siasa za tanzania haziwezi kufanana na nchi za nje .....hatujafika huko jamani! waacheni kina zitto wajitangaze wanaenda kutibiwa kipele Marekani pia, uelewa wa wananchi unawaruhusu kufanya hivyo.
wabunge tanzania wana watoto out of wedlock ......hakuna tatizo ( ingekuwa ulaya, angepata tabu kuwa mbunge au kuendelea na ubunge wake ( kama amepata akiwa mbunge)
wabunge wengi sana wana nyumba ndogo.....................but wananchi hatujali.
wabunge wengi ni mafisadi even.....................na wananchi hawajali wanawachagua hao kwa hao
sioni sababu ya kupiga kelele hili, la mtu kutumia pesa zake kwenda hospitali ujerumani........hakutomnyima kura.
mkamaP...
Wanaacha zoo kutembelea sio zoo ya Tanzania ....bali mbuga za wanyama ambazo kwao hazipo. mheshimiwa zitto angesema anaenda kutibiwa ugonjwa mzito kwa tanzania tusingeshangaa lakini kutibiwa fatigue Ujerumani ndo kulikowacha watu mdomo wazi.
kuwa na nyumba ndogo ndo utaratibu wa kutafuta mke? .....utaratibu wa kuwa na mke unajuulikana na kuwa na nyumba ndogo kunajuulikana. isitoshe wabunge kuwa na watoto nje ya ndoa pia sheria na maadili ya tanzania yanaruhusu?
lets be realistic..................tanzania kwetu kuna big big line baina ya mambo tunayoyaita personal na siasa........hli la kwenda kutibiwa nje naona tumeliingiza kwenye personal kama mtu anavyotafuta mke wa pili kwa kupika na kupakua nyumba ndogo na kuzaa watoto huko huko
Lakini fatique tu ndo ukatibiwe Ujerumani!!...huh! Ubunge raha bana, acheni watu wausake kwa udi na uvumba!
Hivi hii mentality ya viongozi wa Tanzania kuwa wakiumwa kidogo tu wanaenda nje kutibiwa itaisha lini? Kwa nini asitibiwe kwenye ile zahanati yake kule Kigoma kaskazini.
Regards
Hivi ni wapi Zitto Kabwe amesema ama amenukuliwa akisema kuwa anakwenda Ujerumani kutibiwa?
Omarilyas