Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Balozi Isaya Bakari Chialo
NDOVU Resources (Aminex) Tanzania Limited ni kampuni tanzu ya Aminex PLC ya Ireland ambayo inamiliki leseni tatu za utafiti na uzalishaji wa gesi nchini Tanzania.
Aminex PLC ina makao yake makuu jijini Dublin, Ireland ambako imesajiliwa kwa hati namba 72399, ikiwa inajihusisha na uzalishaji wa mafuta na gesi hasa katika nchi za Afrika ambapo imesajiliwa katika masoko ya hisa ya London SE na Irish SE.
Bodi ya Wakurugenzi ya Aminex PLC inaongozwa na Brian Hall ambaye ni Mwenyekiti na wajumbe wake ni Jay Bhattacherjee (Ofisa Mtendaji Mkuu), Philip Thompson (Ofisa Uendeshaji Mkuu), Max Williams (Mkurugenzi wa Fedha na Katibu wa Kampuni), Andrew Hay (Mkurugenzi), Keith Phair (Mkurugenzi) na Tom Mackay (Mkurugenzi).
Balozi Isaya Bakari Chialo ndiye Mkurugenzi Mkazi wa Ndovu Resources (Aminex) Tanzania Limited wakati Thierry Murcia ni Meneja Mkazi nchini Tanzania.
Kwa habari zaidi, soma hapa=> Zijue kampuni zilizowekeza katika mafuta na gesi Tanzania (13) – Ndovu Resources (Aminex) Limited | Fikra Pevu