Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
WAKATI kasi ya 'tumbuaji' majipu inayofanywa na Rais John Magufuli, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameibuka na kusema bado Rais hajagusa kansa ya ufisadi na badala yake anachokifanya ni kupapasa tu.
Amesema pamoja na jitihada ambazo Rais ameanza kuchukua kuhusiana na suala hilo, lakini bado hajagusa maeneo nyeti ambayo yamekuwa kilio kikubwa cha Watanzania ikiwamo suala la Tegeta Escrow, ambalo mpaka sasa mtambo wa IPTL upo chini ya matapeli na kila mwezi serikali inalipa zaidi ya Sh. bilioni nane.
Ufisadi mwingine ambao alisema haujaguswa ni wa hati fungani wa dola za Marekani milioni sita, ambao watu waliohusika wakiwamo benki ya Standard ya Uingereza ambao walitoa rushwa hiyo na waliopokea rushwa maafisa wa Wizara ya Fedha bado hawajafikishwa mahakamani na badala yake waliofikishwa mahakamani ni madalali tu.
Zito alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati kifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho. Alisema suala la hati fungani serikali inalazimika kulipa riba, hivyo imeongeza deni la taifa Sh. trilioni 1.2 bila riba na kwamba hadi mwaka 2020 serikali itakuwa imelipa zaidi ya
Sh. trilioni 1.8 ambazo ni zaidi ya Sh. bilioni 600.
Alisema badala ya Rais Magufuli kushughulikia ufisadi huo ambao Watanzania wanaupigia kelele pamoja na kuweka mfumo madhubuti ambao utazuia rushwa, mpaka sasa hajafanya hivyo.
Kadhalika, Zitto alisema mpaka sasa Magufuli anafanya kazi kidikteta kwa kupoka madaraka ya watendaji wake wa chini na kwamba hadi sasa Baraza la Mawaziri lililopo ni kama hewa kwa kuwa mawaziri hawajapewa nyenzo za kazi isipokuwa Rais wao ndiyo anafanya kazi zote.
Source: Nipsahe