Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Umeme wa REA Jimboni Ndanda

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Mbunge Wa Jimbo la Ndanda Mhe. Cecil David Mwambe amefanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa usambazaji umeme wa REA Jimboni akiwa ameambatana na Meneja wa Tanesco (W) pamoja na Mkandarasi Namis corporate, tarehe 20 Julai, 2023.

Ukaguzi umefanyika kwenye kata ya Mlingula, Namajani, Namatutwe, Chiwale, Lukuledi, Chikunja na Chikukwe.

Mhe. Mwambe alipata nafasi ya kuongea na wananchi wachache waliojitokeza baada ya kupata taarifa ya ujio wake.

Mhe. Mwambe aliongea na wananchi wa Chiroro ambao walipewa taarifa kwamba mkandarasi ameanza kazi na waliahidiwa hadi mwezi September umeme utakua umewaka kwenye vijiji vya Chiroro, Migombani na Ngalole.

Kata ya msikisi leo wananchi wameanza kuwashiwa umeme na zoezi likiwa linaendelea.

Kata ya Chiwale alitembelea chanzo cha maji kwenye kijiji cha Nanyindwa ambapo patapelekwa umeme kwa ajili ya kufunga pump ya kusukuma maji kujaza Tank kwenye kijiji hicho.
IMG-20230720-WA0171.jpg
 
Back
Top Bottom