Zipi faida za kusafirisha Full Container au Loose cargo from China?

kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,800
2,000
Nimekuja tena kwenu wana jamvi naomba msaada wa kujua zipi ni faida za kusafirisha mzigo kama full container au Loose cargo kutoka China au Nchi za Wenzetu.

Moja kuhusu gharama za usafirishaji. Pili kuhusu mambo ya bandarini mzigo ukifika.

Nakukaribisha kwa mjadala.

CC Top leader

1622100681921.png
 
kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,800
2,000
Tumia wasafrishaji wa Tz , we kazi yako ni kuchukua mzigo godown , Ila ukijifanya kuagiza na kutrasnsport mwenyewe , TRA , bandarini , mamlaka husika lazima wakufurahishe ....
Asante
 
Top leader

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
202
500
Inategemea mzigo wako uko kiasi gani but hakikisha unafit kwa container yaanj zile ya 20'ft ua 40'ft

Charger ni zile zile tu kutokana na meli husika ukisafirisha loose kuna njia mbili haswa carrier wanaweza kukusaidia moja ya njia usafirishe kwa kupima cbm ulipie hii kwa harka ila naona ni costfully sana kama mizigo yako ni mingi na inakaribia kufit container at least ya 20ft

Nyinge hao ocean consolidator(carrier)wana tender nyingi kwa watu tofauti labda wate wanaleta mizigo Tanzania wakafanya consolidation ya mizingo yaani nyie shipper watatu mnataka kuleta mizigo Tanzania anakandamiza mizigo yenu kwa pamoja ili ifit kwa container moja then asafirishe hii njia inapendelewa sana mno naona ni cheap sana ila ubaya wake inachukua mda kusafirsha ikatokea ukakosa watu mkajiunga kutumia container moja kusafirshia ila hao carrier ni wajanja ukichonga nae fresh wapo kibao mfano hao silent ocean,sijui kilimanjaro nn wote wnaofisi bongo na china.
 
kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,800
2,000
Inategemea mzigo wako uko kiasi gani but hakikisha unafit kwa container yaanj zile ya 20'ft ua 40'ft

cean consolidator(carrier)wana tender nyingi kwa watu tofauti labda wate wanaleta mizigo Tanzania wakafanya
Asante sana kiongozi ninataka kuagiza vitu sasa saplaya kaniambia kontena la ft20 vinaingia vyote sasa nilitaka kujua ABC namna ya chargers za kulisafirisha
 
Top leader

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
202
500
Asante sana kiongozi ninataka kuagiza vitu sasa saplaya kaniambia kontena la ft20 vinaingia vyote sasa nilitaka kujua ABC namna ya chargers za kulisafirisha
Chukua tu container nzima usiwaze cost na biashara hope upatiga faida na krudisha pesa yako
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,349
2,000
Inategemea mzigo wako uko kiasi gani but hakikisha unafit kwa container yaanj zile ya 20'ft ua 40'ft

Charger ni zile zile tu kutokana na meli husika ukisafirisha loose kuna njia mbili haswa carrier wanaweza
Nje ya mada
Kontena linakuaa mali ya nani baada ya mzigo kushuka?
 
Top leader

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
202
500
Nje ya mada
Kontena linakuaa mali ya nani baada ya mzigo kushuka?
Containers zile empty unafanya booking kwa shipping line wale kama maersk,cosco, messina,evergreen ila hapa unaweza kusaidia hata na carrier au clearing and forwarding agent wako maana sasa kule china wewe utakuwa unaexport na huku bongo unaimport so baadhi ya carrier kila kitu katila izo unawaeleza tu maana kufanya bookinh ni online.

Kama mgen tafuta agent mzuri atakusaidia kila kitu japo ni process tena kutoa kweny forodha unahitaji clearing agent tena.
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
40,095
2,000
Mtoa mada kama una mzigo unaotosha 20ft basi pakia mzigo wote, tafuta agent mzuri atakutolea bandarini.... Ila lazima utapigwa tu, watakuambia TBS wanataka hili na lile afu hizo hela hazina risiti.
Watakuambia kuwa inatakiwa 1mil ya longroom hiyo hainaga risiti.

Bora ulete peke yako kuliko kumlipa agent hela ya cbm.

Pia ukleta mwenyewe ni rahisi kwenye kuandika return maana tin yako inakuwa imetumika kuingiza mzigo
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,349
2,000
Container hurudishwa depot baada ya mzigo kupakuliwa
Hapa ndo nilikuwa haswa nataka kujua , asante.

Kwa maana hiyo ili iwe rahisi ni vyema mzigo ukapakuliwa hapa hapa dar kuliko kupeleka kontena mkoani, maana itabidi lirudishwe depot kwa gharama tena
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
40,095
2,000
Hapa ndo nilikuwa haswa nataka kujua , asante
Kwa maana hiyo ili iwe rahisi ni vyema mzigo ukapakuliwa hapa hapa dar kuliko kupeleka kontena mkoani, maana itabidi lirudishwe depot kwa gharama tena
Gharama ni zile zile maana ukikodi fuso bado utalipa zakutosha tu
 
Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
1,215
2,000
Mtoa mada kama una mzigo unaotosha 20ft basi pakia mzigo wote, tafuta agent mzuri atakutolea bandarini.... Ila lazima utapigwa tu, watakuambia TBS wanataka hili na lile afu hizo hela hazina risiti.
Watakuambia kuwa inatakiwa 1mil ya longroom hiyo hainaga risiti.

Bora ulete peke yako kuliko kumlipa agent hela ya cbm.

Pia ukleta mwenyewe ni rahisi kwenye kuandika return maana tin yako inakuwa imetumika kuingiza mzigo
Hapa kwenye kuletewa mzigo na agent ndio kunawafanya wafanyabiashara kuzichukia EFD mashine kwa wale vat qualifiers😂😂

Unanunua mzigo unaletewa paaap, unalipia usafiri fresh mali inaingia store.

Biashara inaanza paap lazima utoe risiti ya mashine, risiti inasoma 18%, una claim vipi😂
 
kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,800
2,000
Hapa kwenye kuletewa mzigo na agent ndio kunawafanya wafanyabiashara kuzichukia EFD mashine kwa wale vat qualifiers😂😂

Unanunua mzigo unaletewa paaap, unalipia usafiri fresh mali inaingia store.

Biashara inaanza paap lazima utoe risiti ya mashine, risiti inasoma 18%, una claim vipi😂
Umetumia kiswahili kigumu
 
Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
1,215
2,000
Umetumia kiswahili kigumu
Tuanzie kwenye VAT kwa wale wafanyabiashara wenye turnover ya 100m kisheria lazima wawe registered na VAT.

Vat inavyofanya kazi.
Naenda kununua mzigo wa jumla kwa supplier kariakoo wa Tsh 10000 vat inclusive maana kuna 18% ambayao ni 1800 nimelipa kama vat.

Napeleka mzigo dukani kwangu kumbuka na mimi nipo registered na vat.
Huo mzigo nauza dukani kwangu sasa katika kuuza nikauza labda 17000 ambapo thamani ya vat kwa mzigo niliouza ni yani 18% ya 17000 ni 3060. Sasa zile return za hawa bwana wakubwa ya tra hesabu zao zinakua hivi.

Hizo vat hazikuhusu mfanyabiashara ni unawakusanyia tra kwa niaba kwa hivyo kinachotakiwa kupelekwa tra kama makusanyo ya VAT ni hivi 3060 - 1800 = 1260

Kwa hiyo sasa hiyo 1260 inatakiwa iende TRA
Na kama jibu litakuja hasi yani makusanyo yamekua madogo kuliko uliyolipia yani mfano wakati wa kununua 1800 tulitozwa kama vat wakati wa kuuza tukakusanya 1200 kama vat ukija kutoa 1200 - 1800 = - 600 hapa wanatakiwa wakulipe tra ila hawalipi wanachofanya utapunguziwa credit kwenye kodi unayotakiwa kulipa.

Hiyo nimetoa maelezo upate mwanga wa vat tuje sasa kwa wafanyabiashara wanaoagiza vitu nje.

Unapo fanya importation ya goods, au machinery au chochote kuna gharama mbalimbali utatozwa kulingana na aina ya bidhaa., kama alivyo ainisha bwana Root hapo juu, kuna TBS, TMDA, na nyinginezo inategemea aina ya bidhaa uliyoleta inaangukia wapi ukija upande wa kodi kuna import duty, Vat, railway nn sijui, na processing fees nyinginezo.

Hapo tutaangalia vat tu unapolipia vat mzigo ukifika dukani kwako ukianza biashara mwisho wa siku utapeleka TRA tofauti ya VAT iliyopatikana kulipia wakati unaingiza mzigo na ile ya kuuza mzigo.

Sasa kama umenunua mzigo halafu huna vielelezo vya vat na ikiwa wewe hapo umesajiliwa kukusanya vat kitakachotokea ni hivi.

Utaingia gharama kulipia kitu ambacho hukustahili kulipa.

Vat haimuhusu mfanyabiashara yeye ni wakala tu wa kuikusanya, ila usipokua na vithibisho itakulazimu ulipie wewe mfanya biashara.

Wale wanaagiza kupitia mawakala. Wanaofanya clearance wanashindwa kupata hizo nyaraka zote kwasababu anaefanya ni agent, tena anafanya kwa mkupuo wa mizigo ya wateja wake mbalimbali, we unaishia kulipia gharama za usafiri mwisho wa siku mzigo ukifika dukani unajikuta unasita sita kutoa risiti maana vat italalia upande mmoja kwenye mauzo tu kwenye manunuzi huna, na kumbuka kinachopelekwa tra ni tofauti ya vat ya manunuzi na mauzo, sasa ya manunuzi huna utaishia kupeleka ya mauzo tu ambayo itakuumiza yani utalipa hata ambacho hujakusanya😂😂😂😂

Sio mtaalam sana, hayo ninmachache ninayoelewa, kama kuna makosa kwenye maelezo yangu natumai wenye uelewa zaidi watarekebisha.
 
Guangzhou Youngson ltd

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
413
500
Unatakiwa kujua mzigo wako una CBM ngapi na uzito kiasi gani (wengi husahau kuhusu uzito)au kama unaweza kujaa 20ft a 40ft container.Kma unatosha then bora upakie full container na siyo loose cargo.

Faida mojawapo za full container
1.mzigo wote huwa ni wako .Kama utapakilia kiwandani hutakuwa na hofu ya kupoteza baadhi ya vitu kwani mzigo utapakiliwa kiwandani na utashushwa warehouse yako.

2.Gharama za full container kusafirisha + kutoa bongo gharama huwa chini kuliko ukipakia mzigo uleule kama loose cargo.

3.uharaka.full container utapakia tu mzigo wako unapokuwa tayari.Ila kama ni loose cargo ni lazima agent anayesafirisha mizigo awe na mizigo ya kutosha full container ndio na wako autume.

Faida za loose cargo
1.Kama hutaki kusumbuka basi hii option ni nzuri maana mzigo wako ukisha pelekwa kwa shipping agent we ni utasubiri ukufika ukachukue warehouse kwao;.wao watakuwa washamalizana na TRA na kila kitu

2.Kama mzigo wak haujai container
3.Kma mzigo wako ni compressed belo za nguo,betri za pikipiki (huwezi pakia full,ita over weight).Hii kutokana na experince.
kila la heri
 
malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
1,172
2,000
Tuanzie kwenye VAT kwa wale wafanyabiashara wenye turnover ya 100m kisheria lazima wawe registered na VAT.

Vat inavyofanya kazi.
Naenda kununua mzigo wa jumla kwa supplier kariakoo wa Tsh 10000 vat inclusive maana kuna 18% ambayao ni 1800 nimelipa kama vat.

Napeleka mzigo dukani kwangu kumbuka na mimi nipo registered na vat.
Huo mz
Umeeleza sahihi kabisa nando iko hivohivo mzee ukiwa kwenye vat usifanye mchezo kwenye manunuzi hakikisha manunuzi yako Yana vat ili uweze kui claim vat ktk return zako zakila mwezi
 
prince mrisho com

JF-Expert Member
May 2, 2015
2,830
2,000
Containers zile empty unafanya booking kwa shipping line wale kama maersk,cosco, messina,evergreen ila hapa unaweza kusaidia hata na carrier au clearing and forwarding agent wako maana sasa kule china wewe utakuwa unaexport na huku bongo unaimport so baadhi ya carrier kila kitu katila izo unawaeleza tu maana kufanya bookinh ni online.

Kama mgen tafuta agent mzuri atakusaidia kila kitu japo ni process tena kutoa kweny forodha unahitaji clearing agent tena.
wewe hukumjibu badala yake umetoa maelekezo, ila wa chini kamjibu shortly
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom