Jitu la kienyeji
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,445
- 7,987
Leo tunaangalia faida za tunda aina ya tango, kwanza kabisa tango ni tunda ambalo watu wengi hawalipendelei kwa sababu ya radha yake lakini ni tunda ambalo lina faida kubwa na virutubisho vingi katika mwili wa binadamu. Tango lina wingi wa madini ya potassium, vitamin B n.k
zifuatazo ni faida za tunda tango:
1. Huupa mwili maji na kuondoa sumu mwilini
2. Husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani
3. Husaidia mmeng'enyo wa chakula kufanya kazi vizuri na kufanya choo chako kuwa kilaini
4. Lina virutubisho kama vile lariciresinol,pinoresinol na secoisalariciresinol ambazo husaidia kupunguza aina ya kansa, kama kansa ya matiti, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume
5. Hutibu mtu mwenye tatizo la moyo kwa sababu tango lina wingi wa potassium ambayo husaidia moyo kuwa katika mapigo sawa
6. Husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (low na high pressure)
7. Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis)
8. Pia husaidia kupunguza homa inapopanda.