Zijue sheria za Nchi ya Saudia Arabia

Karot

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
1,159
1,309
Habari za majukumu wakubwa na wadogo... Naomba leo tujuzane baadhi ya sheria za Nchi hiyo ikiwa kuna mtu anajua zaidi aongezee ili tupate kuzifaham zaidi. Na pia naruhusu kukosolewa ikiwa kuna sehemu nimekwanga.

Mimi naanza na hizi...

1. Kazi ndogo ndogo zote mfano kujenga, kufagia, kubeba maboksi wanafanya Wahindi, Wabangaladesh na Wanepal.

2. Maofisi makubwa yote wanakaa wenyewe wa Saudia.

3. Mgeni ikiwa kaenda kwa ajili ya kusoma haruhusiwi kufanya kazi yoyote tofauti na shule, ikitokea kuna kampun imekuajiri au mtu binafsi anashitakiwa.

4. Kwa mgeni ikiwa umekwenda kwa ajili ya kufanya kazi unatakiwa kila mwezi ulipie kodi, ikikushinda unarudishwa kwenu.

5. Si mara nyingi kuona askari wa barabarani wanasimamisha vyombo vya moto.

6. Kesi nyingi zitokanazo na makosa ya barabarani haupelekwi mahakamani kule ni faini kwenda mbele.

7. Asilimia kubwa ya mapato yanatokana na makosa ya barabarani, ikiwa hujafunga mkanda unapigwa picha na kamera za barabara, ikiwa umemweka mtoto mbele ya seat, ukiwa na taa mbovu nakadhalika faini ni hiyo hiyo.

8. Unatakiwa utembee na kitambulisho mda wote, polisi wakikushika hauna unatozwa faini.

9. Ikiwa umeajiriwa na kampuni na umepewa gari uendeshe, makosa yote ya barabarani wanalipia wao. Mwisho wa mwezi wanakukata kwenye mshahara wako.
 
***mkitembea barabarani na mwanamke mmeshikana mkono sio mkeo mnachapwa viboko.
***mwanamke haruhusiwi kuendesha gari.
***wanawake hawapigi kura.
***wanaume ndio wanafanya shopping g
 
Back
Top Bottom