Zito umeonyesha ujasiri, lakini!

Barbaric

Member
Aug 14, 2011
34
9
Nadhani wengi tunajua alichokisema mh. z. kabwe jana bungeni alipokuwa anahitimisha hoja ya kamati ya mashirika ya umma. zito alisema anakusudia kukusanya sahihi za wabunge 70 ili aweza wasilisha hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.

Ameonyesha ujasiri na hisia kuwa anachukizwa na utendaji kazi wa m.k.p.p , ugumu ninaouona katika hili ni uwezekano wa kupata 51% ya wabunge, kwa sababu ccm imezaa watoto wengi ambao ni cuf.
Wadau nisaidieni kiutaalam zaid nyie mnalionaje hilo?
 
Chochote kinawezekana. Mambo ya sasa nchini si kama zamani...hata waliokosa masikio, macho, na milango mingine ya fahamu zama za nyuma sasa wameanza kurejewa na milango yao ya fahamu, na wapigakura wao nao wanawakodolea macho kwa kila jambo ili wawaadabishe wale wasiosikiliza wa kujali maslahi na kilio chao. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom