Zimbabwe: Rais Robert Mugabe amemfuta kazi Makamu wa Rais

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
00a02432c3890e329b4653950492af87.jpg
4a7dafeab3e474a8b5dc5a116f980a01.jpg
Rais Robert Mugabe amemfuta kazi Makamu wake wa Rais, Emmerson Mnangagwa kwa mujibu wa Wizara ya Habari nchini humo.

Bw. Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75, ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais. Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari wa Zimbabwe, Simon Kahaya Moyo.

Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa Rais Robert Mugabe, Bi Grece, atafuata nyayo za mumewe za kuwa Rais wa Zimbabwe.

Siku ya Jumapili Bi. Grece Mugabe alitoa wito wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa.

Bw. Mnangagwa, ambaye ni mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi, amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.

Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe, 93' kutishia kumuachisha kazi Bw. Mnangagwa hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo.
 
Naona Zimbabwe inakuwa nchi ya kifamilia, hapa lazima Grace ndiye aliyeshinikiza hili ili yeye awe makamu wa rais, halafu huyu Moyo si alikuwa hapikiki chungu kimoja na Mugabe? leo kawa waziri wa habari?
 
Wanaofuatilia Siasa za Zimbabwe inasemekana huyu ndo alikua akitabiriwa kuwa mrithi wa Mugabe endapo Mugabe akiachia ngazi na kuruhusu mtu mwingine kutoka ndani ya ZANU-PF kugombea uraisi,kufukuzwa kwake leo kunatoa mwanya kwa Mama Mugabe ambaye anaonekana nae kukitaka kile kiti kwa muda mrefu.

mbali na hivyoo kutimuliwa kwake kwa kosa la uaminifu si la kushangaza maana alikua akishirikiana na upande wa upinzani katika mikakati mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kilimo cha kisasa jambo ambalo halikuleta picha nzuri kwa mhe. Rais wa Sasa Mugabe na kuhisi na ilikua wazi kuwa anajiwekea mazingira sawa kuweza ama kuleta ushawishi wa kukirithi kiti cha Mugabe huko mbeleni.

kutimuliwa kwake kuna ashiria nini labda??kufukuzwa kwake kunaweza kuleta vuguvugu ndani ya chama kwa wafuasi wake kuhamasisha mapinduzi ndani ya chama hiko kikongwe au mwanasiasa huyo nguli na mwenye wafuasi wakutosha anaweza kujiengua na kujiunga na upinzani na kuchagiza vuguvugu la kumuondoa Mugabe japo haitakua rahisi maana mugabe amejichimbia mizizi mirefu kama ya mbuyu ambayo kuitikisa inabidi mpaka upinzani ujipange sana.
 
_98636474_1cda66d2-5e3c-46f8-b690-6cb311a1ac5f.jpg
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionEmmerson Mnangagwa
Taarifa kutoka Harare zinasema kwamba, Makamu wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amefutwa kazi.

Bw. Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75, aameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais. Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari wa Zimbabwe Simon Kahaya Moyo.

Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Bi Grace, atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe

Siku ya Jumapili Bi Grace Mugabe alitoa wito wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa.

Bwana Mnangagwa, ambaye ni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi, amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.

Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe, 93, kutishia kumuachisha kazi Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo.
Akihutubia mkutano wa wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili, Bi Mugabe alisema:

"Nyoka ni lazima apiwe kwenye kichwa. Lazima tukabiliane na nyoka mwenyewe anayehusika na migawanyiko chamani. Tunaelekea kwenye mkutano tukiwa chama kimoja."

Bw Mugabe alimtaka Mnangagwa na wafuasi wake kumuonyesha uzalendo au afutwe kazi.

Chama cha Zanu-PF kinatarajiwa kuifanyia mabadiliko katiba yake wakati wa mkutano na kuweka nafasi mbili za makamu wa rais, nafasi moja ikiwa ni ya mwanamke.

Nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa na Bi Mugabe na kuongeza uwezekano wa kumrithi mume wake.
 
Sijaona kitu kipya hapo tofauti na siasa za Afrika!!
 
yaani anaweza kumtimua makamu wake kama mkurugenzi tu. Hiyo katiba ya huko ni shida.
 
nchi inaongozwa na grace kwa miaka sasa, akidai chochote mugabe anatii, mbele ya .......... kila goti litapigwa.
 
Back
Top Bottom