Kasheshe, tuna kitu kama miaka 13 imebaki tufikie 2025 (Vision 2025). Ili kufikia hiyo vision serikali ili-break down plans tukapata miaka mitano mitano na ndipo tukawa na kitu kinaitwa MKUKUTA. Sasa hivi tuko kwenye MKUKUTA 2. Wakati huo huo tunaambiwa kuna 2011-2015 development plan. (Personally sijaelewa kwa nini tuna mipango miwili yaani MKUKUTA na huu wa 2011-16). Lakini nimejaribu sana kupitia bajeti za wizara nyingi ni vigumu sana kujua kama we're on/off track kwa malengo ya Vision 2025. Na kama tuko off track, je, kwa muda huu uliobakia tunaweza
kurebisha mambo na kurudi kwenye mstari?
Kwa mfano, kama tulisema madini yachangie % ngapi kwenye GPD by 2025, sasa tumefikia wapi? Au tulitaka utalii au uvuvi, au kilimo kichangie kiasi gani by 2025 na sasa tuko on/off track? Kama tulisema tunataka tuwe na madaktari 5,000 sasa hivi tuna wangapi?
Sasa hivi serikali inakopa sana, kama sikosei govt ndio mkopaji mkubwa kwenye commercial banks zetu hapa nchini! Kukopa sio mbaya ila tatizo ni tunafanyia nini huo mkopo? Tunakopa kulipa mishahara ya watumishi na sio kugharamia miradi ya maendeleo. Huku ni sawa na mkulima kula mbegu! Deni la taifa tunaambiwa ni 22 trillion, wamefanyia nini hizi hela? Na nani atalipa? and how kama tunakopa kulipa mishahara?
Ndio maana unaona Mkullo alikabidhi bandari ya Mtwara baada ya kushindwa kulipa deni la ndege! Siku zote nimekuwa naamini matatizo mengi tuliyonayo yanasababishwa na bunge. Bunge limelea bajeti za kipuuzi, bajeti za mishahara na posho wa warsha.
Bunge linatakiwa lisome Vision 2025 na MKUKUTA na hii 2011-2016 na kuelewa kila neno, halafu kila wizara ilete mambo yanayoelewa, waeleze wamefanya nini inline na hizo plan na kama wamekwama kwa nini?