Ziara ya Kenneth Nollo katika Kijiji cha Isangha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,862
930

ZIARA YA MHE. KENNETH NOLLO KIJIJI CHA ISANGHA KATA YA CHIBELELA

Mbunge Jimbo la Bahi, Dodoma Mhe. Kenneth Nollo Jana tarehe 13 April 2023 amefanya Mkutano wa hadhara Kijiji cha Isangha Kata ya Chibelela, pamoja na mambo mengine Mhe. Kenneth Nollo aliwajulisha wananchi kupatikana kwa fedha za ujenzi wa Madarasa Matano (5), Nyumba ya Mwalimu na Matundu Manne ya Vyoo.

Hii ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwaka 2022 akiwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali ya kumaliza Darasa la Saba kwa Shule hiyo. Mhe. Kenneth Nollo ameishukuru sana Serikali kwa namna ambayo imeleta fedha hizi kwa wakati na ujenzi utaanza wiki ijayo na Majengo yanatakiwa kukamilika ifikapo Mwezi Juni 30, 2023.

Aidha, Wananchi wameipongeza Serikali kwa ujenzi wa Kilomita 36 pamoja ujenzi wa Daraja la Mpunguzi-Chibelela. Mhe. Kenneth Nollo amewaahidi wananchi wote wa Bahi kuwa atajitahidi kwa uwezo wake kuendelea kufuatilia na kutekeleza changamoto zinazowakabili kwa maeneo yao.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.03.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.03.jpeg
    61.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.04.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.04.jpeg
    58.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.04(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.04(1).jpeg
    49 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.04(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.04(2).jpeg
    39 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.05.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-14 at 15.41.05.jpeg
    52.1 KB · Views: 3
Sikuwahi jua huyu jamaa ni mbunge ,Japo nilikuwa namhudumia huduma za kifedha pale Dodoma area d
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom