Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!

Gang Chomba

Hoja zako ni hafifu sorry! Bado umegubikwa na ndoto ya ukoloni ondoa matongotongo. Afrika itasonga mbele tu haiwezi kurudi nyuma.
 
dua...
afrika haiwezi kusonga mbele kwa misingi ya woga na ya kuwasujudia wakoloni kama ambavyo viongozi wenu wengi wa kiafrika wamekuwa wakifanya...mugabe ni shujaa aliyeutafuta na kuupata uhuru wa zimbabwe hivyo hata mkimuita joka kubwa, dikteta na majina mengine mlioamua kumbatiza still atabaki kuwa shujaa tu, na hawezi kumuachia kibaraka nchi.
 
Life in Zimbabwe




Last night the Zimbabwe currency was trading at about Zim$200-million dollars to US$1

With inflation now running at over 165 000%, Zimbabweans get
little change out of two Z$50-million for a single loaf of bread.




Zimbabwe: Catholic Church says Election Commission can no longer be trusted

Source: Fides

© Independent Catholic News 2008



SADC Ministers Fly for Crisis Talks
A delegation from the Southern African Development Community left Luanda, Angola for Harare to hold crisis talks with the regime and follow up the current situation in the country...........................


Zim voters vow to go back home and finish off Zanu PF in re-run

One thing for sure, Zimbabweans are resilient people and believe me Mugabe is living on borrowed .......time just wait and watch.
 
kuporomoka kwa uchumi kunatokana na vikwazo alivyowekewa dua na si uongozi mbovu...mbona toka mwaka 80 uchumi haukuyumba mpaka walipoamua kumbana jemadari yule?
 
..hivi msimamo wa Tanzania kuhusu huu mgogoro ni nini?

..naona Benard Membe yuko kama hayuko.
 
Kheee! hivi nini kinaendelea huko Zimbabwe? Wameshatangaza mshindi wa uraisi au mazingaombwe (kama ilivyo kawaida ya Waafrika) bado yanaendelea?
 
Huyu Mkapa ndio anataka kututoroka kiaina wakati msalaba wake hapa Tz unamsubiri?? Halafu majitu mengine mambo yao yanawashinda huku nyumbani lakini wako mijicho mbele kujifanya kwenda kusuruhisha matatizo ya wengine...Lakini anapoza maumivu tu lazima kichapo kiendelee...
 
..hivi msimamo wa Tanzania kuhusu huu mgogoro ni nini?

..naona Benard Membe yuko kama hayuko.

tanzania haiwezi kuwa na msimamo wowote juu ya zimbabwe kwa sababu ya zanzibar yanawashinda je watayaweza ya zimbabwe?
na kuhusu huyo membe sijui kama ataweza kupiga hata chafya mbele ya mzee mugabe, kwa sababu hana hoja na hawezi kuongea chochote mbele ya comred mugabe...
 
Zimbabwe inanuka damu ,Mkongwe hana hata utu wa kujali wanamchi wake alimaradi aendelee kutawala hadi kifo kitakapomchukua.Mambo mengine kama siasa za mashamba ni michezo tu ya kujaribu kugeuza chuki kuwa mapenzi.msimamo wa nchi za Kiafrika ni unafiki mtupu.
 
Kheee! hivi nini kinaendelea huko Zimbabwe? Wameshatangaza mshindi wa uraisi au mazingaombwe (kama ilivyo kawaida ya Waafrika) bado yanaendelea?

matokeo ya uchaguzi zimbabwe yametangazwa na kibaraka tshivangirai amepata 47% ya kura na comred mugabe kapata 43% ya kura. hivyo kwa mujibu wa katika ya zimbabwe wanatakiwa watu hawa waongezewe dakika 30 au ikiwezekana zipigwe penati.
ila kibaraka tshivangirai amechomoa kurudia kwa uchaguzi.
na kwa mujibu wa katiba ya zimbabwe endapo mgombea atasusia uchaguzi huyo atakayebakia atatangazwa kuwa mshindi, hivyo kama kibaraka tshivangirai ataendelea na msimamo wake huo ni wazi kuwa rais mugabe atakuwa rais tena wa zimbabwe nchi aliyopambana kuhakikisha anaitoa mikononi mwa wakoloni.
 

kipanga...
wala usiwe na wasi wasi juu ya fisadi mkapa, ni wazi kuwa huko anakokimbilia anakwenda kukutana na bingwa wa majibu, bingwa wa hoja, na mtu msomi so atakachokutana nacho huko hawezi kudiriki kukaa huko zaidi hata ya wiki.
 

alnadaby...
zimbabwe si nchi ya kwanza kunuka damu afrika, na kwa kifupi nchi haiwezi kuongozwa na utu tu huo unaoutaka wewe.
tume ya uchaguzi imetangaza matokeo na sasa watu wanajiandaa kurudia uchaguzi, sasa ni kitu gani kinawafanya mnamchukia "bob" jamani? kama ni katiba anaifuata na ndio imemuweka mpaka leo madarakani, so nyie wazalendo wa kikwete mnamchukia nini mzee wa watu?
 
Mass challenge over Zimbabwe poll



Gukurahundi by any other name



No Arrests made

South African investigators arrive





MDC supporters say they have
been attacked by Zanu-PF supporters





Zanu-PF groups are accused of
destroying MDC supporters' property


Huyu fedhuli hawezi kuondoka kwa amani ataondoka tu kwa Mtutu wa Bunduki kama alivyoingia.
 
ZANU PF admits Violence


Yaani sasa Mugabe na thugs wake watakiona cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya maana bila International observours hakuna re-run ile propaganda yake ya wakoloni imeshindwa kufanya kazi. Yeye ndiye amekuwa mkoloni
 
dua la kuku hilo, nadhani hujamjua mugabe ni nani na huwa hababaishwi na mkoloni yeyote...yeye anawasikiliza makamanda wake waliopambana kumng'oa mkoloni kisha ndo wanaendesha nchi na si vibaraka kama MT.
 


On Saturday, Ivorians in the annual Popo Carnival in Bonoua recreate a scene from colonial times, when the first French governor of Ivory Coast went on his travels.





Zimbabweans sell dried fish over the border
in the Mozambican town of Manica, a popular
destination for Zimbabwean traders.


Sasa mkoloni kawa Mugabe and his thugs.
 
dua naomba tuufunge huu mjadala mpaka maestro robert "bob" mugabe atakapoapishwa...adios
 
Mugabe hints at exit

Ati Anataka miaka miwili kilichomshinda miaka 28 ni kipi? Machozi ya mamba. Zimbabweans have decided whatever the cost he must go .................
 
Mpatanishi mkuu katika mzozo wa Zimbabwe rais Thabo Mbeki wa Afrika kusini , amewasili leo mjini Harare kwa mazungumzo na rais Robert Mugabe kwa ziara yake ya kwanza tangu kutangazwa rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais.

Mbeki ambaye anakosolewa kwa kuchukua msimamo laini dhidi ya rais Robert Mugabe, anatarajiwa kukutana na kiongozi huyo mkongwe wa Zimbabwe, lakini haijafahamika iwapo atakutana pia na upande wa upinzani.Kiongozi wa chama cha MDC Morgan Tsvangirai hivi sasa yuko nje ya nchi hiyo akikutana na viongozi wa Afrika pamoja na wanadiplomasia katika juhudi za kuongeza mbinyo dhidi ya Mugabe mwenye umri wa miaka 84 kujiuzulu baada ya miaka 28 ya utawala wake.

Chama cha MDC pia kimesema kuwa hakipangi kushiriki katika uchaguzi wa duru ya pili. Tsvangirai hajatoa jibu kamili iwapo atashiriki katika uchaguzi huo na iwapo hatatoa jibu kamili Mugabe mwenye umri wa miaka 84 atakuwa mshindi moja kwa moja.

Pia chama cha MDC kimesema kuwa hadi sasa hakijapata mwaliko kutoka kwa Mbeki kukutana na uongozi wake katika ziara yake ya siku moja mjini Harare.
 
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, tayari amekuwa na mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Bwana Robert Mugabe.
Hata hivyo mazungumzo hayo yamemalizika pasipokutolewa kwa taarifa yoyote juu ya nini walichokijadili katika mazungumzo hayo.
Wakati huo huo mabalozi wa nchi za kigeni wamewatembelea waathirika walioshambuliwa na wapiganaji wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa rais Mugabe.
Rais Mbeki amekuwa na mazungumzo mazito na rais Robert Mugabe juu ya hali ya mgogoro katika Uchaguzi wa mwezi machi.
Mbeki ambaye ni mpatanishi mkubwa, baada ya kuwasili mjini Harare alikwenda moja kwa moja kwa ajili ya mazungumzo na rais Mugabe ikiwa ni ziara yake kwanza nchini humo tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais.
Mazungumzo hayo ambayo yamefanyika katika Ikulu ya nchi hiyo yamechukua muda wa masaa matatu kabla ya Mbeki hajaelekea kwenye ubalozi wa Afrika Kusini mjini harare pasipo kutoa taarifa yoyote kwa waandishi wa habari juu ya mazungumzo yao.
Chama cha Upinzani cha MDC, ambacho kilishinda uwakilishi mwingi Bungeni na ambacho kiongozi wake alimshinda rais Mugabe katika awamu ya kwanza ya Uchaguzi Machi 29,kilitaka Bw Mbeki avuliwe wadhifa wake kama mpatanishi wa mgogoro huo kutokana na kushindwa kumwambia ukweli rais Mugabe.Juhudi hizi mpya za upatanishi zinakuja huku kukiwa na madai ya kuendelea kwa ghasia nchini humo ambazo zinalaumiwa kufanywa na magenge ya mgambo yanayounga mkono serikali ya Mugabe.
Kiongozi wa chama Kikuu cha upinzani cha Movement for Democratic Change -MDC, Morgan Tsvangirai amabaye Rais Mbeki nimpatanishi wake na Rais Mugabe, amesema hajakaribishwa katika mazungumzo yeyote na Rais huyo wa Afrika Kusini.
Msemaji wa chama hicho, George Simbotshiwe, amesema wanatambua kuwa kiongozi huyo yuko Zimabwe na anakutana na Rais Mugabe lakini kama Chama hawana mawasiliano yoyote ya kiofisi kuwa atakutana na chama cha MDC au kiongozi wake.
Bwana Tsvangirai, amekuwa nje ya Zimababwe kwa kipindi cha wiki kadhaa sasa, akikutana na viongozi wa Afrika na mabalozi ikiwa ni juhudi za kutaka kuongezwa nguvu ya kumshawishi Rais Robert Mugabe kuachia madaraka baada ya miaka ishirini na nane kumalizika akiwa madarakani.
Viongozi kutokaka mataifa kumi na nne wanachama wa SADC, mwezi uliopita walikutana mjini Lusaka Zambia,na walimtaka rais Mbeki aendelee na kazi yake ya upatanishi baina ya Chama Tawala cha ZANU-PF kinachoongozwa na rais Mugabe pamoja na chama cha MDC.
Rais Mbeki amekuwa akikata kumpinga rais Mugabe hadharani, mbali na kwamba nchi yake imejikuta ikiingia katika gharama mbalimbali za kiuchumi, huku kiasi cha raia wa Zimbabwe milioni tatu wakiaminika kuwa wanatafuta kazi nchini Afrika Kusini.


mbeki anajua ukweli ndo maana hamuungi mkono kibaraka MT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…