Zijue aina za NYUKI na tabia zao

Zijue aina za NYUKI na tabia zao

kidadari na markbusega Hongereni kwa kuitendea haki JF..

Nimesoma sehemu fulani nikashindwa kuamini/kuwelewA, na copy kama ilivyo

Bees have two stomachs - one stomach for eating and the other special stomach is for storing nectar collected from flowers or water so that they can carry it back to their hive

Nachojua tumbo la kuhifadhia chakula kwa wadudu (crop) ndio nyuki hutumia hilo hilo kuhifadhia nectar anapokuwa field tofauti na wadudu wengine Ni kubwa na anamatezi (glands) mengi kwa hiyo tumbo lake lina majukumu mawili labda kama atakuwa anamaanisha utumbo mwembamba


kidadari na markbusega Hongereni kwa kuitendea haki JF..

Nimesoma sehemu fulani nikashindwa kuamini/kuwelewA, na copy kama ilivyo

Bees have two stomachs - one stomach for eating and the other special stomach is for storing nectar collected from flowers or water so that they can carry it back to their hive
 
Last edited by a moderator:
Preta sina uhakıka kama Ni kweli nyuki anaweza kudunga akiwa amekufa nachokifahamu Ni kwamba tendo la nyuki kusukuma sumu kutoka kwenye tezi ya sumu halitawaliwi na ubongo japokuwa hawaelezi bayana linadhibitiwa na nin, katokana sababu hiyo kile kitendo cha mshale wa nyuki kuingia tu tayari mfuko (tezi) wa sumu hujikamua na kumwaga sumu kwa haraka sana nadhani ndio maana hata kama amepoteza fahamu ukichomwa na mshale wake utahisi maumivu pengine labda hali hii ilichukuliwa kwa nyuki hudunga hata akiwa amekufa
 
Khaa!! Ahsante kidadari kwa hakika uumenipunguza ujinga wangu leo 😎
 
Upo vizuri jombaa
Naomba kujua tofauti ya asali wa.nyuki wadogo na nyuki wakubwa
Pia kwa nini wakati wa kulina asali ukiwa unafanya slow nyuki wanakula asali yao
 
Nyuki wanaouma hawa wako genus melifera na wasiouma wako genus trigona kama sikosei , ukiangalia jinsi nyuki wanavyotengeneza asali huhusisha umezaji wa nectar na kutapika wanapofika kwenye mzinga lakini pia nectar hiyo ikiwa tumboni /mdomoni huchanganyikana na content za matezi ya maziwa ya nyuki (royal jelly) kwa ajili ya malkia na watoto wa nyuki (majana)
Sasa tofauti ya content ya matezi ya hizi aina mbili hii Inaweza kuwa chanzo cha tofauti ya radha

Lakini jingine Ni hawa nyuki aina mbili kupendelea maua ya mimea tofauti
Kingine Ni kiwango cha uwiano wa sukari na maji n.k kuwa tofauti wakati wa kuivasha asali ambapo kiwango cha uwiano wa sukari wa nyuki wasiouma au wadogo kama ilivyozoeleka huwa chini ukilinganisha na wanaouma
 
hivi nyuki anang'ata au anakudunga na mwiba wake,naomba kufahamishwa...kama sijaelewa maelezo kwenye hilo..
 
Mshale wa nyuki uko nyuma Ni mwiba ambao una nafasi katikati sawa tu ilivyo sindano ya binadamu au mifugo kwa hiyo ni sahihi kutumia neno kuchomwa au kudungwa
 
mkuu kama utaweza kuweka tofauti ya asali ya nyuki wadogo na wakubwa nitashukuru sana

nilikuwa ushokola kaliua wilaya ya urambo juzi juzi ndio nimeona tofautiya asali ya nyuki wadogo na nyuki wakubwa, asali ya nyuki wadogo ina ladha ya ukali kama ndimu au limau kwa mbali, na asali ya nyuk wakubwa ni full utamu haina huo uchachu chachu
 
mkuu je ni kwl kuwa malkia anapotaka kujamiiana na midume basi huruka juu sana na kundi la nyuki madume humfata na akifika kiwango cha juu sana hujikuta kabaki na dume moja tuu ambalo humuingilia na hao wengine hurudia njiani kwa maana hushindwa kwenda juu zaidi kwa sababu ya hewa na upepo,je kuna ukwl hapa??
 
Stuna nikweli. Malkia akishakamilika hutoka kwenye chumba chake maalum cha malezi siku ya 16 toka yai litagwe baadaye atasubiri siku saba kukomaa kiuzazi akishatimiza muda huo lazima aondoke, anapoondoka hufuatwa na kundi la baadh ya nyuki vibarua na madume, nyuki dume wenye kasi ndio hufanikiwa kumrutubisha (survival for the fitest) ambao kwa wastani wanaweza kuwa kati ya 10 hadi 12 kila mmoja atadeposit mbegu za wastani wa mil 12 nakutunzwa kwenye mfuko maalum wa malkia ujulikanao kama spermatheca baada ya hapo malkia hushuka na kuanza kutaga mayai ndani ya saa 24 tayari kundi jipya la nyuki linakuwa limepatikana kwa njia hiyo
 
Back
Top Bottom