G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Siku chache zilizopita aliyekuwa kamishina mkuu wa TRA ndugu Philip Mpango alitoa 'projection' ya ukusanyaji wa mapato kwa mwezi December kuwa serikali kwa mwezi huo itakusanya jumla ya Tshs. trilioni 1. 3 kama mapato.
Rais Magufuli alimpongeza na hatimaye baadaye akamteua kuwa waziri wa fedha na uchumi. Sina shida na hayo yote!
Shida yangu ni moja, mbona serikali imepata mapato chini ya Tshs. trilioni 1 mwezi huo? (Bilioni 986 Tshs? ). Hizo nyingine zaidi ya Tshs bilioni 300 imekuwaje tena?
Makusanyo ya mapato mwezi uliopita ilikuwa ni pamoja na faini za magari yaliyofanya makosa ambapo kimsingi siyo tegemezi kwani kesho kosa linaweza lisiwepo na hivyo kodi hiyo haitakuwepo! Je serikali ina uhakika wa mapato kiasi gani kwa mwezi huu wa January?