Hii ndiyo mbinu wanayotumia wakinga kuchana msamba badala ya kupiga hatua, umoja ndio siri, ni mbinu rahisi mno

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Ni jamii ambayo ilikuwa haijulikani lakini hivi karibuni kutoitambua ni sawa na kusema hakuna kitu kwenye chumba mlichomo na tembo, hata kwa wanaofunga mizigo yao soko kubwa kuliko yote nchini pale kariakoo ni mashuhuda, hawa watu ni kama wameimeza kariakoo, kuimeza kariakoo ni sawa na kuwa mfanyabiashara mkuu wa bidhaa zinazouzwa madukani nchi nzima.

Sio mbinu ya wakinga, wao walichofanya ni kuiga tu, mbinu hii hutumika sanasana na wasomali hasa nchini kenya.

Mbinu ni nyepesi mno na ninahofia endapo kabila kubwa likiiga basi litakuwa mbali sana kimafanikio, mbali sanaaaa!!

Kinachofanyika ni swala la kuwa na umoja unaowaunganisha wakinga waliofanikiwa Dar kuinua wenzao wenye biashara ndogo mikoani waende kufanya biashara kubwa dar.

Kunakuwa na umoja kwa mfano wanakuwa wakinga 500, kinachofanyika ni kwamba kila mwezi kila mtu awe mfanyabashara au kaajiriwa inabidi atoe elf 50, laki, laki 2, n.k kutokana na status yake, hata ukitoa M ni wewe tu.

Hapo kila mwezi huwa inapatikana takribani milioni 50

sasa kitachofanyika hapo, wanamchagua mkinga ambae ana fanya vizuri kwenye biashara yake ndogo huko mikoani walikojazana kama Mbeya, Songwe, Iringa, n.k..wanamchangia mtaji ahamie Dar, ile biashara ndogo huwa tayari wana watu wanaosaidiana ndio ambao wataendeleza yeye akienda kariakoo.


wale waliomchangia tayari huwa wana frem zao kibao pale kariakoo, watampa frem mwanachama mpya na kumshughulikia mambo ya vibali..

Mwanachama mpya ataamua afanye biashara ipi, akishaamua ataletewa mzigo na wakinga wenzake ambao wamejazana kama utitiri kwenye jiji la Guangzhou huko nchini China, hili jiji lina viwanda vya kutengeneza bidhaa, machimbo ya kununua bidhaa, bandari ya kusafirishia, n.k. wakinga ni wamejazana sana huko (kwa waliofika ni mashuhuda), hao ndio huwa wanasaidia kutafuta na kusafirisha bidhaa kwa wenzao, wana kampuni yao kubwa tu ya kusafirisha mizigo inaitwa mapembelo cargo, hilo neno mapembelo ni salamu ya kikinga, ukisalimiwa mapembelo unajibu vavene 😂


Mzigo ukifika bandarini tayari wama connections za kuutoa chap chap unaingia fasta dukani, huko dukani silaha yao kuu ni kuuza kwa bei ndogo kuliko wengine, kufanya hivyo inabidi wauze kwa faida ndogo, kitu ambacho kinauzwa kwa faida ya elf 30 wao wapo radhi wauze kwa faida ya elf 5, hii ndio tabia iliyowafanya hata wachaga na wapemba wanaouza bidhaa zilezile kama wanazouza wakinga wapakimbie hapo kariakoo.

Sasa ukijumlisha kuuza kwa faida ndogo, kulipa marejesho, kuwa wanachama wapya wanaotakiwa kuchangia mchango wa kuinuana, n.k hapa inabidi wajibane haswaa kwenye matumizi, hapa ndio utakuta ni kawaida yao kubeba chakula walichipikia nyumbani kwenye mahotpot.

Zamani wakinga waliokuwa wanaletwa kariakoo walikuwa wamekulia kijijini kwa muda mrefu sana na umri umenda kidogo ni ngumu kibadilika, ilikuwa ni kawaida sana kukuta mkinga kashazoea kuvaa ndala zake na koti lake, yani kama yupo kijijini na ndio kashazoea, kwa siku hizi zama zimebadilika, hata ukienda kariakoo utawakuta vijana watanashati tu ambao wanaendana na mda.

Kuhusu uchawi kiukweli hili jambo nimelisikia mda mrefu ila nakwambia biashara ni kuwa na bidhaa au huduma sahihi, jua soko linataka nini lete kile soko linataka, ukiuza kwa bei rafiki watu tutakutafuta tu popote

sasa sipati picha kabila kama wasukuma, wachaga, wanyakyusa, wahaya, hawa wenye idadi ya watu milioni 2 na zaidi, kabila moja wapo wajikusanye wawe na umoja wa watu hata elf 10 tu wawe wanachangiana hata elf 50 kila mwezi,

watu elf 10 x shilingi 50,000 = milioni 500 pesa taslimu

ni kiasi kikubwa sana hicho kinaweza kisiishie kuinuana kwa mitaji bali hata kielimu na kuendeleza makwao.

Tatizo kuu wengi hawataki waendelee ili wao wawe juu kuliko wenzao, hiki ndicho kinawapa raha.
 
Suala ka kuinuana nakuunga mkono! Mahali ninapo ishi kuna mkinga kawaajiri wenzake kwenye duka lake na huwa wanafanya kazi kwa si chini miaka mitano, baada ya hapo anawapa mtaji lets say kama ni 20M au 10M then anamsaidia kuanzisha biashara! Note: Ule mtaji unakuwa ni sehemu ya mshahara wake kwa mwezi huwa anawalipa kidogo then kidogo anawahifadhia kisha anawaongezea hela kidogo nao wanaanzisha biashara zao
 
Nidhamu na mtu kupata kile anachostahili bila 'ujambazi wa kalamu'

Amaa kweli haki huinua taifa

Na mdau Mzee Wa Kale Kabisa ameonesha pia factor nyingine kubwa mno. Kuaminiana wao kwa wao. TRUST ni muhimu mno. Kukiwa na trust kunakuwa na umoja.

Hii trust yao imejengwa tokea ngazi ya familia. Mtoto na mama nyumbani wanatambua wazi kuwa baba anashirikiana nao kila kitu starehe na huzuni. Wakiona wamekula mihogo basi na baba yao kala mihogo pia[hotpot].
 
Palipo wawili namimi nitakuja kuwa wa tatu, ila palipo watatu kuendelea hapashindikani kitu maana wanakuwa miungu.
 
Suala ka kuinuana nakuunga mkono! Mahali ninapo ishi kuna mkinga kawaajiri wenzake kwenye duka lake na huwa wanafanya kazi kwa si chini miaka mitano, baada ya hapo anawapa mtaji lets say kama ni 20M au 10M then anamsaidia kuanzisha biashara! Note: Ule mtaji unakuwa ni sehemu ya mshahara wake kwa mwezi huwa anawalipa kidogo then kidogo anawahifadhia kisha anawaongezea hela kidogo nao wanaanzisha biashara zao
Nidhamu ya pesa ni muhimu Sana kwenye kutafuta
 
Umoja ni nguvu utengeno ni udhaifu hakika wameonyesha mfano mkubwa kuwa kila kitu kinawezekauna kanapo nia na umoja ni wa kupigiwa mfano
 
Pamoja na mali zote hizo, napendekeza wayaishi maisha, Yaani utamkuta mkinga ana mali lakini maisha anayoishi hayafananii kabisa. mpaka unashangaa.
 
20230612_120344.jpg
 
Pamoja na mali zote hizo, napendekeza wayaishi maisha, Yaani utamkuta mkinga ana mali lakini maisha anayoishi hayafananii kabisa. mpaka unashangaa.
Wakinga mbona sasa wamebadilika sana wapo kisasa zaidi sio ndio hao wakina vunja bei
 
Back
Top Bottom