Zitto akataa posho ya mil. 238

Zitto akataa posho ya mil. 238

Naipendatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
5,091
Reaction score
8,243
By Zitto,

Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.

Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.

Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.

Source: His facebook page.

Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.

Ila zinga saidia kujenga ACT. Lakini ni sahihi kuwaachia wanyonge kama zitawafikia ( na huu ndio uzalendo wa kweli )
 
Huu ndio uzalendo

Aseme anazostahili kwa mujibu wa sheria ni ngapi? Mbona yeye analipwa wakati alifukuzwa kwenye chama chake na kuukosa Ubunge ? Mbona mpaka leo akina Danny Makanga na Erasto Tumbo , tangu walipofukuzwa UDP hawajawahi kulipwa mafao yao ? yeye analipwakwa utaratibu upi?
 
Nadhani ni zile alizotakiwa kulipwa katika utumishi wake bungeni kwa miaka yote 10 zile za nyongezo ni haramu!
 
Aseme anazostahili kwa mujibu wa sheria ni ngapi? Mbona yeye analipwa wakati alifukuzwa kwenye chama chake na kuukosa Ubunge ? Mbona mpaka leo akina Danny Makanga na Erasto Tumbo , tangu walipofukuzwa UDP hawajawahi kulipwa mafao yao ? yeye analipwakwa utaratibu upi?
Naona povu linakutoka ovyo.
 
jamani hamjamuekewa zzt,kasema fedha zoto za ziada.
sasa kwenye hiyo amount ya 238 atuambie za ziada ni ngapi?
Au hizo 238 zote ni za ziada ??
zitto you can fool some people some time but you can't fool all the all the times.
kawadanganye mwandiga na lwiche sio humu.
 
Aseme anazostahili kwa mujibu wa sheria ni ngapi? Mbona yeye analipwa wakati alifukuzwa kwenye chama chake na kuukosa Ubunge ? Mbona mpaka leo akina Danny Makanga na Erasto Tumbo , tangu walipofukuzwa UDP hawajawahi kulipwa mafao yao ? yeye analipwakwa utaratibu upi?
Mkuu mbona povu linakutoka hivyo?
 
Posho hizo ni kwa mujibu wa sheria so atapokea maana ni mafao kwa mujibu wa sheria ......awadanganye wajinga , zile za posho alisema hatapokea mara atapelekea kwenye NGO yake huko Kigoma , muulizeni ziko wapi ? NGO yake ilipokea ngapi? Mnafiki sana huyu ....
Kina Mbowe, Lema, Mnyika, kuchukuwa milioni 230 kila mmoja na kukaa kimya siyo wanafiki?
 
By Zitto,

Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.

Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.

Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.

Source: His facebook page.

Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.

Akiwa anatoa msaada atasema zimetoka wapi?Lazima atajibu kwenye mafao yangu au?Anatafuta sifa kwa fedha anazoziita haramu.

Wengine tumechoka kudanganywa.Alisema mwenyewe msituamini wanasiasa,ni kweli waongo kwa asilimia 100.
 
Kina Mbowe, Lema, Mnyika, kuchukuwa milioni 230 kila mmoja na kukaa kimya siyo wanafiki?
Zitto, anasema atachukua zile anazostahili kwa mujibu wa sheria , sasa yeye ambazo hastahili ni ngapi? Vipi kuhusu posho ya kukaa ambayoalisema aliacha kuchukua , mbona aliendelea kuchukua ?
 
Back
Top Bottom