Zifahamu vyema Lugha za Mwili katika Mapenzi

Zifahamu vyema Lugha za Mwili katika Mapenzi

saudari

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
2,655
Reaction score
2,783
Pengine hii inawahusu walio katika ndoa na ambao bado!Ni zipi hasa lugha za mwili katika mapenzi?! Hapa nnazungumizia ishara, milio au sauti fulani ambazo ukisikia au kuona kutoka kwa mwenza wako inakupasa uchukua hatua stahili kulingana na mzingira husika. Kwa wale ambao tupo katika ndoa naimani unanafasi nzuri ya kumsoma mwenza wako na kuweza kugundua anahitaji au anamaanisha nini akiwa hivyo.
Kuna baadhi ya wanawake huwa hawawezi kuwaambia waume zao kwamba wanawahitaji kimapenzi, badala yake huweza kujitegesha au kujirahisi mbele zao, kwani wanajua kuwafanyia hivyo kutaamsha hamu kwa waume zao na hatimaye kuipata starehe hiyo pamoja. Mume yakupasa uwe unausoma mchezo mapema kwani si wanawake wote wataweza sema au kujitegesha na ndio maana tunasisitiza isipite wiki bila kupeana na mwenza wako.

Pia wanawake nawashauri wawe "wachokozi" kidogo maana kuna wanaume huwa hawaanzi mashambulizi mpaka washambuliwe, kama hali ipo hivyo basi mwanamke inabidi ndo uwe mpangaji mashambulizi ya awali.

Mwisho niwaambie Mke na Mume, kama inavyowapasa kujua sehemu za mihemuko baina yenu, inawapasa pia muelewe lugha za miili yenu. Miili inaongea bwanaa, ipeni nafasi!!!
 
saudari
umenena kweli akina domozito kama mimi wanawake inabidi watusaidie.Maana kuna wengine asipoambiwa hata mwaka utaisha niko busy,,japo wanawake wengi bado wanaona tendo hili la kueleza hisia zao kama jambo la aibu
Nimuulize Purple na Lisa je sifa hii ni maumbile au inaweza kubadilishwa
 
Last edited by a moderator:
Maandalizi ya ngono baina ya mume na mke ni "process" ambayo yapaswa kuanza kwa maandalizi ya akili halafu baadae mwili, mazingira n.k hufuata....
 
Maandalizi ya ngono baina ya mume na mke ni "process" ambayo yapaswa kuanza kwa maandalizi ya akili halafu baadae mwili, mazingira n.k hufuata....

Kwanza muwe na mawasiliano mazuri ndipo yote mnaweza kuyafanikisha salama.
 
Kumsisimua mwanamme haihitaji much effort...wanawake msiwe wavivu kama unampenda mwenzio
 
saudari
umenena kweli akina domozito kama mimi wanawake inabidi watusaidie.Maana kuna wengine asipoambiwa hata mwaka utaisha niko busy,,japo wanawake wengi bado wanaona tendo hili la kueleza hisia zao kama jambo la aibu
Nimuulize Purple na Lisa je sifa hii ni maumbile au inaweza kubadilishwa

Ni kweli Tatra, Wanawake tumeumbwa kufuatwa na si kufuata, Nina maana gani, ni kwamba mwanamke hawezi kumfuata mwanaume na kumambia nakupenda, hata kama anampenda, tatizo kutamka hilo neno ni gumu sana,mana unaweza jifikiria kuwa atanifikiriaje, je ataniona mm malaya? sasa hapo ndipo pangumu.
Sasa ili ujue kama kakupenda wengi wanatumia Body Language, mfano wengine wanajipitisha, wengine unakuta kila saa anakuangalia, mwingine unakuta anakutumia sms za mapenzi kila mara, mwingine anakuwa anatake care of u kivipi anakupigia simu asubuhi, anadai anakusalim tu, ikifika mchana anakukumbusha kwenda kula, akitoka jioni kwenda home anakuaga . Sasa kama ni mwanaume rijali lazima utaelewa kuwa amekupenda.
 
Basi kama ndio hivyo nina safari ndefu,,kumbe mimi tu napenda ila no real feedback.Thnks
 
hata hizo dalili sijawahi kuona kwa msichana akinifanyia

Umeshafanyiwa sana, sema wewe ndiyo huzijui, sidhani kwamba hakuna msichana hata mmoja aliyekupenda wewe, haiwezekani, sema hujasing'amua bado.Jitahidi kuwajua wasichana wana trick nyingi sana.
 
Back
Top Bottom