Zijuwe dalili za kabla ya kuachwa.

Umesema ukweli me mume wangu alikuwa hadi kuoga anaenda na simu ,sa ya kulala anailalia kwenye mto. Jioni kuanzia saa 1 hadi 4 anazima simu. Mwisho nililetewa kabinti ka form six kamefukuzwa kwao kana mtoto mchanga . Habari ikaishia hapo. Thanx kwa ujumbe mzuri.

Mkaachana au?
 
chentuntu pole sana lakini wengine hawaendi nazo popote lakini izo password hamna utaloona utaishia kuziona zinapiga mbizi humo ndani yaliyomo siri ya mwenyewe.


Umesema ukweli me mume wangu alikuwa hadi kuoga anaenda na simu ,sa ya kulala anailalia kwenye mto. Jioni kuanzia saa 1 hadi 4 anazima simu. Mwisho nililetewa kabinti ka form six kamefukuzwa kwao kana mtoto mchanga . Habari ikaishia hapo. Thanx kwa ujumbe mzuri.
 
Nadhani hizi ni dalili za mtu ambae ameshakupatia msaidizi/mtu wa kuchukua nafasi yako zaidi kuliko anaetaka kukuacha tu.Katika hali ya kawaida mtu anaetaka kukuacha kwa sababu nyingine tofauti na kupata anaemuona bora kuliko wewe hatakua na haja ya kuficha simu au kuikumbatia kama mtoto.Ila wa kuogopwa ni wale ambao leo mnacheka na kufurahi alafu kesho unaambiwa bye bye.Hii ndo hua inawafanya watu wachanganyikiwe maana bila dalili huwezi kujiandaa unakua hukutegemea!

Dada Lizzy mbona hapo zipo dalili za watu mchanganyiko ila tunazihitaji za ziada tuweze kujizatiti na balaa hili la kuachwa.
 
Mkwaruzo bana yamekukuta nini maana du umeongea kweli tupu.........................

japokuwa nimezisikia sehemu ila nami nimejaribu kuziweka zile zilizonikuta mm mwenyewe japo kuwa nilijua kuwa nipo hatarini lkn nitafanyaje coz tulikuwa far apart in location kwa kipindi hicho.
 
kawaida nikiona hizi dalili,mapema namaliza mahusiano hata kama nimependa kupita maelezo,bora nikalilie mbele ya safari kabla mahusiano hayajafika pabaya zaidi

hujawahi kupenda katika maisha yako, naomba one day ikutokee upende kama tulivyowahi wenzako then utaona ugumu wa kufanya maamuzi yako.
 
enzi hzo tukiwa skul, alianza kwa kutojb kadi zangu nilimtumia zaidi ya kadi 5 lakini akamute. mwishowe nikamkuta kafungiwa na mjeda kambini japo baadae aliachwa naye pia na sasa ananililia its too late.
 
Dalili ya mvua ni mawingu ingawaje baadhi ya wakati inaweza kunyesha bila ya hata kuonekana mawingu ya kuridhisha kama dalili yake. Na ni kama hivyo, kabla ya kuachwa huwa zipo dalili tofauti ambazo wengi wetu kwa kuona ni vitu vya kawaida, huwa hatuchukuwi tahadhari za mapema.
Baadhi ya dalili hizo ni hizi zifuatazo ila na wewe ongezea nyengine kwa kujuzana zaidi.

1. Mwenza kukosa raha mnapokuwa pamoja.
2. Kutopenda kutembelewa ikiwa mnakaa sehemu tofauti au kukutaka utowe taarifa kabla ya kumtembelea.
3. Kutoipa umuhimu mitoko yenu ya week end au mengineyo kama ilivyokuwa awali.
4. Kuanzisha majibu ya mkato.
5. Kukujibu kwa kujiamini zaidi.--muhimu kuonesha amekomaa
6. Kutozijibu text zako kwa wakati tofauti na ilivyokuwa awali.
7. Kupenda kuzima simu kwa muda mrefu bila ya sababu za msingi na kutoyajali mawasiliano.--hapa ni kweli anaweza kukuacha
8. Kwenda pembeni kupokea call iliyoingia au kwenda kujibu text. huku ni kucheat
9. Kuchukizwa na kuishika simu yake. -- ni kutojiamini
10. Kutojiamini mnapokuwa pamoja. -- hapa atakuwa anacheat..
Hivyo zinapojitokeza ishara kama hizo ni vyema kuuimarisha upya uhusiano wako kabla hayajakukuta.

Ingawa huku-specify kwamba dalili za kuachana kwa wachumba au wanandoa???
Lakini ni point zuri hasa hapo kwenye red
 
Aksante mwayego angalau utatusaidia kupunguza maumivu.....ila nadhani kuna wengine wanaamua tu ghafla bila warning wala nini..nakumbuka nyamayao alisema wake alimwacha ghafla bin vuuu..........tena jana yake tu alitolewa out kwa vicheko na bashasha....wakarudi na kuagana kwa mabusu moto moto kwa ahadi ya kuwasiliana kesho yake (mh hapa pa mabusu nimeongezea) halafu keshoye ghaaaah simu hazipokelewi, sms hazijibiwi kabla ya kulibwaga its over!!

Sasa sijui ni kushindwa kusoma alama za nyakati au kuna wanaoendesha hisia zai kwa reflex actions/thoughts.

umenisaidia my dearest, hii ya kwangu haikuwa ishu ya kusoma alama za nyakati wala nn, hatukuwa na ukorofi/mgongano wowote kwa wakati huo, yeye ndie alienical tukapate dinner tena na mabusu motomoto kama ulivyosema, nimerudishwa home kwa kumbatio tamu la mahaba, nimelala nikitabasamu....kweli ya kesho anayajua Mungu.
 
ya nyama yao ndiyo kama hayo ya mvua bila ya mawingu ila hayo siyo sana kutokea.

the guy was smart...nilikuja kugundua alikuwa ana uhusiano na wengine wawili,baada ya 2kio sasa frnds ndio wananipa michapo, cjui alikuwa anajipanga vipi coz mie nilikuwa nikimhitaji nampata bila wacwac, ckuona ishara yoyote, kwake nina fungua, weekend ni mama wa nyumba, ckuwahi kuona mashaka kuanzia cm/kwake wala chochote...baada ya muda mnakutana town kakombatia karembo...lile lijamaa liliniumizaga roho sana aisee but limenisaidia kunikaribisha kwenye ulimwengu wa kuvunjwa vunjwa moyo.
 
Umesema ukweli me mume wangu alikuwa hadi kuoga anaenda na simu ,sa ya kulala anailalia kwenye mto. Jioni kuanzia saa 1 hadi 4 anazima simu. Mwisho nililetewa kabinti ka form six kamefukuzwa kwao kana mtoto mchanga . Habari ikaishia hapo. Thanx kwa ujumbe mzuri.

jamani ndoa zina mambo jamani...khaa hii taasisi inatesa bwana.
 
Umesema ukweli me mume wangu alikuwa hadi kuoga anaenda na simu ,sa ya kulala anailalia kwenye mto. Jioni kuanzia saa 1 hadi 4 anazima simu. Mwisho nililetewa kabinti ka form six kamefukuzwa kwao kana mtoto mchanga . Habari ikaishia hapo. Thanx kwa ujumbe mzuri.
Pole chetuntu hyo ni mitihani ktk maisha.
 
Back
Top Bottom