zipe maneno picha hizi

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
8E9U0051.jpg

wakakuleta muswaada wa sheria ya uchaguzi, mzee mwenzagu hukuusoma sawasaswa ukasaini namna hii,
8E9U0063.jpg

Wacha tuwachemshe bungeni waziri wako na mwanansheria mkuu hehehehehehehe jamani sina mbavu

picha hisani ya michuziblogspot
 
Hiyo ya kwanza, Kikwete alimwambia Slaa bado tunakuomba ujiunge na CCM utatupa changamoto sana ndani ya chama chetu na kuleta mabadiliko makubwa. Slaa anamjibu ndani ya CCM kuna matatizo makubwa sana sidhani kama nitafanikiwa kama ambavyo nikiwa CHADEMA.
 
Hapa namjuwa Jakaya tu,huyu mwengine sijui nani?.Hii chupa sina uhakika ni ya nini lakini imefanana na ya mvinyo.Mtumiaji wa hicho kinywaji inaonekana ni huyu jamaa mwengine, kwani glasi na vikombe viko kwake.Kikwete inaonekana hana kiu ya hicho kinywaji ndio maana ameamua asome gazeti lake.
 
Ile ya 2: Jakaya: "Mh. Slaa, kumbe kulikuwa na nyongeza alaa, ilikuwaje?"
Slaa: "Ndiyo, mheshimiwa Rais, tuliliona hilo!" Wanacheka.
 
Tuache utani, Jakaya is very receptive kwa watu, hata wapinzani. Unaona uso uliojaa utu licha ya kwamba yuko na mpinzani wake kisiasa. Huoni uso wa hasira au majivuno au dharau. Amejaa urafiki zaidi, na anaonesha ushirikiano. Nadhani kwa kiongozi ni kitu kizuri. Tz ni nchi nzuri sana. Siku viongozi wetu watakapoamua kuwa serious zaidi kidogo naamini tutapaa kimaendeleo kwa supersonic speed ya blackjack fighter bomber.
 
Hapa namjuwa Jakaya tu,huyu mwengine sijui nani?.Hii chupa sina uhakika ni ya nini lakini imefanana na ya mvinyo.Mtumiaji wa hicho kinywaji inaonekana ni huyu jamaa mwengine, kwani glasi na vikombe viko kwake.Kikwete inaonekana hana kiu ya hicho kinywaji ndio maana ameamua asome gazeti lake.

Mwingine ni Mbunge wa karatu Dr wilbroad Slaa
 
Tuache utani, Jakaya is very receptive kwa watu, hata wapinzani. Unaona uso uliojaa utu licha ya kwamba yuko na mpinzani wake kisiasa. Huoni uso wa hasira au majivuno au dharau. Amejaa urafiki zaidi, na anaonesha ushirikiano. Nadhani kwa kiongozi ni kitu kizuri. Tz ni nchi nzuri sana. Siku viongozi wetu watakapoamua kuwa serious zaidi kidogo naamini tutapaa kimaendeleo kwa supersonic speed ya blackjack fighter bomber.

Babuyao, Mpinzani ni mtu tu wa kawaida tu kama wewe ulivyo, the only difference between mtu na mpinzani, is that you differ on the approach on how to tackle the common problems that you face. Wapinzani hawanuki, wana akili kama binadamu mwingine yoyote na wengine wana akili zaidi ya waliopo madarakani, hivyo si ajabu kwa Mheshimiwa Rais kuwa na Slaa namna hiyo.

Hakuna cha ajabu hata kidogo.
 
Hiyo ya kwanza, Kikwete alimwambia Slaa bado tunakuomba ujiunge na CCM utatupa changamoto sana ndani ya chama chetu na kuleta mabadiliko makubwa. Slaa anamjibu ndani ya CCM kuna matatizo makubwa sana sidhani kama nitafanikiwa kama ambavyo nikiwa CHADEMA.

inabidi hapo tumalizie, ........Hasa nikigombea urais kwa tiketi ya chadema.
 
Hapa namjuwa Jakaya tu,huyu mwengine sijui nani?.Hii chupa sina uhakika ni ya nini lakini imefanana na ya mvinyo.Mtumiaji wa hicho kinywaji inaonekana ni huyu jamaa mwengine, kwani glasi na vikombe viko kwake.Kikwete inaonekana hana kiu ya hicho kinywaji ndio maana ameamua asome gazeti lake.

Si mvinyo zote zenye kilevi!!
 
8E9U0051.jpg

Slaa: Mheshimiwa Rais, Siku ile ninasoma ile list of shame pale mwembe yanga hadi leo kwa nini hujachukua hatua za kuwawajibisha wahusika.

Rais: Bwana Slaa, ebu nikumbushe hiyo list iko vipi tena?

8E9U0063.jpg

Slaa: Soma vizuri hii list mheshimiwa Rais, mtu wa kwanza kuwajibika ni wewe mwenyewe mheshimwa Rais
 
No; 1 anamwambia inabidi ugombee uraisi ili ulete upizani wa kweli mkiniacha na kina lipumba nitonekana kituko kwa wenzetu wa nje,maana hawa wemegombea mara nyingi watu wameshawazoea lkn wewe bado hivyo njoo bw utoe changamoto!
 
8E9U0051.jpg

unaposema sisi ni vyama vya msimu unakosea sana, kwa kweli hivi sasa tunakubalika mno, mijini na vijijini yaani Tanzania nzima, hata repoti zianaonesha hivyo.
8E9U0063.jpg

hahahahahahahahahahahaha, walahi soma vizuri hiyo report ya synovate inaonesha ni jinsi gani ninavyokubalika, haijachakachuliwa hata kidogo ni ukweli mtupu wala usishangae. Ukitaka ya Daily news na yenyewe nitakupa.

picha hisani ya michuziblogspot
:smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:
 
JK anamuambia Slaa aisee mzee siku ukifanikiwa kuingia ikulu ahadi zote ulizowaahidi wadanganyika huyeyuka, Slaa anajibu subiri uone baada ya uchaguzi huu...
 
Back
Top Bottom