Zijue namba hizi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zijue namba hizi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Giro, Mar 17, 2009.

 1. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Theopista Nsanzugwanko
  Daily News; Monday,March 16, 2009 @18:50

  Polisi leo inaanza operesheni maalumu ya kukagua na kukamata daladala, kubaini watakaotoza nauli kinyume na utaratibu ili wachukuliwe hatua za kisheria. Operesheni hiyo ya wiki mbili, inaendeshwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Kanda ya Mashariki na Pwani.

  Katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam, Mohamed Mpinga, alisema miongoni mwa adhabu zitakazotolewa kwa watakaobainika, ni pamoja na kunyang'anya leseni za biashara kwa siku 15.

  Mpinga alisema kutoza nauli kubwa au kujaribu kufanya mgomo baridi kwa baadhi ya wamiliki wa daladala kwa kisingizio cha kushuka nauli, ni kinyume na sheria ya leseni zao. Kutokana na kuwapo taarifa za baadhi ya madereva na makondakta kukaidi kutoza nauli mpya, Mpinga alitoa namba za simu yake ya mkononi akiwataka wananchi kuwasiliana naye kutoa taarifa ya gari linalohusika.

  Namba hizo ni 0754 360046 na 0713 635799. Vilevile alitoa namba za wakuu wa Usalama Barabarani katika Mikoa ya Kipolisi ambazo ni Ilala 0784 304158, Kinondoni 0755624243 na Temeke 0713 260888.

  Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA, Kanda ya Mashariki na Pwani, Walukani Luhamba, alisema wameamua kunyang'anya leseni kwa watakaokutwa na makosa hayo kutokana na uzoefu uliopo kwamba wakitozwa faini, huendelea kutenda makosa.

  Alisema Sumatra imekuwa ikifanya ukaguzi mara kwa mara tangu kushuka kwa nauli na kukamata baadhi ya mabasi ambayo wamiliki walilipa faini kwa kuwatoza abiria nauli kubwa lakini sasa watawanyang'anya leseni. Alisisitiza kupelekwa kwa mabasi hayo katika Chuo cha Ufundi VETA kuandikiwa nauli mpya ubavuni, akisema mabasi machache ndiyo yalitekeleza hilo. Hivi karibuni, Sumatra ilishusha nauli za mabasi ya mikoani na daladala. Kwa upande wa Dar es Salaam, ilishusha nauli ya daladala kwa asilimia 12 ambayo ni sawa na Sh 50.
  ...................................
  Ila kwa tabia ya wadanganyika watakubali vitisho vya makonda hata kama ni haki yao.
   
 2. j

  jaffery hassan Member

  #2
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 9, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mi naona suala la kushusha nauli kwa hizo asilimia12,isiwe ni kanda ya mashariki tu kwani sisi wa mikoani hasa kanda ya kaskazini madereva na makonda wao ni ubabe tu nasi pia tunataka hiyo operation huku mikoani.
   
 3. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naona watu wanatengenezeana hela za Vitoweo. Iko wapi issue ya kuhakikisha Level Seat ndani ya mabasi ilivuma ikaisha bila ya kujua, iko wapi issue ya kuvunja utaratibu wa foleni kwa maana zile daladala ambazo zilikuwa zinapita kando kando ya foleni, hakuna kitu. Watu wapo wapo tuuu peleche peleche nyingi lakini wajibu ni wakuvuma
   
 4. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Suala la kushusha ama kupandisha nauli linatakiwa litumike nchi nzima,kweli mtu wangu hata mimi nashangaa kuwa eti operation inakuwa ya ukanda wa mashariki na pwani huko kwingine ni nje ya Tanzania?!Au ndiyo ubabaishaji tu na kufanya kazi kama zimamoto!!
   
 5. A

  Audax JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hii kweli maana mkoani watu tunaumia saana,ina maana hatuna haki ya kushushiwa nauli? au serikali inaona mkoa mmoja tu? ndiyo maana hamtaki kuamia dodoma nini!! kila kitu ni dar tu!!!!!!!!!!!! misaada yoote dar,events zote dar!!! tukumbukne jamani!!
   
 6. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni nguvu ya soda, utapiga simu kuharibu vi dola vyako eti unawashitaki washika dau wao.

  Nafikir hii ni tishia toto, we are no longer kids kudanganya kila siku hapa.
   
 7. D

  Darling Member

  #7
  Mar 17, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  MI NAONA ISSUE YA KUKAA LEVEL SEAT NI YA ABIRIA WENYEWe. NAKUMBUKA KIBAHA TULIKUWA TUNAWEKWA WATANO KWENYE SEAT BUT ABIRIA TULIKUWA NA MSIMAMO; NOW NI LEVEL SEAT. ABIRIA TUNAJUA KUWA TUKIFIKA WANNE UNAANZA MSTARI MWENGINE SO TUSILAUMU WATUNGA SHERIA..WAKATI MWENGINE TUJISAIDIE WENYEWE JAMANI HAWA MAKONDA WANACHOJALI NI PESA NAWEWE KAMA UNAHARAKA ZAKO BASI UTAPANGWA KAMA DUMU ZA MAJI KWENYE BUTI....

  WASSALAAM
   
Loading...