Ziara ya Wassira Ulaya Imeleta Mafanikio, Avuta Kiwanda cha Matrekta Tanzania

Haya Watalamu wetu mnaohusika hapo jipangeni haraka kiwanda kilete Tija kwa haraka sio kukaa tu utekelezaji miaka 15 ijayo.
Mimi huwa nawashangaa hawa wanaojiita Maengineer mara Watalamu, aibu tupu.
 
Mkuu kama nakumbuka vizuri Serikali haijaruhusu kuhanza kupiga kampeini za URAIS - post hii ina kila dalili za kuelekea huko ingawa in a watered down format.

Masuala ya wa Polish kusaidia ku-assemble matrekta nchini mbona yaliwahi kujadiliwa hata kabla ya Wassira haja hamia Wizara ya Kilimo, sasa haya mambo ya kuhanza kumpamba pamba na kuweka kachumbali yana uhusiano gani na ziara ya Kiserikali Nchini Poland si anafuatilia tu yaliyo hanzishwa na Waziri aliyekuwepo Wizara ya KILIMO.
Hivi hata utekelezaji wa majukumu ni kampeni? Kila kitu siasa, naona October ifike haraka tufanye kazi kwa akili, hii tabia ya kuwaza Uchaguzi kila dakika inatuchelewesha.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kiwanda cha kuunda na kuunganisha, kuunga ni kuwa vifaa vyote vinatengenezwa huko Poland hapa vinakuja kuunganishwa tu kwny karakana na sio kiwandani tena...kusema kiwanda cha matrekta kinajengwa Tanzania ni kujidanganya sana...labda itajengwa karakana..

Mbona hata piki piki za kichina zinatengenezwa huko na hapa zinakuja kuunganishwa???

Kiswahili ni lugha yetu lakini ni ngumu bado!
 
Hivi ma - engineer wetu hawana haya idea ya kutengeneza baiskeli?
Kila kizuri mpaka kitoke ulaya tu!!
 
Mungu mbariki wassira wetu ili adumu katika kuwatumikia wanyonge wetu na Mungu amwinue wassira na kumweka pahala pa juu sana ili watu wa Mungu wauone utukufu wake kupitia wassira.
 
Mungu mbariki wassira wetu ili adumu katika kuwatumikia wanyonge wetu na Mungu amwinue wassira na kumweka pahala pa juu sana ili watu wa Mungu wauone utukufu wake kupitia wassira.

Ni vigumu saana kwa Ngamia kuingia kwenye tundu la sindano.
 
Ujinga mtu miaka yote wana ahidi viwanda lakini holaaaa,hatudanganyiki ala nani kakuambia jamhuri ya czech ni chechnia!? We kilaza
 
Watanzania tunapenda kujisifia ujinga tu
Umesema kweli mkuu, wenzetu wanahangaika kuvumbua vitu mbali mbali, kurusha vyombo angani kama ndege zisizokuwa na rubani lakini sisi tunawasifu viongozi kwa kuzurura nje kuomba omba. Hili lilipaswa kuwa ni jambo la aibu baada ya niaka 50 ya uhuru viongozi wetu wanapigana vikumbo nje ya nchi kuomba omba kutoka kwa wale wale ambao miaka 50 iliyopita walikuwa masikini kama sisi au zaidi yetu. Mpaka leo nikikumbuka kauli ya rais wetu huwa nasikia vibaya sana. Eti rais anasema anasafiri sana nje ili kuhemea vibaba ili tusife njaa. Ukweli kuhemea na kuomba omba ni jambo la aibu hatupaswi kujivunia na mimi nawashsngaa sana wenzetu humu JF wanaposhangilia mtindo wa viongozi wetu kugeuza uongozi kuwa ni kwa ajili ya kuomba misaada. Eti kiwanda cha kuunganisha matrekta? Hayo ni maendeleo kweli ya kushinda tunaunganisha vya wenzenu? Tulikuwa tunaunganisha Scania pale kibaha sasa kiko wapi? Eti hata kujenga maghali mpaka tukapige magoti nje? Pikipiki, baiskeli, vyerahani vyote vijana pale Kariakoo wanaunganisha wala hawahitaji kiwanda. Hivi kiwanda cha kuunganisha vitu walivyotengeza wenzetu nacho tutaita ni kiwanda?! Ndio maana tuna watu wanajiita ma injinia lakini uinjinia wao ni kuunganisha tu walivyotengeneza wenzetu kama madaraja, mabomba, magari, compyuta, kufunga transfoma za Tanesco na kuunganisha waya nk kitu kinachoweza kufanywa hata na mtu asiyesomea uinjinia. Kazi ni kuunganisha tu halafu tunaringa kuwa ni mainjinia! Tuvumbue na tutengeze sisi wenyewe hapo ndio tunaweza kuringa kuwa tuna mainjinia!
 
Hui ndio tofauti kati yao na sisi
 

Attachments

  • 1429427341899.jpg
    1429427341899.jpg
    12.9 KB · Views: 216
Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Stephen Wasira, siku ya jana tarehe 17/04/2015 alikuwa na Kikao na Uongozi wa Chuo kikuu cha Warsaw cha Sayansi ya Kilimo jijini Warsaw Poland (Warsaw University of Life Sciences) mkutano ulilenga kuona uwezekano wa kuanzisha ushirikiano wa Vyuo vya Kilimo vya Poland na Vyuo Vya Kilimo vya Tanzania, mkutano uliongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Marek S. Szyndel.

Leo tarehe 18/04 Mhe. Wasira atakutana na Rais wa jiji la Lublin Ndugu Krzysztof Zuk. Mkutano utafanyika ofisi za Manispaa ya jiji hilo.
Wiki ijayo kutokana na ratiba msafara wa Mhe. Wasira utashiriki kwenye Mkutano wa Shirikisho la Kiuchumi Ulaya (European Economic Summit) katika mji wa Katowice.
Katika mkutano huu wa Saba wa Shirikisho hili (7th European Economic Congress) utajumuisha majadiliano ya tatu ya ushirikiano wa kiuchumi wa Afrika na Ulaya ya Kati.(3rd Africa-Central Europe Economic Cooperation Forum) na Kongamano la 4 la ushirikiano wa kiuchumi la Ulaya na China (4th Europe- China Economic Forum) pamoja na Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Poland na Japan(Poland-Japan Economic Meetings) na Mkutano wa Mwaka wa Uchumi kati ya Poland na Chechinia (The Annual Polish-Czech Economic Meeting).
Pamoja na Mambo mengine ziara ya Mhe. Wasira na msafara wake wa maofisa wachache imekuwa yenye tija baada ya kufanikiwa kuweka makubaliano ya Kushirikiana kati ya Tanzania na Poland kujenga kiwanda cha kuunganisha Matrekta hapa Nchini chini ya SUMA JKT, na ujenzi wa Maghala makubwa ya kuhifadhia chakula chini ya NFRA.
Hongera Mhe.Wasira na msafara wake kwa kazi nzuri, baada ya ziara karibuni nyumbani.
Tatizo TZ sio kuanzisha vitu, ni kumaintain vitu, haya anayofanya Wasira hata baada ya Uhuru yalifanyika na viwanda vyote vimekufa, imekuja RUBADA na Kilimo Kwanza, yako wapi waliyoyapanga, kila kitu kinacholetwa Bongo ni kwa ajili ya Mafisadi kuiba. Hata anachofatilia Wasira kitaibiwa tu, count on me
 
There is no Free lunch in this world.

Hizo zote kama zitajengwa basi zitajengwa kwa mkopo. Nchi karibu zote za EU zina huo utaratibu wa kutoa mikopo ya bei nafuu na kulipa kwa muda mrefu. Nafikiri malipo yatakuwa kwenye asilimia si zaidi ya mbili ambao ni nafuu sana. Pia wakati mwingine unakuwa unaambiwa kulipa kati ya miaka 20 au 30.

Hii safari aliianza PM Pinda na sasa ni muendelezo wa kuangalia jinsi ya kupatikana kwa mkopo huo/msaada na kuanza ushirikiano. Kama mkopo huo ungelitoka Bank ya dunia au kwa akina Ruthchilds, malipo yake ni makubwa sana.

Sawa Mkuu! Lakini mbona yule mwingine amesafiri sana na hajapata mafanikio makubwa kama ya huyu kwa safari moja!
 
Acha wivu,Mawaziri wangapi wanaenda Ulaya na America kubembea? Wengine wanaenda na Wasnii wa Bongo Fleva wamenegotiate na kufanikisha jambo gani?
Huyu Bwana Waziri yuko Vizuri mnoo!

Kwanza soma vizuri nilicho andika, wewe usifikiri tunakurupuka tu - tunangalia Dunia in 3D. Soma vile vile paragraph ya mwisho ya ndugu Steven Sambali - kwa nini hamsemi mwanzilishi wa Project hii alikuwa ni Waziri Mkuu, ndugu Wassira anafuatilia tu - lakini hapa mna-blow out of proportion ziara nzima mnafikiri hatuna akili - Mbona hampigii debe mtoto wa mkulima/PINDA aliyebuni Project nzima?
 
Huo ujinga wa kuomba omba sio mzuri.Dunia ya Leo watu wanafanya partnership agreements sio kuomba kusaidiwa.
 
Mungu mbariki wassira wetu ili adumu katika kuwatumikia wanyonge wetu na Mungu amwinue wassira na kumweka pahala pa juu sana ili watu wa Mungu wauone utukufu wake kupitia wassira.

Nikisema mmeanzisha kampeini mapema mno mnasema ni mambo ya uzushi na wivu!!!
 
IT'S ONLY IN SOUTH AFRICA WHERE AN
ILLITERATE VILLAGER THINKS A QUALIFIED
MEDICAL DOCTOR FROM ANOTHER AFRICAN
COUNTRY STOLE HIS JOB....yeah
 
Back
Top Bottom