Elections 2010 Zitto ajeruhiwa na Polisi, apelekwa Hospitali

Muwe mnaandika na visa mambo ya kusema source ITV ....................BAHATI YAKO NINGEACHIA TUSI
 
Hivi sasa ITV imetoka kumhoji Zitto Kabwe live ambaye amewatuhumu polisi wa mkoa wa Kigoma kumtishia na bastola na bunduki wakitaka kumtoa roho yake kwa sababu ambazo hata yeye hazielewi............
 
Hivi sasa ITV imetoka kumhoji Zitto Kabwe live ambaye amewatuhumu polisi wa mkoa wa Kigoma kumtishia na bastola na bunduki wakitaka kumtoa roho yake kwa sababu ambazo hata yeye hazielewi............

Acha umbea, waache polisi wafanye kazi yao.
 
Hivi wewe unashikishwa ukuta au?usiwe unaandika mauharo yako hapa


Kigogo! msamehe bure hawa ni wale wasiojua wayatendayo wako wengi humu ndani ukiwafuatilizia unaweza kufa kwa kihoro dawa yao ni KUWAPUUZA TU!
Msimu wao humu ndani umeisha ndio wanafunga virago maana walikuja kwa ajiliya uchaguzi sasa wamesha chakachua wanaondoka mmoja baada ya mwingine
 
usiogope! nilikua naendelea ... ni kwamba alikua ameenda kuwatuliza wanachama wa chadema waliochachamaa baada ya matokeo ya ubunge yaliyotangazwa kwa ccm imeshinda jimbo la kigoma mjini . Baada ya wananchi kutulia polisi walivamia
jengo la chadema na kuanza kushambulia na mabomu . wakati wa tukio hilo Mh. zitto aliokolewa na mdogo wake ambae alimkinga na mabomu yaliyokua yakiingia madirishani ambapo yalimuumiza mdogo wake mkononi! Baada ya tukio hilo kwenye chumba alichojificha Mh. Zitto kulikutwa ganda la risasi ambayo inasemekana ilipigwa pamoja na mabom.
 
pole bandugu zitto........lkn kama kuna uwezekano mpeleke mahakamani huyo ofisa wa kops kwa assault
 
usiogope! nilikua naendelea ... ni kwamba alikua ameenda kuwatuliza wanachama wa chadema waliochachamaa baada ya matokeo ya ubunge yaliyotangazwa kwa ccm imeshinda jimbo la kigoma mjini . Baada ya wananchi kutulia polisi walivamia
jengo la chadema na kuanza kushambulia na mabomu
. wakati wa tukio hilo Mh. zitto aliokolewa na mdogo wake ambae alimkinga na mabomu yaliyokua yakiingia madirishani ambapo yalimuumiza mdogo wake mkononi! Baada ya tukio hilo kwenye chumba alichojificha Mh. Zitto kulikutwa ganda la risasi ambayo inasemekana ilipigwa pamoja na mabom.
Wakati Mhe Zitto anafanya jitihada za kuwatuliza wanachma wake polisi walikuwa wapi?? Baada ya wananchi (wanachama wa Chadema) kutulia polisi walifuata nini kwenye ofisi za Chadema?? Kurusha mabomu? Ndiyo, kurusha mabomu kwa kuwa ndicho walichokifanya. Haya basi, madhumuni halisi yalikuwa ni nini? Nani aliwatuma? Maswali haya machache yananifanya nizidi kujiuliza hii amani inayohubiriwa nchi inamhusu nani hasa?
 
Hivi wewe Kishongo unayo akili timamu kweli? yaani unaona ni sawa polisi kutaka kumuua mh. Zitto? Unatakiwa utoe ushirikiano katika kukemea hali kama hii maana ipo siku yatakupata wewe.

Pole sana Zitto. Nashauri uwashitaki hao polisi kama unao ushahidi
 
sasa kufa zitto ni tatizo ? ikiwa anahatarisha amani ya nchi atashughulikiwa bila ya kumuangalia usoni

na huyu dogo anapenda sifa
 
Waingereza wana neno zuri juu ya mtu kama wewe "sadist." yaani mtu anayefurahia shida na mateso ya wengine. Katubu ndugu yangu.

I am sincerely sorry. Nisameheni wote niliowaudhi.
Nimeshatubu pia kama nilivyoshauriwa na ndugu yangu Rugemeleza.
Samahani Mhe Zito. Pole Mhe, Mungu aendelee kukulinda.
It is a blunder on my side. Sitarudia tena.
Once again sorry to you all.
 
Rafiki yangu ngoja nikuambie kitu kimoja kuna wakati unakua unaona mtu anataka kukunyang'anya kitu ambacho unastahili kuwa nacho huwezi ukakaa kimya lazima ukifate na ukimiliki, sasa huyu bwana anakifata kitu ambacho wananchi wamempa let him grab what he is suppose to posses.
 
mbona kuna taarifa zinadai kuwa aliyeumia ni mdogo wake zito ambaye aliona polisi kamwelekezea risasi zito yeye akaruka kumnusuru ndg yake ikampata yeye begani kama kuna mwenye taarifa sahihi akatuondolea utata
 
Waheshimiwa Zitto anaendeleaje? Mwenye taarifa atujuze wasije mchakachua huko hospitali. Mungu akuponye mbunge wetu!
 
Back
Top Bottom