Zikiwa zimebaki siku tano, Home Shopping Centre yasitishwa uwepo wake

Na zile Filling Station zilizopigwa mnada ARUSHA vipi?? Biashara gani hiyo wanataka kufungua?? Nje ya nchi au ndani?? teh teh teh... Wenzako wameshaongea na Kalonzo Musyoka awaletee Helikopta 3 mpya ziwatoroshee South Africa kisha AUSTRALIA.. Wewe utabaki ukisaga meno hapo Mkuranga na Ufuta wako shambani..

Mnaweseseka. Mara wamekimbia mara wao ndiyo waiba kura, mara hiki mara kile.

Mtaisoma namba. CCM tumejipanga!
 
Hii kampuni wafanyakzi wa TRA waliiogopa kama shetani, kwaniukileta za kuleta kuikomalia 'wakuu' wanapiga kwa kamishna unatajwa kwa jina na wanaaamuru pia ufanyiwe nini au uhamishiwe wapi! wapo huku ndani watupe yoote sasa kwani utawala wao umefika ukingoni.
 
Dah inauma sana,, ila hakuna namna maana ukiangalia hawa nao ndio walewale marafiki zao,,, act na chauma ndio wachanga bado masikini, shida ya lowassa naye hawa ni marafiki zake tena kibiashara,, aaah ngoja tumpe magufuri tu maana yeye hana urafiki na hawa ndugu!!! ukawa tulikosea wenyewe,,,
 
Unachekesha kweli ndugu, kamwe unajisumbua ukikaa ukawa na hisia kwamba UKAWA wataingia madarakani.

Kwa timu ipi hasa walionayo ambao ina uwezo wa kuongoza nchi?. Hawa kama wanakimbia na kama walikua wanakwepa kodi, basi ni lazima watakua wameshaona anaeingia ikulu ni yule ambae ana nia ya dhati ya kutokomeza mafisadi nchini, na ambae ni.......

Ambae ni.......L.O.W.A.S.S.A
 
Ninaomba kuelemishwa ni kwa nini home Shopping Center ametangaza kufilisika?. Alikuwa anafanya biashara gani?, Nani swahiba wake katika biashara zake?, Kama alikwepa kodi kwa nini asikamatwe na huku TRA wapo?.
 
Ninaomba kuelemishwa ni kwa nini home Shopping Center ametangaza kufilisika?. Alikuwa anafanya biashara gani?, Nani swahiba wake katika biashara zake?, Kama alikwepa kodi kwa nini asikamatwe na huku TRA wapo?.

Hivi ametangaza kufilisika au ametangaza kufunga biashara zake?
 
Kampuni ya Home Shopping Center Limited (HSC) inayomiliki maduka maarufu ya vifaa vya nyumbani kama mazulia, shuka na mapazia imefunga shughuli zake na kuwa katika mchakato wa ufilisi chini ya Yusufu Mohamed wa kampuni ya Law Domain Advocates ya jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Mohamed kupitia gazeti la serikali la Daily News jana, kampuni hiyo imeingia mchakato wa ufilisi wa hiari kwa kuzingatia Sheria ya Kampuni, Sura 212 ya mwaka 2002 kufuatia kile kinachoelezwa kuwa ni kutokana na uamuzi uliofikiwa Oktoba 5 mwaka huu.

Kadhalika, umma umefahamishwa zaidi kupitia taarifa hiyo fupi kuwa, yeyote mwenye kuidai Home Shopping Centre anapaswa kuwasilisha madai yake kupitia anuani ya mfilisi ndani ya siku 14 kuanzia siku ya kutolewa kwa notisi Oktoba 15, 2015.

Kwa mujibu wa tovuti inayoihusisha kampuni hiyo, inaelezwa kuwa ilianzishwa mwaka 1996 na ilianza shughuli zake kwa kuuza mazulia na shuka kabla ya kupanuka na mwishowe kusambaza bidhaa zake hadi katika nchi nyingine za Afrika zikiwamo za Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Burundi, Rwanda na Kenya.

Chanzo kimoja kimeiambia Nipashe kuwa, kufilisika ghafla kwa kampuni ya Home Shopping Centre katika kipindi hiki cha siku chache kabla ya uchaguzi mkuu na kuingia madarakani kwa serikali mpya kunaweza kuibua maswali mengi kutoka kwa baadhi ya watu, hasa kutokana na tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikiibuliwa dhidi ya kampuni hiyo kwa kuihusisha na baadhi ya vigogo.

Hata hivyo, Nipashe haikuweza kuthibitisha ukweli wa madai mbalimbali yanayoelekezwa kwa kampuni hiyo yenye maduka yake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, yakiwamo ya Msimbazi, Mtaa wa Uhuru, Masaki na Mlimani City.


KAMPUNI KUSITISHWA
Akizungumza na Nipashe jana, wakili mmoja wa kujitegemea alisema hakuna madhara makubwa pindi mmiliki anapoamua kuiweka mufilisi kampuni yake kwani ni uamuzi wa kawaida uliowekewa utaratibu kisheria.

KUMWAGIWA TINDIKALI
Mwaka 2013, mmoja wa wamiliki wa HSC, Said Mohamed Saad, alimwagiwa tindikali eneo la Msasani, jijini Dar es Salaam na watu wasiojulikana. Baada ya tukio hilo, Saad alipelekwa Afrika Kusini kutibiwa.

CHANZO: NIPASHE
 
Baada ya kutafuna rasilimali za watanzania kwa ufisadi uliotukuka chini ya mbawa za Rais kikwete na familia yake, Ghalib S Mohamed Mwenyekiti wa kampuni ya Alosco inayomiliki makampuni mengine zaidi ya kumi ikiwemo Supermarket za Home Shopping Centre, sasa ndio ataongoza kamati ya ufundi ya wizi wa kura kuanzia tar 24 oktoba.

Ghalib akiwa pamoja na Faroukh Bagonza wa kampuni za mafuta ya TSN na Supermarket za TSN wame ratibu wizi wa kura kwa kuagiza masanduku yaliyo jaa makaratasi ya kupigia kura kutoka Msumbiji na vifaa vingine haramu vya kupigia kura ambavyo vimehifadhiwa kwenye Godauni (maghala) ya Faroukh Mtaa wa Gerezani, Mnazi moja.

Ghalib na Faroukh wakishirikiana na jangili mwenzao Abdulrahman Kinana wiki iliyopita wamenunua magari manne kutoka kampuni ya Toyota Tanzania Ltd iliyopo barabara ya Pugu. Magari hayo yatatumika kusafirisha makaratasi ya kura batili na kutumika kama magari feki ya wasimamizi wa kimataifa wa SADC. Mpango ni kupeleka gari mbili Zanzibar na mbili zitakuwa Tanzania Bara. Gari hizo aina ya Toyota Landcruiser Hardtop (2) zenye namba za usajili T 471 DFC na T 469 DFC zenye chasis namba TEEB71 – 90 - 7026583 na TEEB71 – 00 – 7026617. Pia wamenunua Toyota Hilux Double Cabin (2) zenye namba za usajili T 468 DFC na T 470 DFC zenye chasis namba AHTFR22G10 – 6105538 na AHTDR22G00 – 6105546.

Ghalib S Mohamed, fisadi na jangili ambae tangu rais Jakaya Kikwete aliposhika hatamu mwaka 2005, alipewa fursa za kufanya biashara bila kulipia ushuru bidhaa alizokuwa akiingiza nchini kwa ubia na familia ya Rais Jakaya Kikwete. Leo hii kupitia mianya hii ya kifisadi na unyonyaji wa jasho la watanzania, Ghalib ni moja kati ya matajiri wa kubwa Tanzania anae miliki Mali nyingi za kifahari, Majengo, Magari na biashara nyingi za nyuma ya pazia.

Ghalib ana miliki jumba lenye gharama ya bilioni 13 za kitanzania iliyo jengwa kwenye eneo la heka 11 huko Kinyerezi. Eneo hilo ambalo lilimefanya familia zaidi 33 kuhamishwa bila kibali maalum kwa ajili ya ujenzi wa jumba moja la mtu mmoja.

Ghalib huyu huyu ana miliki nyumba 4 Masaki na sasa ana malizia jumba lingine la kifahari mtaa wa Lincoln Masaki ambalo lina jengwa na wakandarasi kutoka china.

Ghalib ana miliki magari tofauti ya kifahari ikiwemo Rolls Royce, Bentley, Ferrari magari kadhaa aina ya Range Rover yenye thamani zaidi ya billioni 3 za kitanzania.

Kazi kubwa ya kifisadi ni ile ya usafirishaji bidhaa bila kulipa ushuru kupitia kampuni yake ya usafirishaji ya Silent Ocean inayosimamiwa na mdogo wake anaye itwa Salaah ambayo makao makuu yake yapo China. Salaah ambae kwa sasa amefanywa balozi mdogo wa Tanzania nchini China bila kuzingatia hiztoria yake ya uhalifu wa kutumia silaha na kutishia kuuwa watu kwenye kumbi tofauti za starehe, zaidi ya hapo salaah hana elimu wala historia ya kidiplomasia lakini uswahiba wa familia yao na JK umempa nafasi hii kubwa kabisa katika Taifa letu.

Leo hii Ghalib ndio nguzo kuu ya ufadhili wa CCM na familia za viongozi wa CCM. Kwa Lugha nyepesi, ghalib ndio anafanya mipango yote na mikakati ya CCM na Serikali iliyopo madarakani. Mkakati mkubwa alionao sasa ni huu wa kuartibu wizi wa kura ambao Ghalib na maswahiba wake wamemwaga pesa nyingi sana ili kufanikisha wizi mkubwa wa kura katika historia ya Taif hili wakijua dhahiri Magufuli hana asilimia 30 ya kura za Watanzania.
 
Duuuu hii sasa hatari. Kumbe ndo maana Mkulu alisema lazima tutashinda na yule mwingine akasema hata kwa goli la mkono, sasa ndo naelewa maana ya zile kauli
 
Ninaomba kuelemishwa ni kwa nini home Shopping Center ametangaza kufilisika?. Alikuwa anafanya biashara gani?, Nani swahiba wake katika biashara zake?, Kama alikwepa kodi kwa nini asikamatwe na huku TRA wapo?.
Namna yako ya kuuliza maswali ni kama vile majibu unayo kwahiyo unataka kuona watu wanasemaje, wewe kuwa wazi tu weka na majibu na sisi tutachangia. Wakikuweka ndani mara baada ya uchaguzi tutakutoa.
 
Sasa ni wazi hali imeanza kuwa tete kwa wafanyabiashara washirika wa vigogo wa serikali na watoto wao... Kampuni ya Home Shopping Centre washaanza kufungasha virago na kukimbia kusikojulikana.

Ikumbukwe kampuni hiyo imekuwa ikihusishwa na moja wa mke wa kigogo hapa nchini, pamoja na mtoto wa kigogo hapa nchi.(Mama na Mtoto).... Home Shopping centre wamekuwa wakishutumiwa zaidi kwenye sakala la ukwepaji kodi, ambapo kwa siku inakadiriwa walikuwa wanakwepa zaidi ya billioni 12 kwa bidhaa wanazoingiza nchini...

Kwa wale wadau wa Kariakoo watakuwa wanakumbuka sakata la hawa majamaa vizuri sana....

Myatake: Serikali ya Ukawa isinyamazie hili jambo. Lazima wawajibishwe kwa ukwepaji kodi hata kama wakisepa....
View attachment 300445

Nadhani wakati mwingine tunaweza pambana na hizi system za kijinga watu kama hawa ni kuamasishana hakuna kununua bidhaa kwao then wanakufa na kuondoka. hii ndio dawa ya kudeal na system mbovu. wenzetu nje wameweza kuwaondosha watu kama hawa kwenye society zao. its better to list all business companies with no doubts na tunapanga not to do business with them. wengine wataogopa kuja na ndio mwisho wa michezo michafu nchini
 
Back
Top Bottom