TESRA
JF-Expert Member
- Nov 25, 2017
- 416
- 416
Mkoa wa Mbeya ulio nyanda za juu kusini ukiwa umepakana na mkoa wa Rukwa,njombe, singida pamoja na nchi jirani kama vile Malawi na Zambia. Wakaaji wa jiji hili wengi wakiwa ni Wasafwa, Wanyakusya, Wandari, Wamarira, pamoja na makabira mengine kama wakinga, nk Mbeya ina wilaya km vile
1. Rungwe: ni kama km 50 hivi kutoka Mbeya mjini hadi wilaya ya Rungwe. Rungwe ni wilaya iliyo barikiwa kuwa na ardhi nzuri yanye kustawisha mazao km vile chai, kahawa, ndizi, parachichi, na matunda mengine Rungwe ni yakijani mwaka mzima uku kukiwa na mvua za kumwaga pamoja na baridi kali.
Pia kuna mlima Rungwe wenye kuifanya wilaya hii ivutie wakaaji wa wilaya ya Rungwe ni watu wema sema, wakalimu na wenye kupenda wageni.
2. Kyela: hii ni wilaya iliyo kusini mwa mkoa wa Mbeya. Hii wilaya inasifika sana kwa kilimo cha mpunga,kakao,nk ...hali ya hewa na nzuri kukiwa na joto la wastani pamoja na mvua za maana kuanzia mwezi wa pili mwishaon hadi mwezi wa nne. Asilimia kubwa ya wakaaji wa hii wilaya ni wakulima hasa mpunga pmj na kakao. Pia kuna ziwa Nyasa watu wanafanya uvuvi pamoja na utalii ktk ziwa hili kuna Matema beach, mwamunyange beach nk., pia biashara kwa sana ktk wilaya ya kyela ambapo wafanya biasha kutoka Malawi hufika wilaya ya kyela kununua badhaa,,,,wakaaji wa wilaya ya kyela ni wakarimu sana.
3. Mbarali: ni miongoni mwa wilaya iliyo mkoa wa Mbeya ni wilaya ya kwanza unapokuwa ukiingia Mbeya kutokea njombe,iringa,nk wilaya ina hali ya hewa nzuri joto lipo lipo,,pia kilimo cha mpunga na mahindi hufanyika wilaya hii.
4. Ileje: Hii wilaya imepakana na wilaya ya Kyela pmj na rungwe. Hali ya hewa ipo vizuri sana kilimo cha mpunga na mahindi hufanywa na wenyeji wa hii wilaya.
5. Chunya: Dhahabu hupatikana wilaya hii. Kilimo cha mahindi kipo ndani ya wilaya hii ya chunya. JHali ya hewa ipo vzr sana. Hizo ni baadhi ya wilaya zilizo ndani ya mkoa wa Mbeya ulio barikiwa kila kitu hasa katika upatikanaji wa chakula, ardhi yake inastawisha kila kitu. Kuna shule kibao ndani ya mkoa wa Mbeya, Mbeya High School, Loleza, Iyunga, Mporoto Rungwe High School, Kyela High School nk. Miundo mbinu ipo ya kutosha hasa barabara wilaya zote zimeunganishwa kwa rami. Ni kitovu cha kibiashara kwa nchi kama Zambia, Malawi ambapo wafanya biashara hufika mkoa huu kwajili ya kufanya biashara. Kuna sehemu nying nzuri kwa ajili ya kula bata km vile beach za ziwa nyasa. Kuna hoteli nzuri. Pia kuna kimondo kilichopo mbozi, kuna daraja la mungu, niwewe tu ushindwe maisha Mbeya.
NJOO UTEMBELEE MBEYA