Ziara ya ghafla ya mgombea edward lowasa

Ziara ya ghafla ya mgombea edward lowasa

Joined
Dec 4, 2006
Posts
18
Reaction score
33
Leo majira ya mchana ndani ya maeneo ya Musoma mjini mkoa wa Mara tulipata ugeni.Na mgeni huyu sio mwengine ni Edward Ngoyai Lowassa.ilikuwa ni ugeni wa ghafla na kwa kweli kwa ughafla wake tumejionea mengi.Kuanzia afya yake aliposaidia kushushwa na kupandishwa kwenye ndege na pili jinsi hela zilizochangwa juzi viwanja vya Hekima,Mikocheno Dar es salaam zilivyoanza kutumiwa.Mie ninawaletea safari nzima.

Baada ya kutua uwanja wa ndege majira hayo, Ndg.Lowasa alipokelewa na Ndg.Veda Mathayo ambaye alimchukua hadi kwenye shamba lake huko Bunda ambapo alifanya naye mazungumzo alimkabidhi taarifa ya hali ya kisiasa ilivyo na ilivyobadilika ikiwemo kuwa Mwenyekiti na Mjumbe wa Nec toka Bunda amekimbia Kambi na sasa anamuunga mkono Mh.Wassira pamoja na wao ni Mnec na Mwenyekiti wa Butiama pia.

Lowasa ambaye alionekana kuchoka sana kiafya na nguvu za kutembea aliamua kuwatafuta wajumbe hawa.Akiwa njiani alisimama Bunda na kuongea na viongozi hao wa Bunda.Baada ya kumaliza Viongozi hao wawili waliongozana na Mh. Lowasa kuelekea Musoma mjini. Msafara huo ulisimama tena Butiama na kufanya hivyo wakaenda na viongozi hao wote hadi mjini.

Walipofika mjini walijumuishwa na viongozi wa mjini akiwemo Mwenyekiti wa wilaya ya Mjini na mwengine aliyetambulishwa kama ndg. Mathayo ambaye ni kiongozi wa Ccm mkoa wa Mara.

Kikao kilifanyika katika hotel ya Matvilla ambayo inamilikiwa na Ndg.Mathayo (Mnec).katika kikao hicho wenyeviti wa wilaya kila mmoja alipewa maagizo ya kuonana na wajumbe wake na kuwapatia kiasi cha shilingi laki moja ikiwa ni sehemu ya kuwapa salamu za Ndg.Mgombea.Wao wenyewe wenyeviti na Wanec wakiondoka na shilingi Laki Tano kila mmoja.

Kikao hicho kilichochukua zaidi ya Lisaa kilijazwa na Jazba toka kwa Bwana Veda na Ndg.Mathayo wakiwalaumu wenyeviti na Wanec wao kulwa kuwa Vigeugeu kwa kubadilikabadilika jambo ambalo walipotoka walikuwa wanasema vipembeni kuwa ..huyu bwana hata Afya hana tutamsaidiaje."

Mimi nipo safarini naye.Ninaendelea wajuza kinachoendelea.Nifuate......
 
Leo majira ya mchana ndani ya maeneo ya Musoma mjini mkoa wa Mara tulipata ugeni.Na mgeni huyu sio mwengine ni Edwars Ngoyai Lowassa.ilikuwa ni ugeni wa ghafla na kwa kweli kwa ughafla wake tumejionea mengi.Kuanzia afya yake aliposaidia kushushwa na kupandishwa kwenye ndege na pili jinsi hela zilizochangwa juzi viwanja vya Hekima,Mikocheno Dar es salaam zilivyoanza kutumiwa.Mie ninawaletea safari nzima.

Baada ya kutua uwanja wa ndege majira hayo, Lowasa alipokelewa na Ndg.Veda Mathayo ambaye alimchukua hadi kwenye shamba lake huko Bunda ambapo alifanya naye mazungumzo alimkabidhi taarifa ya hali ya kisiasa ilivyo na ilivyobadilika ikiwemo kuwa Mjumbe wa Nec toka Bunda amekimbia Kambi na sasa anamuunga mkono Mh.Wassira pamoja na yeye ni Mnec na Mwenyekiti wa Butiama pia.

Lowasa ambaye alionekana kuchoka sana kiafya na nguvu za kutembea aliamua kuwatafuta wajumbe hawa.Akiwa njiani alisimama Bunda na kuongea na viongozi hao wa Bunda.Baada ya kumaliza Viongozi hao wawili waliongozana na Mh. Lowasa kuelekea Musoma mjini. Msafara huo ulisimama tena Butiama na kufanya hivyo wakaenda na viongozi hao wote hadi mjini.

Walipofika mjini walijumuishwa na viongozi wa mjini akiwemo Mwenyekiti wa wilaya ya Mjini na mwengine aliyetambulishwa kama ndg. Mathayo ambaye ni kiongozi wa Ccm mkoa wa Mara.

Kikao kilifanyika katika hotel ya Matvilla ambayo inamilikiwa na Ndg.Mathayo (Mnec).katika kikao hicho wenyeviti wa wilaya kila mmoja alipewa maagizo ya kuonana na wajumbe wake na kuwapatia kiasi cha shilingi laki moja ikiwa ni sehemu ya kuwapa salamu za Ndg.Mgombea.Wao wenyewe wenyeviti na Wanec wakiondoka na shilingi Laki Tano kila mmoja.

Kikao hicho kilichochukua zaidi ya Lisaa kilijazwa na Jazba toka kwa Bwana Veda na Ndg.Mathayo wakiwalaumu wenyeviti na Wanec wao kulwa kuwa Vigeugeu kwa kubadilikabadilika jambo ambalo walipotoka walikuwa wanasema vipembeni kuwa ..huyu bwana hata Afya hana tutamsaidiaje."

Mimi nipo safarini naye.Ninaendelea wajuza kinachoendelea.Nifuate......

WAMA at Work,mwaka huu mtachoka na lowassa,nao a membe anaid kujidhalilisha
 
Haya niko hapa pembeni nami nifuatilie ila usitudanganye sema kweli tupu ili wote tunufaike.
 
Picha za kupandishwa na kushushwa kwenye Ndege.?
 
Sijawahi kushuhudia Lowasa ameanguka jukwaani au akisaidiwa na glucose kupata nguvu ya kusimama na kuongea je anaeanguka majukwaani ba huyu Lowasa ni nani mgonjwa na aliyedhoofu?
 
Mods humu ndani naona sikuhzi nao wanamgombea,habri za majungu zinaletwa wao nao wanashangilia
 
kwahiyo utu wa wajumbe unadhalilishwa kwa kiasi cha tsh laki moja ?
 
Cha ajabu katibu tawala wa Mkoa akisaidiwa na Mnec wamefanikisha ziara mkoani humo, pia mkuu Wa wilaya musoma mjini na maandishi nguli wa itv wamepewa jukumu Hilo
 
Nishidaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa naomba abaki amuone mlisi wa JK 2015.
 
Kama uchaguzi wa ubunge 2010 Membe jimboni kwake alishinda kwa ushindi mwembamba wa 54% dhidi ya mgombea wa upinzani (aliepata 46% tena kwa kufanya kampeni ya chini ya mwezi na ni fukara wa kipato) aliemuwekea pingamizi mahakamani na pingamizi lake kutupwa baada ya kutaka kujitengenezea mazingira ya kupita bila kupingwa.Na katika ujumbe wa kamati kuu kuambulia nafasi ya sita na kuachwa nyuma na vijana wadogo kwenye medani ya siasa kama January Makamba,komredi Mwigulu Nchemba,Membe asitegemee chochote katika urais kwani sio size yake.
 
huyu mtu anaandamwa........akipata urais sijui jf itasalimika....
 
muamkapo,mtembeapo pia mlalapo Edward ngoyai lowassa mnalo mwaka wenu huu na jamaa huyo ikulu.
 
Mnataka kushindana kwa ugonjwa? WaTZ hamkosi vituko. Toka lini afya hupimwa kwa kuangalia mgonjwa mwingine wodini?
Sijawahi kushuhudia Lowasa ameanguka jukwaani au akisaidiwa na glucose kupata nguvu ya kusimama na kuongea je anaeanguka majukwaani ba huyu Lowasa ni nani mgonjwa na aliyedhoofu?
 
Back
Top Bottom