Zidisheni kelele na pazeni sauti, tumtoe nyoka pangoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zidisheni kelele na pazeni sauti, tumtoe nyoka pangoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Oct 18, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Ufisadi wazua balaa kongamano la siasa

  2008-10-18 10:32:03
  Na Simon Mhina

  Kimbunga cha ufisadi bado kinakitesa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi kwamba, sasa hali ya mgawanyiko inajidhihirisha ndani yake kutokana na wabunge wake kujikuta wakimgunia kada wao, Dk. Hans Kitine, aliyesema kuwa nusu ya serikali imejaa mafisadi.

  Dk. Kitine akitoa maoni yake katika mjadala wa mada zilizowasilishwa kwa nyakati tofauti na Jaji Joseph Warioba na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, kwenye kongamano kuhusu rushwa katika siasa na ugharimiaji wa shughuli za vyama vya siasa, alisema iwapo mafisadi waliopo serikalini watashughulikiwa, itabidi nusu ya viongozi wa serikali watoswe, hali ambayo itatikisa taifa.

  Dk. Kitine ambaye amewahi kushika nyadhifa nyeti serikalini, ikiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, waziri, mkuu wa mkoa na mbunge, alisema haoni sababu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuendelea kuwajibika kwa Rais. Alisema badala yake Takukuru inapaswa kuwajibika moja kwa moja bungeni.

  "Unajua suala la rushwa ni kubwa, lakini nasikitika kusema serikali haijalichukulia kwa uzito unaostahili", alisema huku wabunge wa CCM waliohudhuria wakiguna. Ingawa wanasiasa wengine walionekana kushangilia mchango wa Dk. Kitine.

  Dk. Kitine alisisitiza kwamba rushwa nchini ni pana na inawagusa watu wakubwa serikalini, hivyo kwa vile Rais naye ni binadamu, basi suala la Takukuru lisiwe chini yake.

  Kama mnavyofahamu tabia za watendaji wetu, kumpa Rais wetu mzigo wa kuwashughulikia wala rushwa pekee tunampa kazi ngumu sana, naye yule ni binadamu kwa hiyo ili kumuondolea lawama yoyote ni vema Takukuru wakawajibika moja kwa moja bungeni.

  "Unajua Rais akiamua kuwashughulikia walarushwa wote na mafisadi, nusu ya viongozi serikalini watakwenda na maji", alisema hali iliyoamsha miguno kutoka kwa wabunge hao waliokuwa wanahudhuria kongamano hilo lililomalizika jana.

  Kutokana na kuzomewa huko, Dk. Kitine alionekana kukasirika na kuwaeleza wana CCM hao kwamba mwaka 2010 watavuna kama kile walichovuna katika Uchaguzi mdogo wa Tarime iwapo wataendelea na kupuuza mawazo ya ukweli juu ya mapambano dhidi ya rushwa.

  "Mnanipuuza eeh! Sawa bwana endeleeni hivyo hivyo na mjue mwaka 2010 mtavuna kama mlichovuna Tarime, fanyeni kama mlivyofanya Tarime halafu 2010 mtaona habari yake, vita dhidi ya rushwa si lelemama, kuna watu wanapambana na rushwa kama mchezo wa kuigiza, wala rushwa ni wengi mno Kikwete akiamua kuwamwaga serikali itapwaya", alisema.

  Dk. Kitine alisema kutokana na ukweli kwamba viongozi wengi wamezoea rushwa na kuiona kitu cha kawaida, hivi sasa viongozi wanachukua rushwa waziwazi bila kuficho.

  Naye Katibu Mkuu Mtendaji wa Chadema, Victor Kimesera, ambaye ni mzaliwa wa Kiteto, alipandisha mori za Kimasai na kuufanya ukumbi kuzizima.

  Kimesera alisema zamani wakiwa shuleni walikuwa wakifundishwa uzalendo na kila kijana alijivunia uadilifu. Alisema tatizo la kukua kwa rushwa linatokana na Watanzania kukosa uzalendo.

  "Hata tukifanya makongamano mangapi hayatasaidia kupunguza rushwa kwenye uchaguzi, hata tungetunga sheria gani haiwezi kuzuia rushwa ambayo ni tabia inayotokana na dhamira ya mtu binafsi", alisema Kimesera na kisha kuanza kuzungumza Kimasai.

  Baada ya kuzungumza lugha hiyo kwa muda, Kimesera aliwakumbusha kwamba yeye ni Mmasai anayekasirishwa sana na uonevu.

  "Nimechukia kwa vile hata ukitunga sheria kali kiasi gani za kupambana na rushwa hazitafua dafu kwa vile wanaozisimamia nao ni wala rushwa", alisema Kimesera alisema hata kumlaumu Mkurugenzi wa Takukuru ni kazi bure kwa vile naye anawajibika kwa wanasiasa kwa lengo la kulinda mlo wake.

  Awali Waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, alisema rushwa katika siasa nchini, si kubwa kama watu na baadhi ya taasisi wanavyovumisha. Alisema japokuwa tatizo la rushwa lipo, lakini kuna taasisi ambazo kwa makusudi zinaongeza chumvi. Hata hivyo alisema serikali ipo katika mchakato wa kutathimini kwamba mtindo unaotumika kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa unafaa, au ubadilishwe.

  "Tunatafakari kuwa na nyongeza ya kuwagharimia wagombea Urais katika kampeni, lakini pia tunatafakari kuwa kufanya hivyo itakuwa matumizi bora ya fedha za walipa kodi. Hivyo tunaposikia makongamano kama haya yanayoshirikisha wadau wa siasa tunafarijika maana tutapata michango katika kuboresha", alisema Waziri huyo.

  Juzi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, katika mada yake iliyosomwa kwa niaba yake na Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Ferdinand Wambali, alisema rushwa katika uchaguzi ndiyo chimbuko la ufisadi.

  Hoja kama hiyo pia ilielezwa na Jaji Joseph Warioba katika kongamano hilo, huku Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Amir Manento, akishauri kwamba utaratibu wa kuteua mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge ubadilishwe ili mawaziri wasiwe wabunge.
  * SOURCE: Nipashe


  It shall soon be time to stand up and be counted. That time is not too far, it is not too distant - that time is NOW.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Yaani yale yale niliyoyasema majuzi, duh saafi sana ingawa na yeye ni fisadi pia aliyeshikwa, na angeulizwa maswali kuwa kwa nini hakuwashughulikia alipokuwa kwenye power pamoja na kwamba aliwahi kushika nafasi nzito sana na muhimu katika taifa letu kwenye upande huo huo wa dola?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Mkuu field marshall es

  angeanza kushugulikiwa yeye na kesi bado ipo wala ,,asikimbie
  ila tunamshukuru kwa kusema uwazi,mnajua ndugu zanguni ni kwamba hii nchi tusikate tamaa ya kuongea hata kama kupigana tunashindwa tuwaonjeshe kama wanatarime ikibidi waache kuchezea utu wa binadamu
  alamsiki
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ni kweli hakuwashughulikia, lakini ukweli kwamba mambo yalikuwa hayajawa mabaya kama ilivyo sasa!

  Walau wakati ule raisi alikuwa akiwatumikia watu badala ya kakundi ka mafisadi!

  Hata hivo nampongeza kwa kujitoa muhanga kusema ukweli mbele ya mafya hawa! Kwani ukweli ni kwamba kila alilo li sema ni kweli tupu, na watu clean ndani ya CCM mnalijua hilo, shida yenu ni kule kuthubutu kama alivo fanya yeye, you need more ten Kitines kuikomboa CCM vinginevyo kaeni tayari!
   
Loading...