Zile biashara za Forever na zingine kama hizo ziliishia wapi?

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Wakuu Salamu.

Enzi nipo chuo niliwahi kuhudhuria semina moja kuhusu Forever, eebwaaanee wale jamaa wana convincing power ya ajabu.

Yaani wanaku-convice hadi unaanza kujiona tajiri hapo hapo, mwingine atakwambia alikuwa manager wa benki akaacha kazi akaingia kwenye Networking Market na sasa anamiliki benz, majumba kule masaki na walivyo wajanja wanaenda Photoshop kutengeneza picha akiwa beach huko miami afu wanawaonesha wakisema eti hapo ni 'wakiwa mapumzikoni'

Cha ajabu wale waliokuwa mentor wa hizo mambo hadi leo nawaona huku mitaani wakipiga mishe zingine. Nothing changed kwenye maisha yao. Wengine wameacha kabisa.

Hivi hizi biashara huwa ni za kweli au ni ujanja ujanja tu wa baadhi ya watu kuwatumia vijana wa vyuo kupiga pesa?

Sasa hivi naona imekuja hii ya BF SUMA, inatibu matatizo ya uzazi na yenyewe ni wale wale au wapo serious?
 
Kwa kweli hizi kamansio muongeaji utasota sana ila wanavyokuambia mwanzo yani wanushawishi wahali ya juu ila hakuna kitu
 
Ule ulikuwa utapeli tu wa kawaida.
Products zilikuwa ghali sana na watu waligeuzwa kuwa ma salesmen/women kuanya kazi bure bure kabisa bila kujielewa.
 
Forever ndo wakati wa kupiga hela Sasa. Watu wanahitaji Kinga ya mwili kuliko wakati wowote ule
 
Back
Top Bottom