Zingatia haya kipindi cha sikukuu

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Uhali gani ndugu! bila shaka umzima wa afya na unaendelea kufurahia kipindi hiki cha mapumziko ya Sikukuu za kufunga mwaka.

Kama hali yako sio njema, nakupa pole na Mungu aweze kukuvusha uondokane na kikwazo kinachokukabili iwe ugonjwa au tatizo lolote.

Kwa hali yoyote ile ni wazi kuwa kipindi hiki cha Sikukuu ni kipindi chenye hekaheka na matukio mengi ya furaha na huzuni.

Matukio mengi huambatana na kipindi hiki ikiwemo Sherehe za hapa na pale kama Ubatizo, matambiko na matendo mengine ya furaha.

Hata hivyo kipindi cha Sikukuu ni kipindi Kigumu kwa sababu kinahusisha ongezeko la matukio ya huzuni kama vile ajali za barabarani, ujambazi, wizi na vifo.

Kadhalika katika Kipindi cha Sikukuu bei za bidhaa hasa vyakula nazo hupanda kwa sababu ya mahitaji kuongezeka.

Yapo mambo kadhaa ambayo mtu au jamii huweza kufanya kuongeza neema na kupunguza matatizo kipindi hiki cha Sikukuu.

Kwa mtu mmoja ni vizuri kuepuka vitendo kama ulevi, ili kuepuka usumbufu utokanao na ulevi kama vile kupotea na kuanzisha Vurugu.

Kuepuka kutembelea maeneo yenye usalama hafifu mfano maeneo ya fukwe ambayo hayana ulinzi wa kutosha hii itakusaidia kuepuka vibaka na wanyang'anyi.

Wakati huohuo epuka kuendesha chombo chochote cha moto ukiwa umelewa.

Kama kuna uhitaji wa kutumia chombo cha moto unachomiliki ikiwa umelewa mtafute mtu mwingine akuendeshe.

Pia ni muhimu kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya vyombo vya moto kama gari na pikipiki mfano kwenda eneo la mita 500 ambalo kwa mguu linafikika kirahisi.

Kufanya hivyo kutakupunguzia uwezekano wa kupata ajali.

Epuka ukaribu na makundi ya watu yenye Viashiria vya tabia kama wizi, uvitaji bangi na matumizi ya dawa za kulevya, ili kuepuka uwezekano wa kukamatwa na vyombo vya dora ukaamkia lumande.

Kama hali yako ya Kiuchumi ni ya chini basi jitahidi kuchagua maeneo sahihi ya starehe yanayolingana na hali yako ya Kiuchumi ili kuepuka usumbufu kama vile kushindwa kulipa bili ya huduma.

Sio hivyo tu kama huna hela ya kutosha ukaenda viwanja vya watu wa kishua ukaona matanuzi yao unaweza kupata kishawishi cha tamaa ya kuiba au kunyang'anya jambo ambalo ni hatari kwa usalama wako.

Kama huna hela kabisa basi usitoke kabisa kwenda eneo la starehe kama hujaalikwa na mtu baki nyumbani na familia yako ule kilichopikwa Siku iishe ulale.

Kama wewe ni mzazi wa watoto epuka kuwapeleka watoto wako Viwanja vya starehe vya watoto wa kishua wakati wewe huna fedha ya kutosha kuwalipia, wakifika huko watawaona wenzao wanavyong'ara na itawapa msongo wa mawazo na kujiona hawana thamani mbele ya watoto wa kishua.

Katika kujenga upendo na ubinadamu katika Kipindi hiki cha Sikukuu wasaidie majirani, ndugu wasio na uwezo wa kula, kuvaa Kama wewe Mungu atakuongezea ulipotoa.

Wakati unafanya yote hayo usisahau kuudhuria ibada ili matendo yako yote yaliyomema yabarikiwe zaidi na upate neema mbele ya Mungu.

Heri ya Krismas na Mwaka Mpya.

Peter Mwaihola
IMG_16719814749239218.jpg
 
Wewe mtoto bado hujakomaa lala kwanza.

Sisi kaka zako tunakabiliana na hali zote na huu ndo uanaume.Tumeishi Mbeya enzi za nondo na tilitembea usiku,Arusha enzi za kisu kisu na tulitembea usiku,Dar enzi za panyaroad na tulioshi tutakavyo,South Africa uhalifu ni kama chai.

So usituletee ujuaji saaana wewe mtoto wa juzi,na Jf umeijua juzi.Endelea kuwa chawa wa CCM na si kutupangia maisha sawa eee.
 
Wewe mtoto bado hujakomaa lala kwanza.

Sisi kaka zako tunakabiliana na hali zote na huu ndo uanaume.Tumeishi Mbeya enzi za nondo na tilitembea usiku,Arusha enzi za kisu kisu na tulitembea usiku,Dar enzi za panyaroad na tulioshi tutakavyo,South Africa uhalifu ni kama chai.

So usituletee ujuaji saaana wewe mtoto wa juzi,na Jf umeijua juzi.Endelea kuwa chawa wa CCM na si kutupangia maisha sawa eee.
Hayajakukuta, hivyo hauwezi kuthamini andiko hili.
 
Back
Top Bottom