Zinduka: Siasa inanunua watu, Polepole naye kanunuliwa

munirah

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
551
218
Nimekuwa mfuatiliaji wa mazungumzo ya kisiasa na maendeleo ya nchi hii huu mwaka wa 10 sasa na nimekuwa nikivutiwa na wachambuzi wengi mmoja akiwa Humphrey Polepole!

HP ni mchambuzi mzuri ambaye huwa hamumunyi maneno wala kuegemea upande flani hasaa kama ulipata kumuona anavyochambua maswala ya kisiasa runingani!

Leo kupitia chanel 10 ndugu yangu huyu amenifanya nione kwamba siasa inanunua watu! HP leo anashikilia hoja kuwa mgombea wa urais hapaswi kuwa na kashfa. Hapa moja kwa moja ana mlenga ENL (iko wazi) na hata kumtaja kabisa huku akisahau hulka yake ya kuongea facts huku akilenga pande zote husika! HP anashindwa kutumia akili ya kawaida kwamba hata Mh. Magufuli ana kashfa nyingi anamwegemea Mh ENL kana kwamba alitumwa kuja kutuaminisha uozo wa ENL hivyo hatupaswi kumpa kura abadan!

HP, waTz wa sasa wana akili sana! Mbinu chafu zilipitwa na wakati! Watu leo tunahoji na ikiwezekana kuwajibisha! Lowassa ana dhambi zake tena nyingi tu na kitendo cha kuamua kwenda UKAWA ni sawa na kuungama kwa tafsiri ya haraka hivyo usiwaaminishe watu kuwa kila mwenye kashfa hafai! Baba riz1 alikuwa na kashfa na alitajwa kwenye list of shame lakini bado watanzania wakamuona anafaa kuwaongoza wakampa dhamana hiyo!

HP nakushauri utulie kipindi hiki maana sasa utatumika kwa kununuliwa kimkakati kuvuruga akili za watz..

Wadau, kama channel 10, itaendelea kuleta wachambuzi ambao ni bias , kama Humphrey polepole, ni lazima tuikache hii TV kama tulivyo ikataa TBC na star TV, huyu jamaa kutumwa ila amekula vidonge vyake humu JamiiForums na walio mpigia simu wamemchana.

Huyu jamaa siyo mchambuzi huwezi kumshambulia MTU eti ni fisadi , kwamba mwaka 1995 Mwalimu nyerere alimkataa, kama alikuwa fisadi kwanini alipewa uwazili Mbele ya macho ya nyerere, Polepole anasema eti kama CCM ingepitisha mgombea mwenye tuhuma angetembea tanzania nzima kuzungumza ukweli , kapigiwa simu akaulizwa kuwa Maghufuli ni msafi?

Tuhuma za kuuza nyumba za taifa ?

Repoti ya CAG?

Hakujibu anabaki kusema Lowasa ni fisadi?

Nafikiri watanzania kwa umoja wetu watu kama hawa akina Polepole tuwakatae na kuwapuuza ikiwezekana kuwazomea kabisa na Television zinazo leta watu wa namna hii tuzichukie na tusifuatilie vipindi vyao.

Tunataka mabadiliko kama UKAWA siyo wasafi waache wachukue nchi pengine itakuja kuzaliwa kitu kingine Mbele ya safali siyo CCM ituaminishe kuwa ndio wako safi wakati ni mbwa mwitu na fisi wakubwa eti taiga kubwa kama hili liongozwe na mawazo ya Nape, Magufuli na Kinana watanzania tuna matatizo mengi CCM mnataka mtuaminishe na tuyasahau matatizo yetu wakati Wa uchaguzi, hamtatuweza hii ni mwendo mdundo mpaka kieleweke,

Kama Prof.Lipumba amezingua na Dr.Slaa bado analegalega lakini watanzania bado wanaamini katika mabadiliko ndio kwanza watu wanaongezeka itakuwa Humphrey Polepole mchumia tumbo alie tumwa na CCM hamtamzuia Lowassa kuiona ikulu hii ni safari ya mabadiliko nje ya CCM ,

Mwendo mdundo mpaka Ikulu, UKAWA PAMOJA TUTASHINDA.

Channel 10 itapotea kwenye macho ya watazamaji wengi kama ilivyopotea TBC, na magezeti ya Uhuru na Mzalendo kwenye mbao za magezeti nchini. Kama channel 10 ikiendelea kuleta watu kama Humphrey Polepole na uchambuzi wao wa kisiasa usiozingatia ukweli basi watazamaji wataisusa tv hiyo mara moja.

kupitia channel 10 Polepole alisema kuwa CCM ilipaswa kuwakata Lowassa, Pinda na Membe kutokana na aina ya kampeni zao walivyoziendesha zingekigawa chama chao cha CCM kama majina yao yangefikishwa kwenye NEC kutokana na kutawaliwa na makundi.

Lakini hakusema kuwa Lowassa alipaswa kukatwa jina lake kutokana na ufisadi wala usafi wake kwa taifa. Ghafla akairukia chadema kuwa wamemsimamisha Lowassa ambae ni fisadi, kila mtu alishangaa aina ya uchambuzi wa Polepole kupitia kituo cha channel 10.

Mara akatuambia kuwa Lowassa anatuhumiwa kuwa fisadi na kutuhumiwa ni kubaya, lakini ameshindwa kujibu tuhuma za Magufuli kutuhumiwa kuwauzia nyumba za serikali ndugu yake na msichana wake bila kufuata taratibu. Polepole anataka chadema wao wafanye maamuzi yao kwa kutumia tuhuma tu bila kufuata sheria lakini CCM wao ndo wafuate sheria na sio tuhuma za mtu.

Polepole aliendelea kuwashangaza watazamazi wa kipindi pale wana CCM kama yeye kutaka kuwachagulia UKAWA mtu sahihi wa kugombea urais, kila mtu alidhani kuwa kila chama kina mipango yake kwa mujibu wa katiba yao na sheria za nchi na wapiga kura ndio watakaoamua ni mgombea yupi wa kutoka chama gani anawafaa na sio Humphrey na wenzake.

Kufanya hivyo ni kudharau uwezo wa wananchi sawa na CCM ilivyodharau uwezo wa wananchi kwenye kura za maoni za wagombea wa CCM, kura za maoni za rasimu ya katiba ya Warioba na kura za maoni ya kuanzisha vyama vingi nchini. Kupuuza maoni ya wananchi ni hurka ya wana CCM, wanadhani kuwa wao wanafahamu zaidi kuliko wananchi, wanadhani wao wanajua kile wanachotaka wananchi.

Magufuli yupo na Lowassa yupo tuwaache wapiga kura waseme wenyewe nani anafaa sio Humphrey.

Maswali Matano kwa Rafiki yangu humphrey Polepole

1. Kwa kuwa viongozi wa CCM ndio walikua mstari wa mbele kukwamisha maoni ya wananchi kwenye Katiba mpya, kwanini usifanye kampeni ya watanzania kuwakataa viongozi wote wa CCM badala ya Lowassa peke yake?

2. Umesema wapo watu ndani ya CCM waliokua "wanamkakati" wa kukwamisha maoni ya wananchi, mbona hujawataja wote badala yake umemtaja Lowassa tu?

3. Kabla Lowassa hajajiunga UKAWA hukuwahi kutaja hadharani majina ya waliokwamisha mchakato wa Katiba. Ulisema wapo lakini hukuwataja kwa majina. Sasa leo umemtaja Lowassa baada ya kuhamia UKAWA. Na umemtaja yeye tu. Je watu watakosea kuamini ipo "nguvu" nyuma yako? Maana inaonekana Lowassa angebaki CCM usingemtaja.

4. Umesema "wanamkakati" walioshiriki kukwamisha maoni ya wananchi hawafai kuwa viongozi. Kwa "ground" hiyo umempinga Lowassa kugombea Urais. Vp hao "wanamkakati" wengine waliobaki mbona hupingi wao kuwa viongozi. Japo siwajui lakini naamini wapo wanaogombea Ubunge, mbona huwapingi kama unavyompinga Lowassa? Au ubunge sio uongozi?

5. Kwa kuwa Lowassa alipanga "mkakati" wa kukwamisha maoni ya wananchi akiwa CCM, it simply means ukimkataa Lowassa leo, watazaliwa akina "Lowassa" wengine ndani ya CCM na kuendelea kuumiza wananchi. Sasa je kwanini usifanye kampeni ya wananchi kuikataa CCM kwa ujumla ili isizalishe kina "Lowassa" wengine, badala ya kupoteza nguvu nyingi kupambana na mtu mmoja na kuacha kupambana na mfumo?

6. Umesema utafanya kampeni ya kumkataa Lowassa kuwa Rais. Kwa ninavyoelewa kampeni ya kumkataa "Rais" inabidi ifanyike kwa nchi nzima. Bila shaka itakuwa na gharama. Je nani anafadhili kampeni yako? Kwa maslahi gani? Kwa kuwa umeonesha upendeleo dhahiri kwa CCM (Mfumo) je tukisema ndio wanaofadhili kampeni hiyo tutakuwa tunakosea?

Wasalaam,
Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!

HUMPHREY POLEPOLE NA SIFA ZA KIJINGA.

Na Mayembarose.

Sote tunakumbuka vizuri namna mchakato wa katiba ulivyokwenda tangu kuanza hata hitimisho lake. Sote tunafahamu namna tume iliyokuwa inaongozwa na mzee wetu Joseph Warioba ilivyofanya kazi ngumu ya kuhakikisha inakusanya maoni ya wananchi na kuhakikisha katiba inatokana na maoni hayo.

Sote tunaikumbuka vizuri rasimu ya kwanza ya Warioba na maboresho yake.hata rasimu ya pili iliyopelekwa bungeni kujadiliwa kwa makundi mbalimbali.

CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao ambaye ndiye Rais wetu walikuwa wa kwanza kupinga maoni ya wananchi na kuweka maoni yao kwa kuzingatia maslahi yao binafsi.

Nakumbuka Jaji Warioba na akina Humphrey polepole walifedheheshwa sana na chama chama mapinduzi kwa kudharauliwa kwa kazi kubwa waliyoifanya. Faraja kubwa waliipata kwenye umoja ulioitwa UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI( UKAWA). ambao walihakikisha maoni ya wananchi hayapuuzwi.

CCM kwa umoja wao( Ama naweza kusema mfumo wa chama chao) uliwalazimu wote kupinga maoni ya wananchi tena kwa kura ya wazi,wazi kabisa.

Mhe Joseph Warioba, Humphrey polepole, tume nzima ya katiba pamoja na nguvu kubwa ya UKAWA walijitahidi kwa kadri walivyoweza kuhakikisha maoni ya wananchi yanalindwa lakini walijikuta wanaangukia pua kwa uchache wao. Wakaamua kuachana na bunge hilo maalum lililokuwa na kila dalili za kudharau na kupoka haki ya msingi ya wananchi ya kuunda katiba itakayobeba maslahi yao.

KWAKO KAKA YANGU POLEPOLE.

kuna bandiko nimelisoma Leo kwenye ukurasa wako wa FACEBOOK. Umejaribu kugusia suala la katiba kwa kuhusisha na uchaguzi Mkuu ujao. Kwa ujumla wake umejaribu kumkataa MHE EDWARD NGOYAI LOWASA kwa kuwa alikuwa sehemu ya waliokwamisha katiba ya wananchi isipatikane. Haya ni maajabu kwelikweli.

Hebu nikuulize swali.

Ni mwanaccm gani aliyetoka kifua mbele na kuikataa katiba pendekezwa ambayo ilipuuza maoni ya mamilioni ya watanzania?

Hebu nitajie japo wabunge watano tu wa CCM waliounga mkono maoni mliyokusanya wewe na timu yako. Au la basi wawezaje kuhukumu mmoja kati ya wengi waliolazimishwa na mfumo ili kutimiza matakwa yao?

Inasemekana utazunguka Tanzania nzima kumpinga RAIS WANGU MHE LOWASA eti kwa kuwa aliikwamisha katiba, Je MAGUFULI alionyesha juhudi gani kuhakikisha katiba yenye maoni ya wananchi inapatikana?
(Labda kama utatuletea mgombea wako tofauti na hawa tulionao)

NADHANI UMELEWA SIFA.
Baada ya watanzania kukuamini sasa unafanya yako.unadhani kwakuwa uliisimamia katiba basi ni rahisi kuwahadaa watanzania kwa kadri uwezavyo.Umesahau kama mema elfu moja hufutwa na baya moja tu.

Jitafakari upya tena.

Which ground do you stand to throw stones to Lowasa? POLEPOLE

Polepole jibu haya tuone Usafi wako kama unavojinasibu twambie kuhusu mradi wa Kituo cha vijana uliokuwa wa dola laki sita chini ya TYC kwa ushirikiano na shirika toka Denmark ukifadhiliwa na DANIDA kwanini mkataba ulisitishwa kabla hata ya miaka miwili. Kama wewe ni msafi
kwanini MS Tanzania ili terminate mkataba na TYC chini ya uongozi wako?
kwanini MS walisitisha program ya interns toka Denmark

Ukiwa kama mkurugenzi, Polepole ukiweza kufanya siasa na kuua kabisa Steering Committee iliyokuwa inasimamia shirika hivyo kubaki na shirika kama yeye na alikuwa na mamlaka zote ikiwemo kuwa na uwezo wa kutoa fedha bila wengine.

Kati ya 2007-2008 kilikuwa na ushirikiano na shirika moja la Denmark kwa jina la FIC ambapo kwa pamoja kuliundwa joint proposal TYC likiwa implementing partner kwa upande wa Tanzania FIC likiwa Denmark.

Mradi ulifanya kazi kwa mwaka mmoja tu kabla ya kusimamishwa na walibadilisha washirika ambapo TYVA, Open Mind na African Youth ndo watekelezaji wa mradi huo mkubwa.

Mambo yaliyosababisha mradi kusitishwa ni pamoja na yafuatayo.
1. Waajiriwa kuto kulipwa mishahara kama ilivyopangwa na memngine kama Bima ya Afya na NSSF

2. Udanganyifu katika malipo ya washiriki wa mafunzo-kwa mujibu wa bajeti, walitakiwa kila aliyekuwa anahudhuria mafunzo alipiwe nauli ya 10,000/= lakini kwa uhalisia kwa kushirikia na wasimamizi wa fedha Polepole alibadilisha hili wakawa wanawalipa 2,000/= mpaka siku ya monitoring wazungu walipokuja kwenye kikao wakapewa orodha ya washiriki ikionyesha wamelipwa 10,000/= tofauti na rekodi ambazo ambazo walishapewa na maafisa wa kituo maana walitonywa mapema na watumishi wale juu ya huo udanganyifu.

3. Financial Mismanagement generaly

Baada ya haya kutokea, FIC na MS Tanzania (Wakati huo - baadae MS ilijiunga na Action Aid) waliamua kufanya joint audit ambayo ilionyesha gross mismanagement of money especially implicating Polepole.

Mradi ulisimamishwa hapo hapo kumbuka kwa ukubwa wa mradi kodi ya ofisi tu kwa mwezi ilikuwa $1,500

MS walikuwa wafadhili since2004 ila walijitoa ufadhili that very time.

Kuna programu ya wazungu walikuwa wanakuja for intership kila baada ya miezi mitatu kwa kushirikiana na MS hiyo kuna wakati alituhumiwa na baadhi ya wasichana ku ripoti kwamba alikuwa nawanyanyasa kingono kwa maana ya kuwataka kwa lazima kimapenzi. Mradi ulisimamishwa hapo hapo......POLEPOLE HAKUJIBU MASWALI HAYA KAMA KWELI YEYE NI MSAFI. Jibu haya tukuulize mengine!

Pole Pole una dhambi ya kujibu kwa vijana waliokuamini

Kwangu Mungu binafsi maadui wakuu wa vijana wa Tanzania ni Pole Pole na Ruge wa clouds....lakini vijana wenyewe hamjijui....simuongelei Ruge hapa,,, ntamuoongelea Humphrey,

  • Tanzania mpaka sasa haina baraza huru la vijana....imekuwa agenda ya nenda rudi ili kuimarisha UVCCM kuwa ndio taasis ya kitaifa ya vijana...Pole pole ametumika n NGO yake kule kinondon na kiijtonyaama since JK akiwa foreign kwenda ktk mikutano mbali mbali ya kiamataifa kama mwakilishi wa baraza hewa la vijana la kitiafa nchini.....nilishawai hudhuriia mkutano wa vijana wa africa mashariki arusha chini ya EAC mwaka 2005... kati ya nchi zote za africa mashariki ni tanzania pekee aikuwa na youth council lakini ikielezwa mikutano yote ya National youth council iliudhuriwa na NGO ya pole pole.....!! kwa NGO yake kukumbatiwa na serikali kama kivuli ilififisha juhudi zote za kuwa na National youth council ktk Tanzania....mpka leo hii anaingizwa katika tume ya katiba ni ukaribu wa NGO yake na serikali kama ndio National youth council....
  • Pole pole binafs namjua ni mwanaaharakt toka akiwa shulen...ni mdogo wangu sana...alikuwa kabla ya kujipachika ukaribua wa jk na NGO yake alikwa mkereketwa wa kuwa na baraza la vijana , na vikao kadhaa za NGOs za vijana alishiriki lakini alishirki akijua yeye ndio nguru mbili huku anaondoka nchini kwa jina la baraza la vijana.
  • Pole pole ni kati ya vijana wanaofungia vijana wengine nafasi katka ngazi mbal mbali....ikiwa kijana unanunuliwa kutumikia mtu fulan, au kundi unawagawa wanakuona role model...pia hata wateuzi wanasema vijana hawako serious au watoto hawalali na pesa.....nikichukulia la katiba na uchaguzi....!! mf katiba....Sijawahi msikia pole pole akilia au kuongea hadi mishipa imtoke kama tatizo la vijana kukosa barza huru la kitaifa? ni hoja aliokuwa nayo toka mdogo lakini alipofika miaka 20 pale kijitonyama akanunuliwa akawasaliti vijana na mpka saasa ujana unamtoka nafsi yake itamsuta na atakufa nayo moyoni.... Uchaguzi, iweje leo pole pole alikuwa anawakirisha vijana katka tume ya katiba....na tume nzima ilikiri kazi yao imeddharauliwa na CCM,kupitia bunge la katiba na kunyofoa ...na matusi yote...leo hiii CCM ni wazzuri wa kuwapigia debe....ikiwa bado uchakuachuaji ule bado unaendelea? hivi ulikuwa ktk midahalo ile kiunafiki? uliongea na vijana kutoa ukweli wa tume kudharauliwa?? kumbe uliteuliwa katika tume kama mwanaccm...uvccm? leo hii umaarufu na heshima ya tume watu walikupa umeona ni wakti muhimu kutumia umaarufu huo kumshambulia Lowassa?? si shida ya wewe kuwa na haki kumshambulia lowassa kwa ufisadi ww ni mtanzania una haki lakin je...vijana waendelee kukuamini kuwa ww ni mwakilishi wao? vijana wanaotaka mabadiliko na wanaamini katika lowasa wanajiluliza kama wewe ni mzalendo...mbona hujwawakilisha vijana kuwatukuna watu mafisadi wengine ndani ya ccm...kwa nini umtaji Chenge?? tabaijuka? Muhongo? Ngereja? kwa ufisadi wa wazi na brother wako Jk amewapitisha katika katk kura za maoni za ubunge....hivi ni kweli vijana waendelee kukuamini wewe ni mwakilishi wao??
  • Vijana uliokuwa unawawikilsha ktk tume wanakueshimu sana...kwa nguvu zako binafs toka ukiwa shule....pole pole hujabebwa na mtu kufikia katka ngazi za midahalo na hadi kuwa na NGO....high expactation na uwezo kuingia kila mahali vilikugeuza kuwa unaweza kuwasliati vijana wenzako.......!!LOWASSA unaemkshifu kumbuka ana vijana wanaomamini sana tena wengi na hao vijana pia wanakuamini ww na kukusehsimu....LAKINI vijana wenzako wameamua kukata mfumo huu wa vijana kununulika....vijana wa tanzania njaaa imearibu mapigano yetu ya maendeleo...nchi haina strategy ya kubuild vijana kutake part ya leadership..ni vizaz vilivopo katk madaraka ndio wamewekewa mipango kurithi mamlaka....na pole pole ameona ndio fursa kuaingia ktk system hii.....!!

Binafsi nasema niwe hai au maiti iko siku ccm itatoka madarakani tu......CCM ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya vijana....!!!
 
Mie mwenyewe nimemshangaa sana anasema kiongozi hapaswi hata kutuhumiwa anapotuhumiwa tu yatosha kumtoa uongozini kweli lakini alivyosema kwamba waliotuhumiwa CCM ni wengi na angepitishwa mmojawapo kati ya hao watuhumiwa angepita mikoani kusema watu wasimchague vipi kuhusu magufuli JE YEYE HAJAWAHI KUTUHUMIWA au ndo double standard.
 
Usimwamini mtu yeyote akiisha sema yeye ni mwana ccm... Polepole nae ni walewale kwenye some issues.. maana ccm ukimpiga mpinzani au ukimponda basi unapata ulaji... unadhani Polepole nae hapendi huo ulaji? Hapendi asomeshe watoto wake shule nzuri? Thubutu......
 
Wadau, kama channel 10, itaendelea kuleta wachambuzi ambao ni bias , kama Humphrey polepole, ni lazima tuikache hii TV kama tulivyo ikataa TBC na star TV, huyu jamaa kutumwa ila amekula vidonge vyake humu JamiiForums na walio mpigia simu wamemchana.

Huyu jamaa siyo mchambuzi huwezi kumshambulia MTU eti ni fisadi , kwamba mwaka 1995 Mwalimu nyerere alimkataa, kama alikuwa fisadi kwanini alipewa uwazili Mbele ya macho ya nyerere, Polepole anasema eti kama CCM ingepitisha mgombea mwenye tuhuma angetembea tanzania nzima kuzungumza ukweli , kapigiwa simu akaulizwa kuwa Maghufuli ni msafi?

Tuhuma za kuuza nyumba za taifa ?

Repoti ya CAG?

Hakujibu anabaki kusema Lowasa ni fisadi?

Nafikiri watanzania kwa umoja wetu watu kama hawa akina Polepole tuwakatae na kuwapuuza ikiwezekana kuwazomea kabisa na Television zinazo leta watu wa namna hii tuzichukie na tusifuatilie vipindi vyao.

Tunataka mabadiliko kama UKAWA siyo wasafi waache wachukue nchi pengine itakuja kuzaliwa kitu kingine Mbele ya safali siyo CCM ituaminishe kuwa ndio wako safi wakati ni mbwa mwitu na fisi wakubwa eti taiga kubwa kama hili liongozwe na mawazo ya Nape, Magufuli na Kinana watanzania tuna matatizo mengi CCM mnataka mtuaminishe na tuyasahau matatizo yetu wakati Wa uchaguzi, hamtatuweza hii ni mwendo mdundo mpaka kieleweke,

Kama Prof.Lipumba amezingua na Dr.Slaa bado analegalega lakini watanzania bado wanaamini katika mabadiliko ndio kwanza watu wanaongezeka itakuwa Humphrey Polepole mchumia tumbo alie tumwa na CCM hamtamzuia Lowassa kuiona ikulu hii ni safari ya mabadiliko nje ya CCM ,

Mwendo mdundo mpaka Ikulu, UKAWA PAMOJA TUTASHINDA.

Channel 10 itapotea kwenye macho ya watazamaji wengi kama ilivyopotea TBC, na magezeti ya Uhuru na Mzalendo kwenye mbao za magezeti nchini. Kama channel 10 ikiendelea kuleta watu kama Humphrey Polepole na uchambuzi wao wa kisiasa usiozingatia ukweli basi watazamaji wataisusa tv hiyo mara moja.

kupitia channel 10 Polepole alisema kuwa CCM ilipaswa kuwakata Lowassa, Pinda na Membe kutokana na aina ya kampeni zao walivyoziendesha zingekigawa chama chao cha CCM kama majina yao yangefikishwa kwenye NEC kutokana na kutawaliwa na makundi.

Lakini hakusema kuwa Lowassa alipaswa kukatwa jina lake kutokana na ufisadi wala usafi wake kwa taifa. Ghafla akairukia chadema kuwa wamemsimamisha Lowassa ambae ni fisadi, kila mtu alishangaa aina ya uchambuzi wa Polepole kupitia kituo cha channel 10.

Mara akatuambia kuwa Lowassa anatuhumiwa kuwa fisadi na kutuhumiwa ni kubaya, lakini ameshindwa kujibu tuhuma za Magufuli kutuhumiwa kuwauzia nyumba za serikali ndugu yake na msichana wake bila kufuata taratibu. Polepole anataka chadema wao wafanye maamuzi yao kwa kutumia tuhuma tu bila kufuata sheria lakini CCM wao ndo wafuate sheria na sio tuhuma za mtu.

Polepole aliendelea kuwashangaza watazamazi wa kipindi pale wana CCM kama yeye kutaka kuwachagulia UKAWA mtu sahihi wa kugombea urais, kila mtu alidhani kuwa kila chama kina mipango yake kwa mujibu wa katiba yao na sheria za nchi na wapiga kura ndio watakaoamua ni mgombea yupi wa kutoka chama gani anawafaa na sio Humphrey na wenzake.

Kufanya hivyo ni kudharau uwezo wa wananchi sawa na CCM ilivyodharau uwezo wa wananchi kwenye kura za maoni za wagombea wa CCM, kura za maoni za rasimu ya katiba ya Warioba na kura za maoni ya kuanzisha vyama vingi nchini. Kupuuza maoni ya wananchi ni hurka ya wana CCM, wanadhani kuwa wao wanafahamu zaidi kuliko wananchi, wanadhani wao wanajua kile wanachotaka wananchi.

Magufuli yupo na Lowassa yupo tuwaache wapiga kura waseme wenyewe nani anafaa sio Humphrey.
 
kama umemuelewa polepole kachukue katiba ya warioba ambayo ndio chanzo wa haya yote utaelewa ana maanisha nini katika uteuzi wa mgombea ndo uje useme hayo yote.katiba ile imekiukwa
 
Mkatae Lowassa kwanza; alipotetea katiba mpya mlimuona mzungu wa kikoloni mkampa misifa kibao leo katia ndimu katika donda lenu oooh hafai wiki ijayo atachambua uhusiano wa Mnyika na Mbowe
 
kama umemuelewa polepole kachukue katiba ya warioba ambayo ndio chanzo wa haya yote utaelewa ana maanisha nini katika uteuzi wa mgombea ndo uje useme hayo yote.katiba ile imekiukwa

Kama katiba ya Warioba ndiyo anayoisimamia huyu Pole pole mbona ameshindwa kujibu hoja juu ya tuhuma za Magufuli za Uuzaji wa nyumba za serikali na juu ya upotevu wa Tsh. Billion 262 katika wizara yake ambazo hazionyeshi kazi yeyote iliyofanyika na fedha hizo na hii imetokana na ripoti ya CAG na hata Bungeni Magufuli alishindwa kujibu hoja hiyo je kwa tuhuma hizo huyo Magufuli anafaa kugombea Urais kupitia CCM kuringana na katiba ya Warioba?
 
Mkuu labda umgesubiri Jazba ishuke kwanza ndio uandike topic ikiwa imetulia,vinginevyo unakwa kama Polepole in the opposite Direction.
 
Kama katumia katiba ya warioba huyo Magufuli hana tuhuma au ndo umezisahau kwa kuwa ni mgombea wa CCM? Kenyata na Ruto wametuhumiwa Sana ila ndo marais kenya
Mkuu stiki na point yako ya kwanza hayo mambo ya kutuambia kwa kuwa kenya wamefanya na sisi tufanye hatutaki kuyasikia
 
Back
Top Bottom