Zito Kabwe: Asilimia 20% ya Michango ya Pensions ya Waajira Ikatwe Kwa Ajili ya Bima ya Afya

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Zito Kabwe ameishauri Serikali ikate Asilimia 20% ya Michango ya Waajira/Watumishi wa Sekta binafsi na WA Umma ya Kila Mwezi inayopelekwa nssf na psssf Ili itumike kupata Bima ya Afya badala ya kukata Asilimia 3% kwenye Mishahara..

Aidha ameshauri Serikali ichangie Asilimia 30% ya watu wasiojiweza yaani kaya maskini Kwa Ajili ya Bima ya Afya Kwa wote.



My Take:
Naunga mkono wazo la Zito Kabwe kwamba kuliko kukata makato ya Asilimia 3% kwenye salary Kila Mwezi Bora Serikali ikate kwenye michango ya pension..

Zito Huwa anaitendea Haki taaluma yake ya Uchumi Kwa maslahi ya Tanzania na chama chake..

Kile chama kingine sijui Huwa Wana Msaada gani hapa Tanzania zaidi ya kulaumu,kulalamika,kuonesha shida za Watanzania Twitter nk ila hawajawahi kuja na roadmap Wala mapendekezo yeyeote ya utatuzi..

========

"Watu masikini wasio na uwezo kabisa na ambao sasa ni wafaidika wa TASAF serikali iwalipie TZS 30,000 kila mwezi katika mfuko wa hifadhi ya Jamii. 20% itapelekwa NHIF kama bima ya afya Kwa njia hii

⁃Kila Mtanzania atakuwa na bima ya afya ambayo sio ya matabaka. Hapatakuwa na vifurushi. Watu wote watapata bima ya afya yenye huduma za hali ya juu. ⁃Kila Mtanzania atakuwa na uhakika wa maisha ya uzeeni kwani atapata pensheni akifika umri wa utu uzima.

⁃Uwezo wa Nchi kuweka Akiba utaongezeka kwa 5% ya GDP kutoka 16% ya sasa mpaka 21% katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji na hivyo TAIFA kuwa na uwezo mkubwa wa Uwekezaji wa ndani.

⁃Serikali itakuwa inalazimika kutenga angalau 2.5% ya Pato la Taifa kila mwaka kugharamia afya kupitia mfumo huu endelevu"

"Watu wote walio sekta rasmi wanaochangia sasa NSSF na PSSF wawe wanachama wa NHIF moja kwa moja ambapo 20% ya michango yao kila mwezi iende NHIF kwa ajili ya bima ya afya.
 
Back
Top Bottom