Umetumia kiswahili kigumu
Tuanzie kwenye VAT kwa wale wafanyabiashara wenye turnover ya 100m kisheria lazima wawe registered na VAT.
Vat inavyofanya kazi.
Naenda kununua mzigo wa jumla kwa supplier kariakoo wa Tsh 10000 vat inclusive maana kuna 18% ambayao ni 1800 nimelipa kama vat.
Napeleka mzigo dukani kwangu kumbuka na mimi nipo registered na vat.
Huo mzigo nauza dukani kwangu sasa katika kuuza nikauza labda 17000 ambapo thamani ya vat kwa mzigo niliouza ni yani 18% ya 17000 ni 3060. Sasa zile return za hawa bwana wakubwa ya tra hesabu zao zinakua hivi.
Hizo vat hazikuhusu mfanyabiashara ni unawakusanyia tra kwa niaba kwa hivyo kinachotakiwa kupelekwa tra kama makusanyo ya VAT ni hivi 3060 - 1800 = 1260
Kwa hiyo sasa hiyo 1260 inatakiwa iende TRA
Na kama jibu litakuja hasi yani makusanyo yamekua madogo kuliko uliyolipia yani mfano wakati wa kununua 1800 tulitozwa kama vat wakati wa kuuza tukakusanya 1200 kama vat ukija kutoa 1200 - 1800 = - 600 hapa wanatakiwa wakulipe tra ila hawalipi wanachofanya utapunguziwa credit kwenye kodi unayotakiwa kulipa.
Hiyo nimetoa maelezo upate mwanga wa vat tuje sasa kwa wafanyabiashara wanaoagiza vitu nje.
Unapo fanya importation ya goods, au machinery au chochote kuna gharama mbalimbali utatozwa kulingana na aina ya bidhaa., kama alivyo ainisha bwana
Root hapo juu, kuna TBS, TMDA, na nyinginezo inategemea aina ya bidhaa uliyoleta inaangukia wapi ukija upande wa kodi kuna import duty, Vat, railway nn sijui, na processing fees nyinginezo.
Hapo tutaangalia vat tu unapolipia vat mzigo ukifika dukani kwako ukianza biashara mwisho wa siku utapeleka TRA tofauti ya VAT iliyopatikana kulipia wakati unaingiza mzigo na ile ya kuuza mzigo.
Sasa kama umenunua mzigo halafu huna vielelezo vya vat na ikiwa wewe hapo umesajiliwa kukusanya vat kitakachotokea ni hivi.
Utaingia gharama kulipia kitu ambacho hukustahili kulipa.
Vat haimuhusu mfanyabiashara yeye ni wakala tu wa kuikusanya, ila usipokua na vithibisho itakulazimu ulipie wewe mfanya biashara.
Wale wanaagiza kupitia mawakala. Wanaofanya clearance wanashindwa kupata hizo nyaraka zote kwasababu anaefanya ni agent, tena anafanya kwa mkupuo wa mizigo ya wateja wake mbalimbali, we unaishia kulipia gharama za usafiri mwisho wa siku mzigo ukifika dukani unajikuta unasita sita kutoa risiti maana vat italalia upande mmoja kwenye mauzo tu kwenye manunuzi huna, na kumbuka kinachopelekwa tra ni tofauti ya vat ya manunuzi na mauzo, sasa ya manunuzi huna utaishia kupeleka ya mauzo tu ambayo itakuumiza yani utalipa hata ambacho hujakusanya😂😂😂😂
Sio mtaalam sana, hayo ninmachache ninayoelewa, kama kuna makosa kwenye maelezo yangu natumai wenye uelewa zaidi watarekebisha.