Zijue aina za nyoka: Wa kawaida, wa kichawi na wa kimizimu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,227
157,425
Nyoka ni kiumbe atambaaye kwa tumbo. Vitabu vya dini vinatuambia kuwa nyoka alilaaniwa. Vinamfananisha nyoka na yule shetani ibilisi mwenye mapembe.
Tukiachana na vitabu vya dini kuna aina tatu za nyoka. Kuna nyoka wa kawaida, Nyoka wa Kichawi na nyoka wa kimizimu.

1. NYOKA WA KAWAIDA
Hawa ni nyoka waliotokana na kuanguliwa mayai kutoka kwa mama zao. Nyoka hawa wamegawanyika kwenye makundi makuu mawili, wenye sumu na wasio na sumu.
Asilinia 95 ya nyoka hawana sumu iwezayo kumdhuru mwanadamu. Ni asilimia tano tu ya nyoka ndio wenye sumu.
Nyoka wa kawaida hawadhuru watoto.

2. NYOKA WA KICHAWI
Hawa ni nyoka waliotengenezwa kwa nguvu za kishirikina kwa ajili ya kuleta madhara fulani kwa atakayegongwa na nyoka huyu (mlengwa/ mkusudiwa)
Nyoka huyu anaweza kusababisha kifo, ufukara, umasikini, mikosi na majanga mbalimbali.
Nyoka wa kichawi anauwezo wa kukufuata popote ulipo, hata ukiwa ndani ya ndege angani, akakushambulia na akajificha asionekane hata kwa darubini.

3. NYOKA WA MIZIMU
Hawa ni nyoka ambao mara nyingi huwa na vichwa vingi na ni wakubwa kwa umbo.
Nyoka hawa hupatikana kwenye mapango ya matambiko, misitu ya kutambikia, kwenye mito mikubwa nk.
Mijoka hii isipofanyiwa ibada/ matambiko na kutolewa sadaka huleta madhara makubwa, mfano, mijoka hii inaweza kuleta mafuriko makubwa sana kipindi cha kiangazi, maporomoko ya ardhi na mawe etc.
 
Inawezekana jamaa anasema ukweli. Wakati tukiwa wadogo tulikuwa tunacheza mpira barabarani. Ghafla kakatokea kanyoka kadogo kakaanza kumkimbiza dogo mmoja mpaka kakamgonga. Dogo alianguka palepale akafa. Nilikuwa darasa la kwanza ila mpaka Leo lile tukio naliwaza. Maana hatukumwona nyoka alipotokea na baada ya tukio hatukujua kaenda wap afu tulikuwa watoto wengi ila alituacha wote na kumfukuza Ben
 
Mmmh hao nyoka wa kuzimu na uchawi wao hawakutoka kwenye mayai ya mama zao????
Hawa hutengenezwa. Mchawi anaweza kumtengeneza nyoka kwa kutumia kitu chochote, mfano, kisu, njiti ya kiberiti hata karatasi, kisha hunuiziwa maneno na kupewa maagizo ya nani wa kumdhuru, mahali mtu atakayedhurika alipo nk.
Nyoka wa kimizimu hawa ni binadamu waliokufa siku nyingi na wakajibadilisha maumbo ili waabudiwe
 
R
Inawezekana jamaa anasema ukweli. Wakati tukiwa wadogo tulikuwa tunacheza mpira barabarani. Ghafla kakatokea kanyoka kadogo kakaanza kumkimbiza dogo mmoja mpaka kakamgonga. Dogo alianguka palepale akafa. Nilikuwa darasa la kwanza ila mpaka Leo lile tukio naliwaza. Maana hatukumwona nyoka alipotokea na baada ya tukio hatukujua kaenda wap afu tulikuwa watoto wengi ila alituacha wote na kumfukuza Ben
Duuu!RIP Ben.
 
Back
Top Bottom