Ziara ya Wassira Ulaya Imeleta Mafanikio, Avuta Kiwanda cha Matrekta Tanzania

Hii habari ya Poland kutaka kujenga kiwanda cha kuunga matrekta tuliambiwa tangu mwaka juzi; ina maana hata makubaliano yalikua bado? Nadhani Watanzania tunapenda sana kupiga makelele wakati hakuna tufanyalo.

Kumbuka kuwa wakati huo Mh Wasira hakuwa Wizara hiyo,baada ya kuingia tu kaanza na kero za wakulima kwa kusimamia ulipaji madeni yao ya mahindi,
Na sasa anawasimamia kuwasogezea zana za kisasa za kilimo.
Binafsi nampongeza Mh Wasira.
 
Mkuu, Wataalam/Maengineer hawana tatizo hata kidogo, wenye matatizo ni wana siasa ambao kila kitu wanakichukulia kisiasa siasa tu - Mtanzania mwana siasa aliyekuwa tofauti na wenzake kimawazo na kuona mbali ni Baba wa Taifa, hakuwa binadamu wa kawaida yule! Aliheshimu sana masuala ya sayansi na teknolojia kawapeleka wanafunzi wengi Ulaya ya Mashariki na Magharibi tulikuwa na wataalamu lukuki lakini wanasiasa wakawapiga danadana na kuwakatisha tamaa - wengi wao wakatimukia nchi za nje ambako wamefanya maajabu na kuheshimika - wapo Watanzania ambao wanafanya kazi kwenye taasisi ya NASA huko Merikani nk, katika sauala hili la sayansi na Teknolojia hata Mh.JK analipa kipaumbele sana, tatizo ni utekelezaji kwa wale aliyo wapa dhamana za kusimamia nyanja hizo.
Shiiiiiih!FaizaFoxy atakusikia!
 
mpaka 70s tanzania ilikuwa ina kiwanda cha kuunganisha matrekta, kikataifishwa kuuliwa na kufunguwa na badala yake kikajengwa kiwanda cha majembe ya mkono na wachina (ufi).

Fikiri, tunauwa kiwanda cha matrekta tunafunguwa kiwanda cha majembe ya mkono!

Inasikitisha sana.
lmfao!
 
Mkuu kama nakumbuka vizuri Serikali haijaruhusu kuhanza kupiga kampeini za URAIS - post hii ina kila dalili za kuelekea huko ingawa in a watered down format.

Masuala ya wa Polish kusaidia ku-assemble matrekta nchini mbona yaliwahi kujadiliwa hata kabla ya Wassira haja hamia Wizara ya Kilimo, sasa haya mambo ya kuhanza kumpamba pamba na kuweka kachumbali yana uhusiano gani na ziara ya Kiserikali Nchini Poland si anafuatilia tu yaliyo hanzishwa na Waziri aliyekuwepo Wizara ya KILIMO.

Kwani unadhani ni Waziri gani ambaye huwa hatekelezi aliyo yakuta yameachwa na mwenzie?
Na je unadhani hilo ni NJE ya majukumu yake ili tusimpe hongera?
Na je unadhani hapa tume mpa hongera au tumempamba?
Na je nikikwamboa wewe UNAWIVU utakataaa? ImageUploadedByJamiiForums1429675526.880673.jpg
 
Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Stephen Wasira, siku ya jana tarehe 17/04/2015 alikuwa na Kikao na Uongozi wa Chuo kikuu cha Warsaw cha Sayansi ya Kilimo jijini Warsaw Poland (Warsaw University of Life Sciences) mkutano ulilenga kuona uwezekano wa kuanzisha ushirikiano wa Vyuo vya Kilimo vya Poland na Vyuo Vya Kilimo vya Tanzania, mkutano uliongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Marek S. Szyndel.

Leo tarehe 18/04 Mhe. Wasira atakutana na Rais wa jiji la Lublin Ndugu Krzysztof Zuk. Mkutano utafanyika ofisi za Manispaa ya jiji hilo.
Wiki ijayo kutokana na ratiba msafara wa Mhe. Wasira utashiriki kwenye Mkutano wa Shirikisho la Kiuchumi Ulaya (European Economic Summit) katika mji wa Katowice.
Katika mkutano huu wa Saba wa Shirikisho hili (7th European Economic Congress) utajumuisha majadiliano ya tatu ya ushirikiano wa kiuchumi wa Afrika na Ulaya ya Kati.(3rd Africa-Central Europe Economic Cooperation Forum) na Kongamano la 4 la ushirikiano wa kiuchumi la Ulaya na China (4th Europe- China Economic Forum) pamoja na Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Poland na Japan(Poland-Japan Economic Meetings) na Mkutano wa Mwaka wa Uchumi kati ya Poland na Chechinia (The Annual Polish-Czech Economic Meeting).
Pamoja na Mambo mengine ziara ya Mhe. Wasira na msafara wake wa maofisa wachache imekuwa yenye tija baada ya kufanikiwa kuweka makubaliano ya Kushirikiana kati ya Tanzania na Poland kujenga kiwanda cha kuunganisha Matrekta hapa Nchini chini ya SUMA JKT, na ujenzi wa Maghala makubwa ya kuhifadhia chakula chini ya NFRA.
Hongera Mhe.Wasira na msafara wake kwa kazi nzuri, baada ya ziara karibuni nyumbani.

Kiwanda cha ku-assemble ndo unakuja na mbwembwe zote hzo?Mm nilidhanı wanajenga kıwanda cha kuunda matrekta hapa na watatumia mavito ya Mchuchuma na Lıganga.
 
Kinachosifiwa hapa ni upuuzi wa hali ya juu. Huwezi kuanza kushangilia kwa kuambiwa kuwa jamaa watafungua karakana ya kuunganisha treka. Hapa hakuna ujuzi wowote tutakaopata. Kazi ya kuunganisha trekta hata fundi wa gari ambaye anaweza kushusha engine na kuirudisha anaweza kuunganbisha hayo matrekta yenu. Lakini, kifaa chochote kikiharibika huwezi kutengeneza kipya hata kama ni kidogo namna gani, mwishoe itabidi tu uagize kutoka kwao.

Sisi kama Tanzania tunahitaji kuwa na ujuzi wa kuchimba chuma chetu kilichojaa kule Liganga-Ludewa, kukiyeyusha na kutnegeneza vifaa mbali mbali. Kama hujui hata microstructures, chemical compositions, fatigue life and all sort of mechanical properties na hauna hata wataalam wa kuhakiki siutakuwa unafurahia tu kuwa umepata trekta halafu baada ya muda yanaanza kuharibika.

Metallurgists an mechanical engineers tunao lakini Serikali haina vipaumbele vya kuendeleza viwanda na kwa chuma tulichonacho hata viwanda vya kutengeneza gari inawezekana.
Viongozi wote waliotangaza nia ya kuutaka Urais sijaona mwenye nia na uwezo wa kubadilisha Matatizo yetu ya kiuchumi,Viwanda na Miundombinu walau hata kuyalinganisha na haya uliyoyataja hapa.

Tumekosa weledi na viongozi shupavu wa kuweka vipaumbele katika malengo ya Taifa letu.

Walau Wasira may have something to contribute.
Lakini roho inaniuma kuona Nchi hii inavyochelewa kukua kiuchumi.
 
Sawa Mkuu! Lakini mbona yule mwingine amesafiri sana na hajapata mafanikio makubwa kama y huyu kwa safari moja!

Watu wana namna hii wengi ndo wafuasi wa ACT,little brain.Karakana ya kuassemble anaona dili saana!Washamba nyie bandugu!Israel watu wenye akili zenu hizo mnawekwa custody kuliko kuchafua cream ya wateule!
 
Nchi hii ina watu wanaopenda kulalamika tu muda wote, hamtoi suluhu kazi kulaumu tu.
Jifunze kidogo kwa wenzako hapo juuu wameandika nini.
Watu kama wewe na mimi ambao ni vilaza na tumekosa ubunifu ni rahisi Sana siku zijazo kuanzisha Xenophobia kwasababu akili zetu zimeishia hapo.
 
Kilimo kwanza na power tiller, subirini maumivu mengine, mimi nawasubiria kwenye sanduku la kura.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kiwanda cha kuunda na kuunganisha, kuunga ni kuwa vifaa vyote vinatengenezwa huko Poland hapa vinakuja kuunganishwa tu kwny karakana na sio kiwandani tena...kusema kiwanda cha matrekta kinajengwa Tanzania ni kujidanganya sana...labda itajengwa karakana..

Mbona hata piki piki za kichina zinatengenezwa huko na hapa zinakuja kuunganishwa???

Kiswahili ni lugha yetu lakini ni ngumu bado!
Sasa unadhani nini kifanyike ili kuisaidia Nchi? Bora karakana ili tuanzie kujifunzia hapo au bora aende kubembea Ulaya halafu tuendelee kukuna nazi na kula madafu?
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kiwanda cha kuunda na kuunganisha, kuunga ni kuwa vifaa vyote vinatengenezwa huko Poland hapa vinakuja kuunganishwa tu kwny karakana na sio kiwandani tena...kusema kiwanda cha matrekta kinajengwa Tanzania ni kujidanganya sana...labda itajengwa karakana..

Mbona hata piki piki za kichina zinatengenezwa huko na hapa zinakuja kuunganishwa???

Kiswahili ni lugha yetu lakini ni ngumu bado!

Ama kweli lugha ngumu...karakana kwa Kiingereza ni garage na kiwanda cha kuunganisha matrekta/magari ni Tractor/automobile assembly plant. Ila bila kujali technicality za lugha karakana au assembly plant vyote vinaongeza ajira directly and indirectly
 
Acha wivu,Mawaziri wangapi wanaenda Ulaya na America kubembea? Wengine wanaenda na Wasnii wa Bongo Fleva wamenegotiate na kufanikisha jambo gani?
Huyu Bwana Waziri yuko Vizuri mnoo!

Hata prezidaa anakwenda kubembea. Na kuunganisha matrekta sioni kama ni ishu kubwa kwa serikali inayojua kazi yake. Ilitakiwa sasa hivi tuwe tunaweza kutengeneza locomotives za kwetu frm scratch. Nina imani materials zooote (au karibia zote) tunazo nchini kwetu. Tatizo ni kwamba serikali nzima ni kama haina mtu hata mmoja mwenye uwezo wa kufikiria kuhusu mustakabali wa nchi siku zijazo. Kila mtu analenga next election tu, basi! Tujifunze kupitia wale waliokuwa wachovu kama sisi mfano South Korea wamefika fikaje hapa walipo wakati sisi tunasindikiza harusi.
 
Kinachosifiwa hapa ni upuuzi wa hali ya juu. Huwezi kuanza kushangilia kwa kuambiwa kuwa jamaa watafungua karakana ya kuunganisha treka. Hapa hakuna ujuzi wowote tutakaopata. Kazi ya kuunganisha trekta hata fundi wa gari ambaye anaweza kushusha engine na kuirudisha anaweza kuunganbisha hayo matrekta yenu. Lakini, kifaa chochote kikiharibika huwezi kutengeneza kipya hata kama ni kidogo namna gani, mwishoe itabidi tu uagize kutoka kwao.

Sisi kama Tanzania tunahitaji kuwa na ujuzi wa kuchimba chuma chetu kilichojaa kule Liganga-Ludewa, kukiyeyusha na kutnegeneza vifaa mbali mbali. Kama hujui hata microstructures, chemical compositions, fatigue life and all sort of mechanical properties na hauna hata wataalam wa kuhakiki siutakuwa unafurahia tu kuwa umepata trekta halafu baada ya muda yanaanza kuharibika.

Metallurgists an mechanical engineers tunao lakini Serikali haina vipaumbele vya kuendeleza viwanda na kwa chuma tulichonacho hata viwanda vya kutengeneza gari inawezekana.

Huko mbona Kikwete kishafanya zamani, umelala?

Amka uelewe na sasa Wasira anawaleta waunda matrekta, kwa kuwa chuma unacho na smelter tayari umewekewa iliyobaki kazi ni kwako tu, ni "part" ipi utawaundia ili wasiiagize kutoka kwao, uki meet standard na design nzuri, kwanini wasinunuwe kwako?

"The construction of the iron ore mining and iron smelting plants at Liganga will start early next year and production is scheduled to start in 2018," Mkucha said.

The construction is a joint venture between China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) and NDC. About $3 billion will be spent on both projects.
Mkucha said "As we will be producing 1.1 million metric tonnes a year, Tanzania will save a lot of revenue as the importation of iron will be reduced to pave way for local production.

Soma zaidi: Tanzania set for ore sales
 
Ulitaka iwe nini? Waafrika ndo maana mnauwana wenyewe kwa akili finyu, ili upate 9 lazima uanze na Moja.

Mbona hao wazungu kwenye kikao wanaonekana kujawa na hofu, kwa nini? Jamaa wabaguzi kweli. Halafu ile suti ilivyoliacha wazi tumbo la Rais ajaye, mmmh!
 
hichi chenyewe kinataka 'ushirikiano' kati ya Poland na Tz. Je, waTZ hawa wapo tayari kufanya kazi bila 10% maana najuwa Poland watataka kufanya 'ushirikiano' kwa njia za kawaida tu.

Ndiyo maana tunataka viwanda waendeshe wenye viwanda, vile vya kutaifishwa na alivyojenga Nyerere havikuwa na tija yoyote kwa kuwa aliwapa wajomba zako kuviendesha wakaviua vyote kwa wizi, uvivu, ubadhirifu, uongo, majungu, uchawi, upumbavu, ujinga na bila kusahau laana ya waliodhulumiwa.
 
FF, uko sawa kabisa unachoandika. Siwezi hata kuongeza labda tu kusisitiza.

Kiwanda hiki ni mkopo na si msaada kama wengi wanavyojadili.

Pia kama kitaanza hapa kazi, baadhi ya bidhaa zinaweza kuanza kutengenezewa hapohapo Tanzania.

Matairi yanaweza kutoka General Tyre Arusha. Vyuma vikatoka Liganga.

Kwa vitu kama Engine kwa sasa ni ngumu sana na ndiyo maana kuna makampuni wao ndiyo watengenezaji wa engine na wengine hununua kwao. Ukiangalia hata hizi Ursus au Belarus za Belarusia, engine zake ni haohao akina Pelican, John Deer etc. Hata kwenye magari, wengi hutengenezewa hizo engine na sababu ni kuwa technology yake ni ngumu sana kwa sababu kwenye engine block, wanatumia Alloy kuunda.

Hao Ursus watakuwa hapo Tanzania kwa mfano kwa miaka 15 na baadaye Suma JKT wataachiwa na itakuwa mali ya Tanzania na hapo sasa itakuwa uamuzi wetu tufanye nini.

Mhindi alianza na Tata-Benz yaani akishirikiana na Mgeruman. Sasa hivi Tata wako mbali sana na ndiyo owner wa magari ya Rand Rover na Jaguar.

Jaguar-cars.jpg
 
Ndiyo maana tunataka viwanda waendeshe wenye viwanda, vile vya kutaifishwa na alivyojenga Nyerere havikuwa na tija yoyote kwa kuwa aliwapa wajomba zako kuviendesha wakaviua vyote kwa wizi, uvivu, ubadhirifu, uongo, majungu, uchawi, upumbavu, ujinga na bila kusahau laana ya waliodhulumiwa.

Posti yako hii si tu kwamba inawafaa waliofirisi viwanda bali pia safu nzima ya serikali na chama tawala sasa. Wizi, uvivu, ubadhirifu, uongo, majungu, uchawi, upumbavu, ujinga na bila kusahau laana ya wanaowadhulumu. Kila siku wa wanaiba na hawachoki kuiba. Si kwenye madini, umeme wa dharura, ujenzi wa barabara, halmashauri, mahakama, police, hospitali, nk.

Nchi ilishapoteza mwelekeo, kwa maana nyingine, chama tawala kilishapoteza mwelekeo!!
 
= waliofilisi

Waliofilisi ni wale wale waliofanya maamuzi ya kijinga ya kudhulumu (taifisha) na kuwakabidhi watu wasiojuwa kuendesha viwanda.

Naam, yalianza lini? msome Ludovick Mwijage kwa majibu sahihi.

Makosa yalifanyika kwenye misingi ya utawala, njia sahihi zimechukuliwa na hiyo misingi mibovu tuliyoirithi imebomolewa na ndiyo maana hutaona Serikali ikijenga tena kiwanda cha Umma, tumeondoka huko kwenye uozo.
 
Back
Top Bottom