Zijue sababu zilizoiwezesha China kukua kwa kasi kiuchumi, tujifunze

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
KUPITIA HADIDU ZA REJEA HIZO HAPO CHINI TANZANIA TUNAWEZA KUJIFUNZA KITU KUTOKA UCHINA.

Ukuaji wa kiuchumi wa China kwa sehemu kubwa umechangiwa na kuhama kutoka uzalishaji wa kilimo kwenda uchumi wa viwanda yaani mapinduzi ya viwanda.

China ilijiunga na Shirika la Biashara la Kimataifa WTO mwaka 2001. Bidhaa nyingi zinazouzwa na kununuliwa Uingereza, Afrika, Asia na Marekani hutengenezwa China. Baada ya mapinduzi ya viwanda China ilijiunga WTO ili iwe rahisi kufanya biashara.

Hivyo Tanzania itumie fursa ya kuwa SADC, EAC, AU nk kufungua fursa za biashara kwa kuwawezesha raia wake kuwekeza kwenye nchi hizo kibiashara ikiwa ni pamoja na kuwauzia bidhaa za Tanzania.

Bakhresa ameweka mfano wengine wawezeshwe na kuhamasishwa kufanya biashara na nchi nyingine za Afrika hasa zinazotuzunguka.

Ukuaji wa sekta ya viwanda China unazo sababu lukuki, zikiwemo hizi zifuatazo:
1. China imetengeneza fursa mwanana sana kwa watu wake kufanya biashara hususani katika hatua ya kuanzisha biashara.

Yaani serikali haiwakwazi wananchi wake wanapotaka kuanzisha biashara.

Serikali inahakikisha miundombinu wezeshi inakuwepo na mazingira ya kodi yanakuwa rafiki.

2. Motisha inatolewa kwa wawekezaji wa ndani na wa kigeni. China imeanzisha Special Economic Zones (SEZ) ambazo zinatoa motisha za kodi kwa biashara za nje.

Shenzen ni SEZ inayofahamika zaidi.

3. China inacho kiwango cha juu kabisa cha watu wenye ujuzi na maarifa highly-skilled labour ambao wameifaa china ktk ukuzaji sekta ya viwanda.

Hata mataifa makubwa kama Marekani yamekuwa yakitegemea skilled labor ya uchina kutekeleza mambo yao.

Wakati fulani China iliwekeza kuwasomesha watu wake teknolojia kwenye mataifa ya nje yaliyoendelea ambao walirejea nyumbani na kupasisha ujuzi hatimaye kuambukiza ujuzi kwa vizazi na sasa China inakimbia.

Tanzania tulishawahi kuwa na utaratibu huo watu wetu walienda nje ya nchi kv USSR lakini sijui tulikwama wapi.

Tujitathmini upya tuwajengee uwezo vijana wetu kiteknolojia waende nje na wasome ndani ili tukuze uchumi.

Kilimo pekee hakitatutoa, viwanda viwanda viwanda. Na tuna advantage ya masoko.

4. China imewekeza katika soko la ndani zaidi. Wanauza ndani zaidi mali inayozalishwa ndani zaidi. Pesa inabaki ndani zaidi.

Tanzania nashauri tuanzie kwenye nguo. Tununue nguo za Tanzania baada ya kuviwezesha viwanda vya ndani na kukuza kilimo cha pamba.

Sekta ya Textiles itatutoa kwa haraka sana. Hii nchi ina watu wengi sana wanaohitaji nguo na vitambaa kila uchao.

Baada ya msosi ni vitambaa. Tuwekeze kwenye kilimo cha pamba na tuhamasishe viwanda vya nguo kisha soko la nguo za nje tupandishe kodi iwe juu. has a growing domestic market for goods because of its large population.

5. China ina sifa ya kuwa na maadili ya hali ya juu ya ufanyaji kazi. Mchina hachezi na kazi. Akifika kufanya kazi ni kazi kweli kweli. Hana ubabaishaji.

Huu ni utamaduni tunaweza kuujenga. Ikiwa ni pamoja na kuongeza masaa ya kazi kwenye utumishi wa umma na private sekta.

Kupunguza sikukuu zisizo lazima. Watu wapige kazi. Na mjini kama mtu hana kazi yenye anuani, yaani yupoyupo tu arudishwe kijijini akalime au achukuliwe kupewa shamba alime.

Na mwenye ujuzi apewe mtaji.

6. Usalama na Afya mahala pa kazi sio kipaumbele hivyo makampuni hayalazimiki kutumia bajeti kubwa sana kuwekeza kwenye eneo la usalama.

Mfanyakazi anaambiwa ajilinde mwenyewe na bima itafanya kazi yake akizembea akapata ajali.

7. China haijaweka kiwango cha juu sana cha udhibiti kwenye uzalishaji. Tofauti na huku Afrika.
 
Mi nimependa Sana kwenye kipengele Cha kazi ulipoeleza Kama mtu yupo tu Hana kazi ajaribu hata kuangaria fursa kijijini kwa ajili ya kilimo.niongeze kwa kusema vijana wetu wa Tanzania sio wavivu endapo serikali atawaunga mkono,Hakuna mtu ambaye anapenda kukaa kijiweni bila kazi.Ni vema serikali angetenga mapori na vijana wangepewa maeneo kwa ajiri ya shughuri za kilimo sidhani Kama wangekataa.Vijana watanzania wanapenda kilimo tatizo ardhi, watengewe hata maeneo na wapewe Kila mtu plot yake na sheria imlinde.Kila mkoa serikali itenge mapori ili vijana ambao hawana kazi wapate maeneo ya kuanzisha mashamba.nchi Kama Indonesia,Sir Lanka,Vietnam,Thailand,Malesia na China wamewekeza kwenye kilimo,biashara na viwanda.malighafi za viwandani mfano katani,pamba,michikichi,hupatikana kwenye kilimo hizi sector ya kilimo, biashara na viwanda zinategemeana.

Sent from my itel A32F using JamiiForums mobile app
 
Nimependa sana ulivyowazungumzia wachina katika kazi. Nilishawahi fanya kazi na kampuni moja ya wachina uko iringa mafinga, majama wanafanya sana kazi ukiacha mapungufu mengine waliyonayo ya kibinadamu ni wachapa kazi mno na wanaheshimu sana muda katika Nazi. Nimejifunza mengi kutoka kwa hawa jamaa watanzania kweli tuige mfano wa wachina katika kazi.
 
Tatizo ni ubinafsi na siasa kamwe hatuwezi mpaka tutakapo badili mtizamo hasa wa kisiasa ubaguzi ni mkubwa lakin ardhi tunayo na tunaweza kutoka.. refer yaliyowakuta mtwara, so shida ni siasa tuuu.
 
Back
Top Bottom