Jamani mliowahi kuwapo pale Mbeya, enzi zile timu ya soka ya TAZARA ilipokuwa inavuma, naombeni mnifafanulie kama huyu jamaa ndiye yule mshambuliaji wa kati aliyekuwa anaitwa Dunia Nkwarulo, ambaye amecheza na akina Amri Said 'Stam'. Kuna kipindi pia aliichezea Ujenzi ya Rukwa, ila alikuwa anapaisha sana mipira juu ya lango kila mara hata kama goli liko wazi, hadi kocha akaamua aanze kumpanga wingi ya kulia ili hata kama atapaisha krosi, walau mpira utabaki uwanjani. Je, ndiye huyu Dunia wa CUF? Kama ndiye basi naombeni namba za pale Uhamiaji.