bigilankana
Senior Member
- Dec 15, 2009
- 144
- 4
Si vibaya kutoka professional nyingine na kuingia katika siasa kama unawito na unapenda siasa. Hi haina tofauti sana na mtu kuhama kazi toka kampuni moja kwenda nyingine. Lakini kitendo cha Zitto kusema siasa sio chaguo lake la kwaza si kauli nzuri kama kweli aliitamka. Kauli hii inaonyesha anaibeza kazi iliyompa umaarufu pengine kwasababu sasa inamshusha umarufu huo.Kutokana na mwandishi hapo juu, kama kweli Zitto anataka kuacha siasa wala asisite kujiuzuru, wapo watu wengi sana wanaotaka nafasi hiyo atakua ametoa nafasi mhimu kwa watanzania wengine kushirika katika siasa. Namshauri hiyo barua aliyoandika aiwakilishe mapema tu na hakuna atakae mlazimisha kugombea tena.
Zitto hatawapa mnachotaka.
Mkuu bigilankana nimesoma utetezi wako wote kwa Zitto - umejaribu sana na nakupa pongezi lakini sasa naona unaanza kuchoka. Kama umefikia kusema kuwa Zitto hatatupa tunachotaka, bila shaka sasa unakubaliana na sisi wengine kuwa kwa mwendo wake huo, hatufai. Naomba umpe ushauri mdogo tu - ukishachagua kuwa mwanasiasa yabidi utekeleze na miiko yake mojawapo ukiwa kuwapa wengi wanachotaka. Kwa kuwa hawezi kutupa tunachotaka, basi aachane na siasa na wengi tutaheshimu huo uamuzi wake. Kafulila, rafiki yake mkubwa Zitto, tayari huko NCCR alikohamia kunafuka moshi na hata miezi sita bado !
mnaotaka na kusukuma ahame chadema msahau hahami. keshasema mwenye nguvu katika chama huwa hahami. huko NCCR ni majungu tu ya Tanzania Daima. Habari yenyesoma ni fitna tupu. wamezoea vya kunyonga...... vya kuchinja hawaviwezi
Binafsi mimi sikufuatilia kipindi hiki, lakini kama anasema tena on public kwamba maamuzi ya vikao yalikuwa batili huyu kijana si makini, anahitaji kumaliza matatizo yake ndani ya vikao vyao. lakini kama karudia tena kauli zake amefanya makosa makubwa, watanzania walifanya makosa sana kumwamini huyu dogo kama mwanamapinduzi wa kweli - nafikiri hizi njaa bado ni tatizo kubwa hasa kwa wanasiasa vijana.
Hata kama umetofautiana na viongozi wako kwa namna yoyote ni mwiko kusema mambo ya siri ya chama nje, ni sawa na kusema siri na mkeo kikojizi mbele za kadamnasi inakuwa aibu ya nani? hii ni miiko ya kisiasa. kwa nini msimalize matatizo yenu humo ndani ya chama chenu? kutuambia sisi mambo yenu ndiyo tuone wewe unaonewa?
Fuaten nyayo za wanasiasa wavumilivu, uanasiasa si kuagiza kitimoto na bia baridi, kuna mifano bora mizuri ya kuiga kwa wakongwe walivyofanyiwa na chama chao
a) Mzee malechela asingekuwa mvumilivu asingekuwa hapo alipo, kwa kukatwa jina lake baada ya kazi ngumu kuzunguka nchi nzima mzee wa watu kutafuta wadhamini kungombea urais.
b) Mzee Salim asingekuwa mvumilivu asingekuwa hapo alipo baada ya kusemwa yeye ana damu ya uarabu......si mtanzania wakati kashika nyadhifa kubwa sana serikalini ya Umoja wa Nchi huru za kiafrika akitokea tanzania.
Wapo wengi tu, Zitto ndugu yangu mimi nilifikiri hutaongea tena on Public sasa umerudia kosa tena? sasa kutembea na barua mfukoni kuna maanisha nini? office za CHADEMA umezisahau zilipo kwa nini usiipeleke? au unangoja wakuite wakuulize tuhuma zako?. We unakijua CHADEMA vizuri hawatakuita ng'oo na hiyo barua itachakalia mfukoni kwako kama hutaki kuipeleka. wale jamaa wata kuignore utakuwa upoupo tu pale ofisini unazunguka.
Watu tayari washaanza kukuweka kundi moja na Mrema usipokuwa makini nduguyangu siasa ndiyo baba jeni bye bye.
Nijuavyo, muungwana ukitaka kuacha mke, unakamilisha taratibu zote kunakohusika na wanaohusika kisha unaangalia anga zingine kwa wakati wako. Sidhani kama ni sahihi kuutangazia umma ubovu wa huyo mke na kuzunguka na rasimu ya talaka ambayo unakusudia kumtwanga muda usiojulikana. Pengine ndio kama isemwavyo kwamba kwenye siasa kitu ustaarabu hakipo - ni mikakati tu!
Ugumu wa kuwasilisha hiyo barua ya kujiuzulu unatoka wapi kama kweli Mh. Zitto keshapoteza interest kwenye CHADEMA na siasa kwa ujumla? Au uongo? Ni kweli kuwa ni maisha yake (hayatuhusu) kama wasemavyo wengine, lakini ukishaingia katika public domain na kuwapa tumaini wengi kwa vipaji na ujasiri kama alivyoonyesha huyu dogo hapo nyuma, tutasema tu kuwa tumekuwa disappointed na hii anticlimax inayojitokeza sasa.
nianze kwa kukiri kuwa mimi siyo chadema ila ninaipenda sana chadema na nipo tayari kutoa support yeyote muhimu kwa chadema. Endapo nitaamua kujiunga na chama chama hicho kitakuwa ni chadema. Lakini nakiri kuwa Zitto hafai kuwa kiongozi wa chadema kwa sasa.
Kiongozi mzuri hawezi kupinga maamuzi ya vikao halali vya chama tena ktk vyombo vya habari, vinginevyo awe amejiuzuru kwa kutokukubaliana na maamuzi ya chama. Zitto anaendeleza ajenda yake ile ile kwamba yeye pekee ndiyo kiongozi anayefaa chadema. I'm sorry to say it.
Wakuu,
Haya yanatokea leo sio bahati mbaya ni mpango maalumu ilioaandaliwa tangu mwaka jana mwezi Desemba, na inasadikiwa unaratibiwa na Profesa mmoja wa chuo kikuu UDSM na mwingine mwenye shahada ya uzamivu toka hapo UDSM. Bahati mbaya au nzuri CHADEMA wamekuwa makini sana katika kushughulikia hii ishu ya Zitto, vinginevyo mambo makubwa yangekuwa yametokea kama Zitto mwenyewe alivyowahi kusema kuwa atafanya maamuzi magumu. Mpango huu unaratibiwa katika namna ambayo Zitto atapojitoa CHADEMA ionekane kuwa chama ndio kimemfanya ajitoe na sio yeye. Sasa CHADEMA hawajawa ''reactive enough'' vile mkakati ulivyotarajia, ndo maana kila siku linaibuka jambo jipya.
Tatizo jingine ndani ya CHADEMA kuna wanachama waandaamizi ambao hawakubaliani na mambo/uongozi wa makao makuu kimtaani nasema hawakubaliani na ''uchaga'' sasa hawa wamejipanga kumuunga mkono ZItto kwa gharama yoyote kisa tu anapambana na Mbowe, bila kujali kuwa athari za mpambano huo ni kubwa zaidi kwa Chama kuliko watu binafsi kama Mbowe, Slaa au Zitto mwenyewe.
Mimi najua mchezo unaondelea kwa vile nina rafiki yangu mmoja yupo karibu na jamaa wanaoratibu huo mpango, angalia posti zangu za nyuma kuhusu Zitto nilishaandika hapa siku nyingi sana kabla hata hajatangaza kugombea huo uenyeketi.
Nilishasema huko nyuma, kwa siasa za TZ huwezi kuwa mpinzani at the same time ukawa unaifurahisha serikali- haiwezekani kabisa. Kwa wale ambao mna mapenzi ya kweli na mageuzi TZ na mnapenda upinzani nawashauri ZITTO sio mtu wa kuwekeza imani na feelings zenu atawaumiza- subirini...............
Niliwahi kusema hivi mwaka jana na subirini mtaona mengine, maana jana nasikia vinara wake na wanaomuunga mkono hawajapendezwa na mahojiano yake na TBC wanadai ''kajianika'' sana
Nilishasema huko nyuma, kwa siasa za TZ huwezi kuwa mpinzani at the same time ukawa unaifurahisha serikali- haiwezekani kabisa. Kwa wale ambao mna mapenzi ya kweli na mageuzi TZ na mnapenda upinzani nawashauri ZITTO sio mtu wa kuwekeza imani na feelings zenu atawaumiza- subirini...............
Nadhani Zitto anatafuta sababu ya kutimuliwa CHADEMA ili aweze kurejesha nafasi yake kisiasa ambayo kwa kweli ameanza kuipoteza kutokana na kauli zake tata. Mwanzono nili-sympathise naye wakati wa Mchakato wa Uchaguzi wa CHADEMA na aftermath lakini sasa ukiongeza yalosemwa kwenye magazeti hasa Mwananchi naona kama anapoteza mwelekeo.
Kitu nachowapongeza CHADEMA ni kumwangalia tu na kusubiri atakachoamua yeye Zitto na ni vema watulie na wasikurupuka kumvua Uongozi au Uanachama kama walivyowafanyia Kafulila na Juju nadhani muda si mrefu tutamsahau kama tulivyowasahahu Wanasiasa wengine waliovuma kama vile Dk Lamwai na Dk Kaborou. Hata hivyo, nahisi Zitto anaweza kuwa Msaliti mkubwa sana wa Vyama vya Upinzani baada ya kuondoka CHADEMA na navishauri vyama vingne vya Upinzani kujihadhari na Zitto hasa hao NCCR ambao nadhani wana mpango wa kumsimaisha Kafulila ambaye anaungwa mkono na Zitto kule Kigoma.
umejiunga na haters. maneno yako yote hayana basis na yamejengwa na matofali ya CHUKI.
CHADEMA wanamwangalia tu? kuwafukuza watu wake na kusambaza majungu ni kukaa kimya? hujui usemalo. Zitto hatoki CHADEMA na hicho chama hakimfukuzi kwani hana kosa kwa mujibu wa katiba yao. labda wasikilize watu wenye chuki kama wewe na uliojiunga nao
- Nafikiri anapswa kujutia kuwa exposed, hivi watu wanawezaje kujua kuwa kwenye briefcase yako kuna barua ya kujiuzulu, si mpaka uwe umewaambia mwenyewe, sasa wewe kweli unaweza kuaminika na siri muhimu za chama? Licha ya za taifa as kiongozi?Re: Zitto ajutia kuingia kwenye siasa?
Nakubaliana na we FMES.- Nafikiri anapswa kujutia kuwa exposed, hivi watu wanawezaje kujua kuwa kwenye briefcase yako kuna barua ya kujiuzulu, si mpaka uwe umewaambia mwenyewe, sasa wewe kweli unaweza kuaminika na siri muhimu za chama? Licha ya za taifa as kiongozi?
- Sasa what this has to do na siasa mpaka kufikia hatua ya kuijutia? I mean somebody help me sioni the connection hapa! To me humo kwenye siasa Zitto amepanda exactly anachovuna, sasa anajutia what? siasa au matendo yasiyofanana na siasa?
- I mean I am lost!
Respect.
FMEs!
Zitto aibuka tena, amvaa Dk Slaa aapa kumsaidia KafulilaNAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ambaye ameibuka na kudai kuwa kamwe hata acha kumsaidia Kafulila katika mapambano yake ya kisiasa.
ASEMA SIASA SI CHAGUO LAKE
Salim Said na Fidelis Butahe
NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ameibuka tena na kutonesha majeraha ya mgogoro uliokuwapo ndani ya chama chake, akisema haridhiki na uamuzi wa chama hicho kuwaengua David Kafulila na Danda Juju.
Ingawa Kabwe hakutaja jina, kauli yake kupinga maamuzi ya kuwavua madaraka wanachama hao; imeonyesha kumzungumzia Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa kwa vile ndiye aliyesema Kafulila na Danda si kitu ndani ya chama hicho na kwamba, anaweza kuwashughulikia bila vikao vya chama.
"Mimi sipendi siasa za kinafiki, uamuzi wa kuwavua nyadhifa zao kina Kafulila haukuniridhisha kwa sababu haukuwa mzuri, ingawa ulipitishwa na mamlaka husika, katika vikao husika," alisema Kabwe katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1) jana asubuhi na kuongeza:
"Unajua unaweza ukawa na maamuzi yaliyofanywa katika vikao halali, lakini yasikuridhishe, pia unaweza ukawa na maamuzi katika vikao hivyo hivyo yakakuridhisha. Lakini mimi sikuridhishwa na mamuzi ya kina Kafulila kuvuliwa nyadhifa zao."
Mwanasiasa huyo kijana, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma, alisema siku zote haridhishwi na siasa za kinafiki, ndio maana siasa haikuwa chaguo lake tangu mwanzo.
"Chaguo langu la kwanza lilikuwa ni ualimu na nilifundisha sana mimi, lakini pia napenda sana kusoma, kuandika na kutafiti, hivyo Watanzania wajue hilo kwamba siasa sio chaguo langu," alisema Kabwe.
Katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa kuthibitisha kauli yake ya kutoshabikia siasa za kinafiki, Zitto alisema uamuzi wake wa kumsaidia Kafulila, umetokana na uwezo alionao kushika nafasi ya ubunge kupitia upinzani.
"Mimi naamini kuwa kujenga upinzani imara ndio tutaleta mageuzi ndani ya nchi, kwa hiyo nimeamua kumsaidia Kafulila kwa sababu ameingia upinzani, lakini, kama angeingia CCM nisingemsaidia," alisema Kabwe na kuongeza:
"Pia nilimwona ni kijana mwenye âcommitmentâ (mchapakazi). Mimi siamini kwamba Chadema pekee inaweza kuleta mabadiliko ndani ya nchi, bali kwa kujenga upinzani imara kuleta mabadiliko ni rahisi sana."
Zitto alikanusha madai kwamba, ndiye aliyemwingiza Chadema na kueleza kuwa alichofanya ni kumwandaa mwanasiasa huyo kijana kugombea ubunge jimbo la Kigoma Kusini.
"Namsaidia kwa sababu nilimwandaa kuwa mbunge, baada ya kumkuta makao makuu ya chama nikamchagua kuwa msaidizi wangu katika shughuli zangu za ubunge na hakuwa pekee alikuwa na wenzake, nikamuona anafaa kuwa mbunge," alisema Kabwe na kuongeza:
"Mimi nilipata safari ya kwenmda Ujerumani kusoma; kwa bahati mbaya huku nyuma akavuliwa nyadhifa zake ndani ya chama. Ingawa kuna watu wanasema alikuwa ameajiriwa; si kweli kwa sababu ndani ya Chadema hatuajiri."
Kabwe alifafanua kuwa aliamua kumsaidia Kafulila kwa sababu katika Jimbo la Kigoma Kusini ambalo kijana huyo anatarajia kugombea ubunge, kila mwaka wa uchaguzi kura zinagaiwa baina ya vyama vya CCM, NCCR na Chadema.
"Ninamsaidia Kafulila na nitaendelea kumsaidia kadri ya uwezo wangu, hilo naweka wazi kabisa," alisema Kabwe.
Kufuatia kauli na msimamo wake kuhusu maamuzi yaliyofanywa ndani ya Chadema, wadau mbalimbali wa masuala ya siasa walibahatika kutuma ujume wao wa maneno katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC1, walitafsiri kuwa mwanasiasa huyo huenda anataka kuhama chama au kuacha siasa.
Zaidi ya jumbe fupi 100 zilizomuhusu Kabwe, zilitumwa TBC1 ambapo zilisomwa moja kwa moja na mtangazaji wa kipindi hicho jana, Marine Hassan Marine.
Yussuf Msaliko wa Tabora alisema, inavyoonyesha asilimia 80, Kabwe anaelekea kuhama ndani ya Chadema au kuacha siasa.
Samuel Thomas kutoka Arusha, alimtaka Kabwe kutoacha siasa na kumtaka aangalie vizuri chama chake kwani kimejaa âumimiâ.
Mchangiaji mmoja kutoka Bukoba ambaye hakutaja jina lake, alimueleza Kabwe kuwa kuachana na siasa si mwisho wala njia ya kuepukana na maumivu ya serikali ya CCM.
Mchangiaji mwengine kutoka Tabata jijini Dar es Salaam alimueleza Kabwe kupitia ujumbe wake kuwa, âKwa vile umeonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya vikao vya chama chako, hapo hakuna ushirikiano na viongozi wenzako.â
Wachangiaji wengi walimuomba Kabwe kutoachana na siasa kwa sababu mchango katika sekta hiyo unahitajika ili kulipeleka mbele taifa changa la Tanzania, huku wengine wakimtaka aingie CCM.
Majina ya Kafulila na Zitto yalitawala vyombo vingi vya habari mwishoni mwa mwaka jana, baada ya Katibu Mkuu wa Chadema kuwavua nyadhifa zao Kafulila, aliyekuwa Ofisa Habari wa chama hicho na Danda Juju aliyekuwa Ofisa Mwandamizi wa Masuala ya Bunge.
Dk Slaa alinukuriwa akisema Kafulila na Juju ni sisimizi tu ndani ya Chadema. Aliwatimua kwa madai kuwa walikuwa wanavujisha taarifa za ndani ya chama kwa vyombo vya habari, jambo ambalo liliwafanya wanasiasa hao kuhamia NCCR-Mageuzi na kupata mapokezi makubwa na ya heshima. Zitto aliondoka juzi usiku kwenda masomoni Ujerumani na anatarajiwa kurejea mwisho wa mwezi huu kuendesha vikao vya Kamati ya Bunge anayoingoza.
Zitto kasema azma yake toka mwanzo ilikuwa ni kufundisha ..
ila anajisikia uchungu sana pale anapowafikilia walioingia kwenye siasa kupitia yeye
Bado sijaelewa hiyo kauli
Naona Waberoya na Bigilankala wamejitahidi sana kumtetea Zitto maana kila aliyetofautiana na misimamo ya Zitto wao wamekuwa wakipinga. Mimi nitawajibu kwa kifupi.
Kama Chadema wameshamuona Zitto hafai wasije wakalogwa kumfukuza wala kumshirikisha kwenye mambo nyeti ya chama waachane naye awepowepo tu kama mtu mzima atajistukia mwenyewe kuwa hatakiwi.
Waberoya anauliza hasara zitazotokea Zitto akiondoka Chadema, hasara gani mimi sioni hasara kwani Zitto amefikia umaarufu kumzidi Kabuoru, kabuoru alikuwa Kabuoru kule Kigoma hadi CCM wakamzushia si Mtanzania. Sasa huyu Zitto hata CCM wenyewe wameshadharau anajimaliza mwenyewe hawataki lawama ni kama kumpiga nyundo marehemu utanunua kesi bure kwanza ni kumpa umaarufu wa bure.
Mimi nafikiri hasara anayoisema waberoya ni kupoteza jimbo, kipi bora kupoteza jimbo au kuua chama. Kama wakimwacha aendelee kuropoka (ila wasimfukuze kuna mbinu nyingi tu za kumfanya asisikike) atakiangamiza chama kizima na kupoteza hata majimbo mengine.
Zitto ni mchanga sana kisiasa nadiriki kusema hajui siasa ni nini, mengi yamesemwa ila nitakupa mfano mmoja umelala wewe na mkeo majambazi yanaingia yanataka pesa mkeo anajiunga nayo kukushambulia sijui kesho yake mtaangalianaje na mkeo. Ni sawa na Zitto anavyotaka kuwasaidia NCCR kupitia kwa Kafulila na wewe unataka Chadema waendelee kumchekelea tu Zitto, sijui kama anajua anachotaka kukifanya kama anajua basi simuungwana (gentleman) wala si mwanasiasa ana malengo yake wala si ya kisiasa.
Waberoya unaweza kunipa sababu tatu tu unazoona kuwa Zitto ni mwanasiasa mahili au anafaa kuongoza chama cha siasa nafikiri sifa za kiongozi bora unazijua si bora kiongozi ukiacha tukio la kufukuzwa bungeni na Richmond/Dowans. Nasikia ana rekodi ya kufukuzwafukuzwa Chuo kikuu wakati akiwa Daruso ila sina data kwa hili.
Chadema waendelee na mipango yao kama kawaida Sangara mbee kwa mbele mchuzi mzito pilipili kwa mbaaaliiiiiii na kachumbari pembeni.