Zimbabwe

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
ROBERT GABRIEL MUGABE BABA WA AFRIKA PEKEE ALIOBAKI MADARAKANI.

"Tokea kuwa Mwalimu mpaka mpigania Uhuru, sasa rais wa nyakati mpya Afrika"

Na Comred Mbwana Allyamtu.
20/8/2017

MAKALA hii ni Amended Article kutoka Kwenye Toleo [HASHTAG]#namba[/HASHTAG] 116[009/2016]

Moja ya majina maarufu zaidi barani Afrika na hata nchini za magharibi ni Robert Mugabe. Mugabe alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zimbabwe chini ya serekali ya Raisi Banana Canan. Mugabe ndio raisi anayetajwa sana duniani na vyombo vya habari hasa kutokana na visa na vituko vyake visio kwisha kila siku lichomokapo jua.

Ni wazi kuwa kwa sasa, raisi Mugabe wa Zimbabwe ndiye kiongozi aliyebaki Afrika anayeandikwa zaidi na vyombo vya habari duniani. Ujasiri wake wa kupinga sera za Magharibi ikiwemo na masuala ya ndoa jinsia moja yamemfanya kuwa mtu wa kipekee kabisa katika zama hizi za usasa. Sio rahisi kupita wiki bila kumsikia akitoa maneno makali dhidi ya Viongozi wa nchi za magharibi. Ingawa anatajwa na nchi za Magharibi kama kiongozi mbovu na asiyeheshimu Demokrasia lakini bado anakubalika Zimbabwe na Waafrika wengi wanamuona kama shujaa na Simba wa Afrika mpya.

Robert Gabriel Mugabe alizaliwa tarehe 21 Februari 1924 katika familia ya bwana Gabriel Matibili(Alikuwa fundi mwashi) mwenye asili ya Nyasaland (Kwa sasa ni Malawi). Mama yake ni Bi Bona anayetokea kabila la Washona. Alihitimu masomo yake katika chuo cha Mtakatifu Francis Xavier mwaka 1945 katika mji Katuma alipokulia, Aliendelea kufundisha hapo Rhodesia(sasa ni Zimbabwe) na baadaye alikimbilia nchini Ghana huko aliendelea na kazi yake ya ualimu kwa miaka kumi na mitano. Akiwa Ghana alikutana na mke wake wa kwanza Sally Hayfron, wakaoana. Alijiunga na chuo kikuu cha Fort Hare kwa masomo ya ngazi za juu zaidi.

Mwaka 1960 akiwa na digrii tatu, aliacha kazi ya ualimu huko Ghana na kuamua kuungana na harakati za ukombozi wa nchi ya Zimbabwe kupitia vuguvugu la Zanu(Zimbabwe African National Union) na kuchaguliwa kuwa katibu mkuu. Ni katika kipindi hicho ambapo Waungu walioishi Zimbabwe nao walijitangazia uhuru. Aliyekuwa waziri wa fedha katika serikali ya Wazungu nchini Zimbabwe Ian Smith aliteuliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1964. Hakuwa mtu aliyejali nafasi ya watu weusi katika siasa za huko, mtu mwenye msimamo mkali na aliyependa kutumia nguvu kubwa dhidi ya harakati zozote toka kwa Waafrika. Utawala wake ulionekana ni shimo refu kupatikana kwa uhuru wa Wazimbabwe, akitoa kauli kali na za kukatisha tama alisema.

‘Katika maisha yangu yote sioni kama waafrika wanaweza kuwa imara au kuwa na sababu ya kujiongoza; Niseme tu kuwa hakuna kitu kinachoitwa Utawala wa Waafrika katika maisha yangu’
Hakika alimaanisha alichosema kwani miezi mine baadaye yaani Agasti 1964 alipiga marufuku vyama vyote vya kisiasa. Kikiwemo ZANU kilichoongozwa na Mugabe, kama haitoshi aliwaweka Mugabe, Nkomo, Sithole na wanaharakati wengine katika vizuizi.

Robert Mugabe alitumikia miaka kumi na moja kama mfungwa wa kisiasa, Akiwa kizuizini alijikita katika kufundisha wafungwa wengine lugha ya Kiingereza pia aliendelea na masomo kwa njia ya posta katika chuo kikuu cha London. Mwaka 1974, alikimbilia uhamishoni katika nchi ya Zambia baadaya kuachiwa toka kifungo cha kisiasa. Aliendelea na harakati zake za kisiasa huko Msumbiji, Chama cha ZANU kiliendelea kuimarika nje ya mipaka ya Zambabwe.

Mawazo ya kijamaa hasa ya waandishi Karl Marx na Mao yalimbadilisha na kuona kuwa ni mtutu wa bunduki tu ndio ungewezesha kuleta ukombozi wa waafrika. Mugabe alienda Ulaya ya Mashariki na Asia kujifunza mbinu za kijeshi. Lakini pia alipata misaada ya kifedha toka kwa marafiki wengine waliokuwepo Ulaya ya magharibi. Serikali ya Wazungu chini ya Ian Smith ililegeza msimamo wake mwaka 1978 kutokana na kushamiri kwa harakati za kudai uhuru. Ili kujihakikishia maslahi ya wazungu yanalindwa alichaguliwa Askofu Abel Muzorewa kama waziri mkuu wa nchi ya Zimbabwe Rhodesia. Serikali hiyo mpya ilikosa udhibiti kwani hakitambuliwa kimataifa sababu haikujumuisha vyama vya ZANU na ZAPU.

Makubaliano kati ya vyama viwili ZANU na ZAPU yalipelekea kuundwa kwa serikali mpya ya Waafrika mwaka 1979 ambayo pia ilikuwa na wajibu wa kulinda haki na mali za wazungu ambao walikuwa wachache. Baada ya kushinda uchaguzi wa tarehe 4,1980 Mugabe alianza kazi ya kutafuta ushawishi toka kwa makundi mbalimbali wakiwemo wazungu wapatao laki mbili 200,000.

Inaelezwa kwamba katika kampeni za kutuliza upinzani hasa toka maeneo walimoishi wandebele, serikali ya Mugabe ilitumia jeshi na kupelekea vifo vya watu wa kabila. Kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika, Mugabe alikuwa na hofu ya kupinduliwa hivyo basi mwaka 1987 aliongoza muungano wa chama chake cha ZANU na chama cha ZAPU kisha kuunda ZANU-PF. Yeye akawa raisi huku akifuta kabisa mfumo wa vyama vingi nchini Zimbabwe.

Alishinda kwenye chaguzi zote za miaka ya 1990, akiwa katika hali ya kuchoshwa na hali ya wananchi wa Zimbabwe kuwa na ardhi isiyotosheleza kwa kilimo. Mugabe aliongoza mabadiliko ya katiba ya Zimbabwe mwaka 2000, Katiba hiyo ilimpa nguvu zaidi raisi na kuiruhusu serikali kupokonya ardhi yenye rutuba toka kwa wazungu na kuigawa kwa waafrika. Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na uingereza yalipinga mchakato huo, aliitwa kila jina baya, hakujali hata Zimbabwe ikawekewa vikwazo na nchi hiyo. Mabadiliko ya katiba yalizaa chama kipya kilichojulikana kama Movement for Democratic Change (MDC) ambacho kilipinga katiba mpya.

Hali ikiwa bado ni tete, kuliibuka kikundi cha wapigania uhuru wa nchi hiyo waliamua kuvamia na kujigawia mashamba yaliyokuwa yanamilikiwa na wakulima wa wazungu. Machafuko makubwa yalitokea hivyo Wazungu wengi ilibidi kukimbia na kuwaachia Waafrika wakijigawia maeneo. Vurugu na vikwazo vya kiuchumi vilipelekea kuadimika kwa bidhaa muhimu hasa za vyakula.
Mwaka 2008 uchaguzi mkuu ulifanyika huku Mugabe akikabiliwa na upinzani mkali toka kwa kiongozi wa chama cha MDC, Morgan Tsvangirai. Zilikuwa zama mpya katika siasa za Zimbabwe kwani kuliundwa serikali ya umoja wa kitaifa ikishirikisha chama cha ZANU-PF na MDC. Mugabe aliongoza serikali hiyo huku Tsvangirai akiwa makamu wa raisi
Miaka ya hivi karibuni amejikuta katika nguvu kubwa inayomtaka kuondoka madarakani, hata hivyo inaelezwa kuwa amekuwa mkali juu ya matamko yanayomtaka kung’atuka.Alipoulizwa na mwandishi wa gazeti lijulikanalo kama Herald kuwa ataachia lini madaraka ya uraisi wakati wa sikukukuu yake kuzaliwa, alijibu kwa mzaha “Unataka nikutwange ngumi uanguke chini ndipo uamini kwamba bado nina nguvu?” akaendelea “Mbona nikubali kuendelea kuongoza iwapo nina maradhi au ninaugua au siwezi kuongoza?” aliuliza katika sherehe iyo ya kutimiza umri wa miaka 92. Tukio hilo limefuatiwa na lingine la kukamatwa kwa afisa wa polisi anayeitwa Thomson Joseph Mloyi kwa kudaiwa kusema tu kuwa Mugabe ni mzee sana kuwa kiongozi.

Yapo matukio mengi ya kuvutia na hata ya kukera ya raisi mzee zaidi duniani Robert Gabriel Mugabe..............

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu.

copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
Napatika kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Email-
384c685598524d41d997c861cbcb224e.jpg
mbwanaallyamtu990Gmail.com


9bdfd50ffde3fc087fd2a50551527aa4.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom