Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
FEBRUARI 24, 2016 Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and Power Tanzania Limited ilitangaza ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika Bonde la Mto Ruvu yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 2.17.
Ugunduzi huo mpya umefanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.
Katika ugunduzi huo mpya kwenye kisima cha Mabambakofi-1, kiasi cha gesi yenye ujazo wa futi trilioni 2.01 kiligundulika ambapo awali kampuni hiyo ilikuwa imegundua kiasi cha futiza ujazo trilioni 0.16 kwenye eneo hilo.
Kwa habari zaidi, soma hapa => Zijue kampuni zilizowekeza katika mafuta na gesi Tanzania (14) – Dodsal Resources Limited | Fikra Pevu