishati na Madini, January Makamba, za kutaka uchunguzi juu ya suala hilo ufanywe, hazikuzaa matunda.

Katika kutafuta kiini cha upotevu, kwa mara nyingine, wa mabilioni ya shilingi TANESCO, gazeti hili lilimtafuta Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jenerali mstaafu Robert Mboma, bila mafanikio.

Hata hivyo, alipopigiwa Makamu Mwenyekiti wake, Victor Mambalaswa, alisema yuko jimboni na kwamba taarifa hiyo ya CAG kuhusu upotevu wa mabilioni hayo haijafika TANESCO.

"Kama kuna mtu kaiona hiyo taarifa itakuwa serikalini lakini TANESCO bado haijafika," alisema Mwambalaswa.

Kwa upande wake Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, Mnyika, alisema anaungana na Zitto kuwataka viongozi hao wa serikali watoe kauli kwa umma akiwamo CAG na Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA).
Alisema iwapo kauli hazitatolewa kwa wakati atatoa nyaraka na majina ya wahusika.

Mnyika alisema alichoeleza CAG kwenye taarifa yake kama ilivyonukuliwa kwenye gazeti la The East African la Novemba 24-30 kuhusu dola milioni 54 (bil. 86) ni sehemu tu ya tuhuma za ufisadi zinazotokana na ukiukwaji wa sheria ikiwemo ya ununuzi katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme.

"Lakini ukweli kuwa tuhuma za ufisadi, Waziri Muhongo, Waziri Mgimwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Jenerali Mbona wanapaswa kutoa kauli kurejea taarifa ya Zitto ya jana na taarifa yangu ya Novemba 23 mwaka huu," alisema Mnyika.
 

iMind

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Messages
2,123
Points
2,000

iMind

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2011
2,123 2,000
Ni mjuavyo prof kama hizi taarifa ni za kweli basi lazima watu wang'oke. Hata hivyo Ikumbukwe kuwa hawa mawaziri wameingia hivi karibuni na hawawezi wakawa wamesoma kila report. Wapewe muda watatolea ufafanuzi.
 

Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
13,431
Points
2,000

Jay One

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
13,431 2,000
Ni mjuavyo prof kama hizi taarifa ni za kweli basi lazima watu wang'oke. Hata hivyo Ikumbukwe kuwa hawa mawaziri wameingia hivi karibuni na hawawezi wakawa wamesoma kila report. Wapewe muda watatolea ufafanuzi.

hey.... hey...!!

Before u discuss anything in any media KWANZA JUA SOURCE NI NANI..!!! INA INTEREST GANI NA NANI NA CHAMA KIPI etc....!!!

Hapa ni TANZANIA DAIMA.... cdm news paper...!!

Zitto a cdm mp....

Mbaya zaidi Zitto anawafanya Tanzanians wapuuzi wa first order as if hatufikiri hata kidogo kuhusu issue ya mafuta mazito ya IPTL...!!

Zitto ndie aliyekuwa anapewa RUSHWA YA MAFUTA YA IPTL ILI MCHEZO MCHAFU WA KUUZA MFUTA UENDELEE WAKATI MAJI YAPO WANAKATA UMEME MAKSUDI ILI KUSEMA MAJI NI MACHACHE SO WAWASHE IPTL POWERPLANTS ILI WAUZE MAFUTE WAKATI MAJI YAPO TELE....!!!

So Zitto anajua hata kabla huyu Waziri Muhongo hakumbua bungeni....!! Na bunge kuunda tume kuchunguza bahati mbaya ushahidi ulikosekana kwani ili tume ilipokea rushwa...!! Prof Mhungo alishatoa tuhuma za uwizi za fedha hizi kabla ya kuwa waziri 2011/2012.....

Mbaya zaidi Zitto alimtetea sana Mhando kabla ya kufukuzwa na Waziri meaning Zitto alikuwa anapata fedha zake kupitia Mhando thru dili la Mafuta hayo....

Baadae Mhando kakutwa na tshs 800million ktk account yake na imewekwa at once kupitia tanesco...!!

So Zitto ni NDUMILAKUWILI, mnafiki sana.... ana bifu na Prof. Muhongo.... of which akili ya Zitto is only 30% ya Prof. Muhongo....!!

Finally Zitto ataaibika ww subiri time soon is coming.... In short Zitto Mwizi...!!!
 

FJM

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
8,083
Points
1,225

FJM

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
8,083 1,225
Report ya CAG imetoka lini, na hizo hela zilipotea lini? Zitto anakumbukumba alikuwa anamtetea Muhando? Pengine Muhando atakuwa na majibu mazuri/ya kina kuhusu matumizi ya hizo hela kuliko Prof Muhongo.

Kadri siku zinavyoenda uwepo wa Prof Muhongo unatoa mwanga kuhusu characters za baadhi ya wabunge!
 

Adrian Stepp

Verified Member
Joined
Jul 1, 2011
Messages
2,452
Points
2,000

Adrian Stepp

Verified Member
Joined Jul 1, 2011
2,452 2,000
Niliongea na muhongo na alimpaka sana kwa kumuita kwamba ana madai ya zitto ana madai ya kipuuzi na hana facts na inaonekana zito anamkwepa muhongo ..sasa sijui nani wakuaminiwa!
 

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
9,743
Points
0

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
9,743 0
Ni mjuavyo prof kama hizi taarifa ni za kweli basi lazima watu wang'oke. Hata hivyo Ikumbukwe kuwa hawa mawaziri wameingia hivi karibuni na hawawezi wakawa wamesoma kila report. Wapewe muda watatolea ufafanuzi.
kung'oka peke yake kunatosha????aaaargh,
 

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
9,743
Points
0

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
9,743 0
Report ya CAG imetoka lini, na hizo hela zilipotea lini? Zitto anakumbukumba alikuwa anamtetea Muhando? Pengine Muhando atakuwa na majibu mazuri/ya kina kuhusu matumizi ya hizo hela kuliko Prof Muhongo.

Kadri siku zinavyoenda uwepo wa Prof Muhongo unatoa mwanga kuhusu characters za baadhi ya wabunge!
wanasiasa wanatupotezea sana MUDA WETU
 

cedrickngowi

Senior Member
Joined
Jun 9, 2012
Messages
148
Points
0

cedrickngowi

Senior Member
Joined Jun 9, 2012
148 0
Tusikwepe ukweli,haijalishi aliyesema ni nani au anatoka chama gani.This issue is of a National interest.Whats matter is the validity of the statement.Basically usitegemee habari kama hii itoke kwenye gazeti la uhuru,so Chadema are doing their work as opposition part.And has CAG become a CDM member too?Tafakari...............chukua hatua.....
 

nice 2

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Messages
747
Points
0

nice 2

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2011
747 0
Nyie watu mna matatizo sana, kitu akikisema Zitto tu mnaweweseka utafikiri nini, mnaacha kujadili mada na kuanza kumjadili yeye, mtakufa siku si zenu maana yeye anaendelea kufanya wajibu wake kwa taifa lake.
Mmeshikilia tu Zitto alikuwa anamtetea Mhando, Zitto alikuwa anamtetea Mhando, bila ya kujua Zitto alikuwa anataka taratibu tu zifuatwe. Na siku zote obsession ni mbaya, ushabiki ni mbaya, bila kuangalia maslahi ya taifa. Wakati wa bajeti ya wizara ya Nishati na Madini mmefanya upuuzi huu huu wa kushadadia na kumnyon'gonyeza Zitto kahongwa, Zitto kahongwa, matokeo yake ukweli umejulikana na bajeti ilishapita bila kujadili maswala muhimu kabisa kwa maendeleo ya nchi yetu zaidi ya kushabikia uzushi ule. Silly country with silly people.
Wewe unayejiita MR.PRESIDENT hapo juu unayedai Zitto alihongwa, nakuambia tena kwa herufi kubwa, humjui Zitto unayemuongelea, Zitto hana bei mbele ya nchi yake. Kama hutaki unaacha lakini habari ndio hiyo. Zitto huyu anayewindwa na maadui waliojaa nje na ndani ya chama chake, amini nakuambia, siku anapatikana na tuhuma za kuhongwa hata big G tu, mwisho wake kisiasa utakuwa umewadia.
Ngugu Zitto songa mbele, usichoke kulitumikia Taifa lako.
 
Last edited by a moderator:

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Messages
6,733
Points
2,000

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2011
6,733 2,000
Nakubaliana na mengi ambayo Mh. Zitto anayafanya lakini hili la kurumbana na Prof. Muhongo naanza kuingiwa na wasiwasi nalo.

Binadamu wote wana mapungufu. Mapungufu ya Mh. Zitto ni kutokubali kuonekana kama naye ni binadamu mwenye mapungufu na hili linapelekea kuonekana kama ni mbinafsi wa fikra.

Huyu waziri ameanza kazi wakati Zitto akiwa tayari mwenyekiti wa kamati. Mh. Zitto alitakiwa kuyajua haya madudu mapema kabla ya Prof. muhongo kuwa Waziri wa hiyo wizara. Kama hakuweza kufanya hivyo, morally anakuwa hatendi haki kwa Prof. muhongo pale anapoanza kumpa pressure kujua kama anafanya nini kuhusiana na hilo wakati yeye hata hakuwezi kufanya lolote wakati watanzania wanakatiwa umeme ili watu wachache wanufaike na uuzaji wa mafuta.

Mh. Zitto anakuwa kama ana bifu za kibinafsi na Prof. muhongo baada ya Prof. muhongo kuirushia madongo kamati yake.

Mh. Zitto anafanya hivi ili kuonyesha kama kamati yake iko makini katika utendaji wakati ukweli uko wazi.

Wamewaangusha wananchi kwa hili pamoja na kwamba wanataka waonekane kama serious committee
 

Manyi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Messages
3,254
Points
1,195

Manyi

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2011
3,254 1,195
Ki uhalisia, Waziri hawezi kutoa majibu ya haraka haraka, lakini ilitakiwa asiseme kwamba yeye si mtu wa kulumbana, alitakiwa aseme atalifanyia kazi, na kama ni ukweli basi ajue cha kufanya!
 

Wamunzengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Messages
810
Points
250

Wamunzengo

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2012
810 250
Ng'wamapalala Sioni tatizo la Zitto hapa, hata kama kamkomalia prof. Muongo, lakini si ni kweli hizo billions hazijatolewa ufafanuzi zipo wapi??? ccm wameshatufanya kitu mbaya kwa muda mrefu. hata hawa kina prof. Muongo hatutakiwi kuwapa nafasi. muda si mrefu na wao wataendeleza wizi uleule tuu kama watangulizi wao. Watanzania inatakiwa tuungane katika kuhoji pesa zetu na tusijali nani anahoji na nani anahojiwa. issue hapa ni pesa zimepotea na sio nani kaziulizia, Mbona watanzania tunachanganyana sisi kwa sisi???
 
Last edited by a moderator:

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Messages
6,733
Points
2,000

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2011
6,733 2,000
Sioni tatizo la Zitto hapa, hata kama kamkomalia prof. Muongo, lakini si ni kweli hizo billions hazijatolewa ufafanuzi zipo wapi??? ccm wameshatufanya kitu mbaya kwa muda mrefu. hata hawa kina prof. Muongo hatutakiwi kuwapa nafasi. muda si mrefu na wao wataendeleza wizi uleule tuu kama watangulizi wao. Watanzania inatakiwa tuungane katika kuhoji pesa zetu na tusijali nani anahoji na nani anahojiwa. issue hapa ni pesa zimepotea na sio nani kaziulizia, Mbona watanzania tunachanganyana sisi kwa sisi???
Mkuu,
Labda tukubali kutokubaliana lakini naona tatizo hapa ni pale Zitto anapohoji kwa misingi ya kisiasa na kibinafsi zaidi ambapo madhumuni yake ni kutaka kuionyesha jamii kama yeye na committee yake ni active tofauti na ilivyosemwa na Pro. muhongo.
Kuna taratibu zinatumika za kutaka kujua yale ambayo Mh. zitto anataka kujua ikichukuliwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa committee ndiyo maana Pro. muhongo amejibu kwa kusema yeye siyo bingwa wa malumbano.

Mh. Zitto anaweza kuwa na nia njema lakini mazingira yanatoa mwangwi wa uwalakini kwa kile kilichomo ndani ya hoja yake ukizingatia kuwa ni Pro. Muhongo aliyefurumusha haya madudu.
 

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,870
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,870 1,225
JUMATANO, NOVEMBA 28, 2012 05:00 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM


SERIKALI imesema inaandaa taarifa rasmi za kumjibu Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), kutokana na tuhuma nzito alizotoa za upotevu wa Sh bilioni 86. Juzi, Zitto alitoa taarifa kwa vyombo vya habari, akiituhumu Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwa zimefuja mamilioni ya fedha kwa ajili ya kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme ya Kampuni ya IPTL.

Habari za uhakika zilizopatikana jana kutoka ndani ya wizara hiyo, zinasema tangu juzi maofisa wa wizara hiyo, wamekuwa na vikao vya mara kwa mara ambavyo vinapitia kumbukumbu za manunuzi.

"Tangu juzi, baada ya Zitto kutoa tuhuma hizi, kumekuwa na vikao vizito hapa, moja ya jambo kubwa ni kujadili madai ya mbunge huyu, hapa ni kama Serikali inaweka mtego wa kumnasa Zitto.

"Baada ya kukamilika kwa vikao hivi, Wizara itatoa taarifa rasmi ya madai ya Zitto ambayo yanaonekana wazi ni kama anatafuta umaarufu wa kisiasa, tumesikitishwa mno kwa nini atumie kunukuu gazeti," kilihoji chanzo chetu.

"Nakwambia kaka tumeandaa majibu mazuri ambayo Watanzania watatuelewa juu ya madai ya Zitto, naomba muwe na subira ndugu zangu," kilisema chanzo chetu.

"Hatutaki kukurupuka kutoa majibu kabla ya kufanya utafiti wa jambo lenyewe, wizara imekaa na imeandaa ufafanuzi mzuri ambao utaelezwa muda wowote kwa Watanzania, kupitia vyombo vya habari, sasa subiri kuanzia kesho (leo) au kesho kutwa (kesho) ufafanuzi utatolewa.

"Wizara hii, haitaki kufanya kazi kwa siasa, tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa, hata kama kuna taarifa za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), zimebaini jambo lazima hatua zichukuliwe kwa kufuata taratibu," alisema.

Siku mbili zilizopita, Zitto alisema Sh bilioni 86 zimepotea ndani ya wizara ambazo ni za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu, Eliackim Maswi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Robert Mboma na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kutoa ufafanuzi kwa umma.

Mbali ya kuwabana, lakini hadi sasa viongozi hao wamekuwa kimya huku wakiwaeleza waandishi kwamba, hawataki malumbano kwa kuwa wao sio fani yao kama ilivyo kwa wengine.

Katika sakata hilo, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), aliungana na Zitto kudai ufafanuzi juu ya taarifa ya CAG na Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA).

Mnyika, alisema iwapo kauli hazitatolewa kwa wakati atatoa nyaraka na majina ya waliohusika na upotevu huo.
 

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Messages
3,926
Points
2,000

PhD

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2009
3,926 2,000
hey.... hey...!!

Before u discuss anything in any media KWANZA JUA SOURCE NI NANI..!!! INA INTEREST GANI NA NANI NA CHAMA KIPI etc....!!!

Hapa ni TANZANIA DAIMA.... cdm news paper...!!

Zitto a cdm mp....

Mbaya zaidi Zitto anawafanya Tanzanians wapuuzi wa first order as if hatufikiri hata kidogo kuhusu issue ya mafuta mazito ya IPTL...!!

Zitto ndie aliyekuwa anapewa RUSHWA YA MAFUTA YA IPTL ILI MCHEZO MCHAFU WA KUUZA MFUTA UENDELEE WAKATI MAJI YAPO WANAKATA UMEME MAKSUDI ILI KUSEMA MAJI NI MACHACHE SO WAWASHE IPTL POWERPLANTS ILI WAUZE MAFUTE WAKATI MAJI YAPO TELE....!!!

So Zitto anajua hata kabla huyu Waziri Muhongo hakumbua bungeni....!! Na bunge kuunda tume kuchunguza bahati mbaya ushahidi ulikosekana kwani ili tume ilipokea rushwa...!! Prof Mhungo alishatoa tuhuma za uwizi za fedha hizi kabla ya kuwa waziri 2011/2012.....

Mbaya zaidi Zitto alimtetea sana Mhando kabla ya kufukuzwa na Waziri meaning Zitto alikuwa anapata fedha zake kupitia Mhando thru dili la Mafuta hayo....

Baadae Mhando kakutwa na tshs 800million ktk account yake na imewekwa at once kupitia tanesco...!!

So Zitto ni NDUMILAKUWILI, mnafiki sana.... ana bifu na Prof. Muhongo.... of which akili ya Zitto is only 30% ya Prof. Muhongo....!!

Finally Zitto ataaibika ww subiri time soon is coming.... In short Zitto Mwizi...!!!
viingereza hivi vya kuunga lol
 

Raimundo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2009
Messages
13,507
Points
2,000

Raimundo

JF-Expert Member
Joined May 23, 2009
13,507 2,000
Huu ni upepo tu, utapita. JK kashakaa na mawaziri wapya kwenye semina elekezi? Maana naona wanafata nyendo zake za kupotezea kitu kipite.
 

Forum statistics

Threads 1,389,285
Members 527,879
Posts 34,022,131
Top