Kisutu: Mahakama imemkuta na kesi ya kujibu Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,103
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania imemkuta na kesi ya kujibu, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne, Februari 18, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani hiyo, Huruma Shaidi baada ya kupitia majumuisho ya pande zote mbili yaliyowasilishwa mahakamani wiki mbili zilizopita.

Katika kesi ya msingi, Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo akabiliwa na mashtaka matatu yote ya uchochezi, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28 mwaka 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Katika shtaka la kwanza, inadaiwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi alitoa maneno ya uchochezi.

Alitoa maneno ya uchochezi kuwa "watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi, wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya cha Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua."

Baada ya kukutwa na tuhuma za kujibu, Zitto ameieleza mahakama kwamba atakuwa na mashahidi kumi na atatoa ushahidi wake kwa kiapo.

Upande wa mashtaka tayari umetoa mashahidi 15 katika kesi hiyo.

Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 17, 18,19 na 20 mwaka 2020 ambapo mshtakiwa atanza kujitetea.

1582014034008.png



Rejea:
Zitto Kabwe afikishwa Mahakamani Kisutu, asomewa mashtaka matatu na kuachiwa kwa dhamana. Azungumzia Kongamano la Uchumi

 
Je Hakimu Shahidi yko huru? au anafanya kazi kwa remote ya akina Makonda?
Anawezaje kuwa huru ?, si yeye tu bali system nzima ya mahakama pamoja na Boss wao CJ wote wanongozwa na remote, hawana uwezo wa kutumia Utashi wao na Taaluma zao
 
Mbona tokea kipindi hicho, hatujaona huo uchochezi huku mtaani...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom