Ziito Kabwe ameongea ukweli mchungu

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,611
Reaction score
164,629
Zitto Kabwe:
Wakati Biashara zinafungwa mawaziri walikuwa wanasema kuwa wanaofunga ni WAPIGA DILI. Leo nimeshangaa kuona eti Rais anashangaa kwanini Biashara zinafungwa. Eti na maagizo yanatoka kuwa TRA isifunge Biashara za Watu sababu za Kodi. Biashara zaidi ya 200K zimeshafungwa!

Ziito Kabwe:
Leo siku nzima nimefuatilia Mkutano wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara kutoka nchi nzima. Nawapongeza Wafanyabiashara waliojitoa bila woga kueleza hali halisi. Yote yaliyosemwa tumekuwa tukiyasema Bungeni na Nje ya Bunge. Fikra zangu kuwa tunahitaji Uongozi mpya zimeimarika

Zitto Kabwe:
Ninawasihi Watanzania kuwa tusipumbazwe na haya ‘mateke ya punda anayekata Roho’. Serikali ya CCM ya awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli haipaswi kuongezewa hata siku moja Ikulu. Njia ya uhakika kurejesha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi ni kufanya MABADILIKO.

Zitto Kbwe:
Baada ya mkutano ule wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara nimetazama makadirio ya makusanyo ya Kodi za Wafanyakazi nchini kwa Bajeti ya 2019/2020 na nimekuta makadirio yameshuka kwa zaidi ya TZS 500 Bilioni. Hii maana yake ni kuwa ajira rasmi zimeshuka sana

Chanzo:Ukurasa wake wa twitter.

My take:
Ipo siku tutakuja kuelewa ukweli huu wakati tukiwa tumechelewa.

CCM ni wajanja sana tumieni akili watanzania(hapa kuna siasa inaendelea).

Kushughulikia watu wachache kwa faida ya chama na kiongozi wao kwao si tatizo.

Maandalizi ya 2020 yanaendelea.

 
Ukweli ni kuwa Mh. Rais amefanya makosa mengi sana kwenye uchumi, demokrasia na haki za binadamu.

Tunachoshukuru ni kuwa na yeye ameanza kuyatambua makosa aliyoyafanya lakini kwa bahati mbaya damage iliyofanyika ni kubwa, na ni vigumu sana kuyaondoa madhara yake hata kwa miaka kumi. Leo Tamzania imeingizwa kwenye kundi la risk countries for foreign investments.

Makosa yaliyofanyika katika awamu hii yanatukumbusha umuhimu wa katiba mpya ambayo haimpi mtu mmoja mamlaka ya kufanya chochote anachokitaka bila ya kushirikiana na taasisi nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…