Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 330
- 1,244
Mwanangu,
Kwenye maisha, si kila mlango unahitaji kugongwa,
si kila siri unapaswa kuijua,
na si kila ukaribu una maana ya kwamba una ruhusa ya kuvuka mipaka.
Heshimu mipaka ya watu.
Kuna watu hawapendi kuulizwa maswali ya faragha.
Kuna wengine hujificha nyuma ya tabasamu, na si kwa sababu wanafuraha bali kwa sababu wanapambana kimya kimya.
Usivunje ukuta wao kwa makusudi kwa kisingizio cha "kujua ukweli".
Mwanangu,
Upendo wa kweli una heshima.
Urafiki wa kweli una mipaka.
Na utu wa kweli una mpaka wa kusema, "Hili si langu, nitaliacha."
Kumbuka: Mtu anapokupa nafasi ya kuwa karibu naye,
anakuamini… usivunje mipaka.
Kuwa mwangalifu na maneno yako, kauli zako, na vitendo vyako.
Kwani mara nyingi huwezi kuomba msamaha kwa jambo ulilovuka mipaka kabla hujajua madhara yake
BABU