Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Bw. Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75, ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais. Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari wa Zimbabwe, Simon Kahaya Moyo.
Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa Rais Robert Mugabe, Bi Grece, atafuata nyayo za mumewe za kuwa Rais wa Zimbabwe.
Siku ya Jumapili Bi. Grece Mugabe alitoa wito wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa.
Bw. Mnangagwa, ambaye ni mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi, amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.
Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe, 93' kutishia kumuachisha kazi Bw. Mnangagwa hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo.